Je, ukubwa anaopewa Mungu anaustahili?

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
26,215
56,855
Naomba niegemee ktk pande hizi mbili,Mungu wa kikristu na yule wa kiislamu.. kwangu Hawa ni Miungu wawili tofauti(sipo kulijadili hili), Msingi wa mada husika utaegemea ktk pande hizo mbili!.

Mungu amekuwa akihubiriwa kuwa na utukufu,uwezo na nguvu za ajabu!. Binafsi nimepata walakini kuhusu yeye!, Uwezo alionao ni Kama unakuzwa zaidi ya vile aviwezavyo!
Mfano imekuwa ikitajwa kuwa Mungu Ni muweza wa kila kitu Sasa je,Mungu anaweza kujipoka nguvu zake na uwezo wake na asiweze kuurudia..?

Kifikra ni vyema kuondosha mwiba barabarani kuliko kuuacha ili uje umche na mwengine!..
Ni ipi haja ya Mungu kumuacha shetani atese viumbe vya Mungu avipendavyo...? Kuna faida gani ya kuviweka viumbe viovu motoni Kama havikupunguzii ama havikuongezei chochote ktk utukufu wako maana Mungu ndo hitimisho la yote..?

Ni ipi faida ya kuwa na Mungu kwenye dunia yetu ikiwa shida tunazipata wakati hatujawahi kumuomba kutuumba kwetu..?
Kwanini anapewa sifa ya wema tu wakati hata huyo shetani muovu alitokea kwake ambapo Mungu ndio muanzilishi wa kila kitu,hii inamaanisha Mungu anasifa ya wema na uovu maana kwake ndio chanzo cha kila kitu na shetani aliitoa wapi asili ya uovu..? Kama asili ya uovu haitoki kwake Basi kuna asili nyengine tofauti na Mungu ambayo inasifa ambazo hazitoki kwake!

NB;Mimi ni Agnostic kwa maana ya sijui Mungu kuwa yupo au hayupo.. sababu za kuwepo au kutokuwepo kwake binafsi hazijakidhi!!
 
Hivi mtu unaweza kukaa na kufikiria kitu ambacho hujawahi kukiona? Yaani ukiambiwa utaje kitu ambacho hakipo utataja kitu gani?
Unajua huwezi kufikiria au kuwaza nje ya vitu ambavyo havipo either umeviona au kuvisikia.?
Kwa mantiki hiyo Mungu kama asingekuwepo hata wewe usingeweza kumuwaza. Mungu ana exist akili yako yalifahamu hilo ndio maana unamuwazia kua atakua hayupo.

Sawa Mungu inawezekana hana uwezo mkubwa kiasi hiki ambacho binaadamu tunamuona anacho. Je wewe unadhani ni sahihi Mungu anauwezo mdogo sana kwa jinsi unavyooona?
 
Mkuu umetoa hoja Nyepesi mno.
 
Nawe unahabari kuwa mazingira Yana affect namna ya kuwaza kwako..? Binadamu tunaamini kuwa kila tunachokiona kimetengenezwa!,hatuamini kuwa hakuna kilichokuwa tu pasipo ufanisi fulani!! Basi hii ndio chachu ya mwanadamu kufikiri kuwa yupo pia alieundwa tunavyoviona kuviskia n.k Sasa je,Ni kweli hayo yanafaa kuamini,kujua,kuidhinisha,kuthibitisha kuwa Mungu yupo..?

Navyoona anauwezo mdogo tofauti na anavyokuzwa! Huenda hata hawezi kujua yajayo ndio maana shetani akajitokeza.. kwani ukiangalia hakuna faida ya kumuacha shetani ambae atapindisha watu wengine waende motoni wkt anauwezo wa kumuondoa kabla ambapo shetani huyo asingeshawishi yoyote ili aende motoni!! Kupi kuna faida kumuacha au kumuondoa..?
Kuna nini cha muhimu kuwa motoni au peponi wakati hata tusipokuwepo hakumfaidishi Mungu..?
 
