Je, ulokole una nafasi gani katika mahusiano?

if not now

Senior Member
Mar 4, 2017
186
171
Habari zenu wanaMMU,

Jioni ya leo ningependa tuweze kushiriki katika mada twajwa "Ulokole". Umekuwa ni mwiba kwa baadhi ya ndoa pia ulokole umeweza kuzisaidia ndoa nyingi. Mimi haswa nitazungumzia utumikaji vibaya wa ulokole katika ndoa.

Namquote Paulo katika 1Wakorintho 7:5 "Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, ili mpate faragha ya kusali; mkajiane tena, Shetani asije akawaharibu kwa kutokuwa na kiasi kwenu."

Ukweli ni kwamba asilimia kubwa ya watu waliokoka wanautumia Ulokole kama kisingizio cha kutokutimiza majukumu yao na hii husababisha mahusiano kati yao na wenza wao kuzorota na mwisho kufikia kuvunjika huku lawama zote wakimwangushia Shetani huku wanasahau kuwa wao wenyewe ndio chanzo cha tatizo.

Hivyo nawaomba walokole wenzangu mkaupitie huo mstari kwenye bibilia kupunguza wimbi kubwa la ndoa zilizovunjika na zinazoendela kuvunjika.

Matumaini yangu kwa namna moja ama nyingine sitakuwa nimemkwanza yeyote kwa Bandiko hili.

Shukrani wakuu
 
Mkuu upo huru kuongea chochote.
Ila huo mstari kwa kiasi fulani unatetea watu fulani wasio na ndoa kufanya kile kitendo pendwa bila ndoa, ili mradi muwe mmekubaliana
Kama mtu ataenda kusoma huo mstari mkuu lazima ataelewa nini Paul alikuwa anamaanisha, hapo yeye hazungumzi wale wasiokuwa na ndoa
 
Mkuu bado hujaweka wazi nini kinatokea kwenye mahusiano kama mtu ana ulokole...

Yaani habari haina cohesion...! Bado tatizo hujaliweka wazi...
Kweli mkuu jambo hili nimelizungumzia juu juu. Ni mambo mengi sana hutokea kwenye ndoa hasa za walokole... Nakumbuka juzi nilisoma habari kwenye mtandao (jina nimesahau) Mama mchungaji anamlalamikia mumewe kwa kutompa haki yake kwa takribani miaka mitatu... Just imagine unaishi na mume ndani mnamaliza miaka mitatu hajakugusa si huuaji huo,jana pia huku jf nimeona dada yetu mmoja akilalamika mumewe hajishughulushi na maswala ya familia wote wakitumia kivuli cha ulokole kutokutimiza majukumu yao.
 
Kuna uncle wangu mkatoliki mke wake kaokoka. Duh! Yule mama kuanzia J5 mpaka Jumapili anashinda kanisani na kurudi nyumbani saa 3 usiku. Mume anarudi home saa 12 jioni. Hajui mumewe anakula chakula gani au kama ana mahitaji mengine. Anasali kwa 'nabii' fulani hivi. Huyo nabii anaweza piga simu anytime akiomba usafiri in case gari yake ina matatizo. Aunt yangu ndiye anakuwa dereva. And when things go wrong you start cursing the poor devil. Kweli watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.
 
Hapa tayari ndoa ipo kwenye hati hati

Kuoa hawa wanaosali kwa manabii inahitaji moyo
 
Kama mtu ataenda kusoma huo mstari mkuu lazima ataelewa nini Paul alikuwa anamaanisha, hapo yeye hazungumzi wale wasiokuwa na ndoa
Si rahisi kuelewa mstari kama unavyofikiria! Ni bora uelezee tu. Kuna dini/imani kibao zimetoka kwenye hiyo biblia moja na sababu ni kwamba kila mtu anaielewa kitofauti. Ko tueleze ulivyoelewa wewe mkui
 
Back
Top Bottom