Prakatatumba abaabaabaa
JF-Expert Member
- Aug 2, 2022
- 1,465
- 4,675
Umaskini unatesa, umaskini unaaibisha sana, hakukosea aliyesema umaskini ni wa kuchukia na kukimbia, hakuna atakaye kujali mpaka utakapokua tajiri wazee.
Ukiwa maskini kwenye ukoo watakuona kama mpiga kelele tu, imagine mtu mzima 30's napata kipato cha laki nne kwa mwezi, sina kiwanja wala mke wala mtoto, najua kukata tamaa ni Mwiko lakini nawaza niingie vijiji vya mbeya huko labda naweza kupata mawazo mapya hata ya kilimo.
Sielewi kabisa, natembea kilometers moja kulifata kanisa, watu wamepaki magari nje mimi nipo nipo tu, kutoa zaka yenyewe ni mgogoro, watu wanajadili mipango na maendeleo ya kanisa, hawakushiriki kwa sababu wanajua huna uwezo wa kutoa. Mtaani napo watu wanakuchukulia poa tu, hasira zote hizi nimezipata baada ya mtu kunidharau waziwazi kwamba sina mbele wala nyuma Dah.
Kiukweli umaskini sio wa kuchezea, maisha haya yenyewe ni mafupi utajikuta unaishi kwa shida na stress sio poa.
N.B, kuna million 15 nataka niikope sehemu hebu nipeni ramani nianzie wapi niishie wapi, sina elimu yoyote ya biashara sijawahi kufanya biashara yoyote ile, nifanyaje kidogo niingie 40's nikiwa na kibanda?