Hivi mtu unaweza kukaa na kufikiria kitu ambacho hujawahi kukiona? Yaani ukiambiwa utaje kitu ambacho hakipo utataja kitu gani?
Unajua huwezi kufikiria au kuwaza nje ya vitu ambavyo havipo either umeviona au kuvisikia.?
Kwa mantiki hiyo Mungu kama asingekuwepo hata wewe usingeweza kumuwaza. Mungu ana exist akili yako yalifahamu hilo ndio maana unamuwazia kua atakua hayupo.

Sawa Mungu inawezekana hana uwezo mkubwa kiasi hiki ambacho binaadamu tunamuona anacho. Je wewe unadhani ni sahihi Mungu anauwezo mdogo sana kwa jinsi unavyooona?

Spiderman na RANGO ushawahi waona kihalisia nje ya masimulizi yao?

Kwasababu majina yao yapo je hiyo inamaanisha kua wapo kihalisia?

It's Scars
 
Naomba niegemee ktk pande hizi mbili,Mungu wa kikristu na yule wa kiislamu.. kwangu Hawa ni Miungu wawili tofauti(sipo kulijadili hili), Msingi wa mada husika utaegemea ktk pande hizo mbili!.

Mungu amekuwa akihubiriwa kuwa na utukufu,uwezo na nguvu za ajabu!. Binafsi nimepata walakini kuhusu yeye!, Uwezo alionao ni Kama unakuzwa zaidi ya vile aviwezavyo!
Mfano imekuwa ikitajwa kuwa Mungu Ni muweza wa kila kitu Sasa je,Mungu anaweza kujipoka nguvu zake na uwezo wake na asiweze kuurudia..?

Kifikra ni vyema kuondosha mwiba barabarani kuliko kuuacha ili uje umche na mwengine!..
Ni ipi haja ya Mungu kumuacha shetani atese viumbe vya Mungu avipendavyo...? Kuna faida gani ya kuviweka viumbe viovu motoni Kama havikupunguzii ama havikuongezei chochote ktk utukufu wako maana Mungu ndo hitimisho la yote..?

Ni ipi faida ya kuwa na Mungu kwenye dunia yetu ikiwa shida tunazipata wakati hatujawahi kumuomba kutuumba kwetu..?
Kwanini anapewa sifa ya wema tu wakati hata huyo shetani muovu alitokea kwake ambapo Mungu ndio muanzilishi wa kila kitu,hii inamaanisha Mungu anasifa ya wema na uovu maana kwake ndio chanzo cha kila kitu na shetani aliitoa wapi asili ya uovu..? Kama asili ya uovu haitoki kwake Basi kuna asili nyengine tofauti na Mungu ambayo inasifa ambazo hazitoki kwake!

NB;Mimi ni Agnostic kwa maana ya sijui Mungu kuwa yupo au hayupo.. sababu za kuwepo au kutokuwepo kwake binafsi hazijakidhi!!
Ili uhoji utukufu wa Mungu kwanza unapaswa kujitoa katika kumwamini(kama mtoa Mada) kisha unajitengenezea maswali ya kumuhoji kulingana na sifa alizo kupitia vitabu vitakatifu vya wanaomwamini(waislamu na Wakristo) kisha unaanza kutafuta majibu yakupima utukufu wake na uwezo wake kulingana na mapungufu unayoyaona katika maswali yako, mwisho unajipa majibu ambayo huyatengenezea hoja na mada ili wengine wajue mtizamo wako, lakini mtizamo wa kwenye HAMNA, maana unacho hoji hujawahi kukiiona wala hakionekana na majibu yako yanakuwa from real world to mythical world, Je mtizamo wako unakuwa chanya??? Majibu yote anayo mtoa mada. Nafkiri nyakati hizi ingelikuwa vema kama huamini katika Mungu utafute kitu kingine cha kuamini kama mbadala wa Mungu, kisha unatengenezea sifa na utukufu kisha unavivika katika huyo mungu wako, vinigne ni Dogmatic haviwezi badilika ama badilisha mtizamo wa yule alieamua kufuata njia yake.
 
Mungu huenda akawepo ila sivyo tunavyomdhania! Unaweza ukafikiri mazingira hayakujui! Lkn yanakujua ndio maana unapata mahitaji yako toka kwenye mazingira! Tuzo moja wapo tuliyopewa na mazingira ni ufahamu(akili).. Kuna vitu vinatokea kwenye mazingira tunaona kama hatuja tendewa haki lkn kumbe ndio utimilifu wa mazingira!.. hatupendi kufa lkn kufa ni utimilifu wa mazingira
Jinsi mwanadamu anavyoviwazia vitu fulani vilivyo kumbe sivyo!.
Sifa ambazo tunavipa vile tuviitavyo Mungu huenda sivyo hasa tukiangalia weledi wa uhalisia! Kuna vitu tunavitenga kuwa si vya Kiungu(sio sifa za Mungu) wakati huohuo vitabu vimeandika Mungu ndio Alfa na Omega hakuna ambacho hakija toka kwake!! Kama uovu haujatoka kwake hii inamaanisha yeye si chanzo Cha kila kitu hivyo vitabu vyake vinajipinga!!
Sidhani tunavyomdhania Mungu kuwa alivyo ndivyo alivyo!!

Ukifatilia sana utagundua there is kind of laws in this universe we still don't know na ndio maana tunapata walakini ktk vyanzo vya Mungu nakuishia kujigubika ktk lindi la ati siri za imani!,ati yeye ndie Alfa na Omega!! Hili ni ombwe tulilojifunika and I think we can predict God by looking the universe and not blabla.
 
Naamini katika Logical Thinking, kuna vitu viko beyond nature and Natural laws, mtizamo wowote unategemea wapi unasimamia, huwezi kuwa scientologist ukawa unasimamia Utukufu wa Mungu, ni nadra sana, huyu huamini katika mabadiliko ya sayansi na teknolojia kung'amua maisha na mfumo mzima wa mwanadamu, hutengeneza theory kisha huzithibitisha kwa mfumo wa kisayansi, ikishindikana huacha iendelezwe na Wengine (Akina steph hawking, Aristotle na wengine).

Ukishakuwa Theist unakubali uwepo wa Mungu kwa kusimama katika Holy Dogmatic book with ability to learn, meditate and understand things about the universe in faithful belief ways. Apa ndio msingi wa Mtu kuamini katika Mungu huzaliwa, apa ndio msingi wa Imani na kuamini kuwa kuna Roho iliyo na nguvu huwapo katika mawazo na maisha ya mwanadamu, kuna vitu sayansi haiwezi kujibu vile vile kuna vitu katika Dogmatic Holy books haviwezi kujibika katika ulimwengu wa damu na nyama hadi uishi katika ulimwengu wa kiroho zaidi, unyambue mambo kuanzia Kiroho kuja kimwili, uanze kutafuta majibu kuanzia kiroho kuja kimwili, kila tatizo unalolikabili unaanza kulitazami kwenye ulimwengu wa Kiroho kuja kimwili, hapa ndipo huanza kupata majibu ya mambo mbalimbali na ndipo imani juu ya Roho yenye nguvu hutokea, Kuna vitu Nature na sayansi haviezi kujibika unto mpaka uishi kiroho zaidi ndipo utakapopata majibu yake.
 
Majibu yapi ya kiroho yanaweza jibu maswali yangu hapo juu..?
 
Kuna kitu kimoja Unatakiwa kukielewa kwamba ili umwelewe Mungu ni lazima ubadilike uwe kwenye nafasi ya kuweza kukaa umwelewe.Hata wengi walio katika dini Bado hawajamuelewa..Kuna namna binadamu alitakiwa awe aishi ndani ya ukaribu na Mungu kama samaki alivyo ndani ya maji ndivyo na binadamu alitakiwa asitoke Karibu na lile joto au ukaribu na Mungu.

Kukamilika binadamu hakupo kwa sababu binadamu anaishi chini ya kiwango alichotakiwa kuishi,,na anamdoubt Mungu kwa sababu anadhani anaweza kutumia akili zake kumwelewa.

Adam alipokuwa Eden Alikuwa darasani namna ya management ya dunia.At the same time Alikuwa kwenye nafasi sahihi ya kufundishwa.

Alipokula tunda aliondoka kwenye nafasi ya ukaribu na Mungu na pia alilikosa darasa la kumjua Mungu.
Na ndipo era ya kuishi kwa kutumia akili pekee ilipoanza.

Kwa hio mwandishi Mambo ya Mungu ukitaka kuyajua ni juhudi zako binafsi tu zinahitajika kumtafuta.Kumtafuta kama kitu cha thamani au kupata nafasi ambayo Utaweza kutengeneza relation nae.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi mtu unaweza kukaa na kufikiria kitu ambacho hujawahi kukiona? Yaani ukiambiwa utaje kitu ambacho hakipo utataja kitu gani?
Unajua huwezi kufikiria au kuwaza nje ya vitu ambavyo havipo either umeviona au kuvisikia.?
Kwa mantiki hiyo Mungu kama asingekuwepo hata wewe usingeweza kumuwaza. Mungu ana exist akili yako yalifahamu hilo ndio maana unamuwazia kua atakua hayupo.

Sawa Mungu inawezekana hana uwezo mkubwa kiasi hiki ambacho binaadamu tunamuona anacho. Je wewe unadhani ni sahihi Mungu anauwezo mdogo sana kwa jinsi unavyooona?
Changia mada mkuu Leo sijakuelewa na Leo hujatoa hoja yenye mashiko to a hoja nzito hapa ili tusaidiane kuelewa
 
Kuna kitu kimoja Unatakiwa kukielewa kwamba ili umwelewe Mungu ni lazima ubadilike uwe kwenye nafasi ya kuweza kukaa umwelewe.Hata wengi walio katika dini Bado hawajamuelewa..Kuna namna binadamu alitakiwa awe aishi ndani ya ukaribu na Mungu kama samaki alivyo ndani ya maji ndivyo na binadamu alitakiwa asitoke Karibu na lile joto au ukaribu na Mungu.

Kukamilika binadamu hakupo kwa sababu binadamu anaishi chini ya kiwango alichotakiwa kuishi,,na anamdoubt Mungu kwa sababu anadhani anaweza kutumia akili zake kumwelewa.

Adam alipokuwa Eden Alikuwa darasani namna ya management ya dunia.At the same time Alikuwa kwenye nafasi sahihi ya kufundishwa.

Alipokula tunda aliondoka kwenye nafasi ya ukaribu na Mungu na pia alilikosa darasa la kumjua Mungu.
Na ndipo era ya kuishi kwa kutumia akili pekee ilipoanza.

Kwa hio mwandishi Mambo ya Mungu ukitaka kuyajua ni juhudi zako binafsi tu zinahitajika kumtafuta.Kumtafuta kama kitu cha thamani au kupata nafasi ambayo Utaweza kutengeneza relation nae.

Sent using Jamii Forums mobile app
Bwana Loeb umo ndani kuna point kubwa sana ni namna tu ya kuzifafanua ila jibu halipo mbali na ukiyoandika.
 
Kuna kitu kimoja Unatakiwa kukielewa kwamba ili umwelewe Mungu ni lazima ubadilike uwe kwenye nafasi ya kuweza kukaa umwelewe.Hata wengi walio katika dini Bado hawajamuelewa..Kuna namna binadamu alitakiwa awe aishi ndani ya ukaribu na Mungu kama samaki alivyo ndani ya maji ndivyo na binadamu alitakiwa asitoke Karibu na lile joto au ukaribu na Mungu.

Kukamilika binadamu hakupo kwa sababu binadamu anaishi chini ya kiwango alichotakiwa kuishi,,na anamdoubt Mungu kwa sababu anadhani anaweza kutumia akili zake kumwelewa.

Adam alipokuwa Eden Alikuwa darasani namna ya management ya dunia.At the same time Alikuwa kwenye nafasi sahihi ya kufundishwa.

Alipokula tunda aliondoka kwenye nafasi ya ukaribu na Mungu na pia alilikosa darasa la kumjua Mungu.
Na ndipo era ya kuishi kwa kutumia akili pekee ilipoanza.

Kwa hio mwandishi Mambo ya Mungu ukitaka kuyajua ni juhudi zako binafsi tu zinahitajika kumtafuta.Kumtafuta kama kitu cha thamani au kupata nafasi ambayo Utaweza kutengeneza relation nae.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanini kuwe na haja ya Mimi kumtafuta yeye wakati sikuwahi kumuomba aniumbe..? Kwakuwa sikumuomba aniumbe na akaniumba hili linaonyesha kuwa yeye ndo anashida na sisi!,hivyo yafaa yeye kututafuta sisi..

Kimantiki kosa la Adam kuumiza mpaka binadamu wengine unaona li sahihi..? Kivipi..?

Mi naona ni Kama vile nyie ndio hamumuelewi huyo Mungu!
Mungu yupo ktk pande zote mbili wema na uovu hakuna cha kumtenga! Na ndio maana hilo tunda la uovu hakuumba shetani bali Mungu huyohuyo na kwakuwa imeandikwa kuwa kamuumba binadamu kwa mfano wake hata ulaji wa tunda hilo binadamu katimiza sifa za muumba wake!! Mzunguko ni uleule..
Huwezi kukubali kuwa Mungu kaumba kila kitu Kisha ukatae uovu haukutoka kwake! Kwani itakuwa si muumba wa kila kitu.

Kwanini Mungu mnamuweka ktk picha ya kuabudiwa tu..? Hana Mambo mengine ya kufanya..? Kabla hajaumba wa kumuabudu alipungukiwa nini mpk kutaka kuabudiwa..?
Kama alivyoviumba vinatoka kwake vyote,shetani, binadamu,malaika n.k Kuna haja ipi ya kuadabisha vikikosea wakati vinatoka kwake pasi na uovu..?
Hili tendo mi nalishangaa maana Ni sawa na kucheza gemu! Unajinyofoa ktk uwezo wako unaunda kitu kutoka ktk sifa zako kisha kikienda hovyo unakiadhubu!!!!!!!!!!! Sijui kama unanielewa na ukiweza kunielewa hapa utaona upuuzi uliopo hapo hadi ninaona kuwa Mungu anavyotafsiriwa sivyo inavyotakiwa..
 
Kitabu kipi ni kitakatifu kati ya hivi viwili?
Kimoja kinasema Yesu Kristo alisulubiwa kingine kinasema hakusulubiwa.
Kimoja kilisema Ngamia ni najisi kingine hakikuwahi kusema hivyo.
Kimoja kinasema hata majini wako wazuri kingine hakikubali hivyo
Tofauti ziko nyingi sana,hizi ni baadhi tu

Kwa nini pia umechagua hivi viwili tu na kuviita vitakatifu wakati kuna vitabu vingine vya dini nyingine?
Ili uhoji utukufu wa Mungu kwanza unapaswa kujitoa katika kumwamini(kama mtoa Mada) kisha unajitengenezea maswali ya kumuhoji kulingana na sifa alizo kupitia vitabu vitakatifu vya wanaomwamini(waislamu na Wakristo) kisha unaanza kutafuta majibu yakupima utukufu wake na uwezo wake kulingana na mapungufu unayoyaona katika maswali yako, mwisho unajipa majibu ambayo huyatengenezea hoja na mada ili wengine wajue mtizamo wako, lakini mtizamo wa kwenye HAMNA, maana unacho hoji hujawahi kukiiona wala hakionekana na majibu yako yanakuwa from real world to mythical world, Je mtizamo wako unakuwa chanya??? Majibu yote anayo mtoa mada. Nafkiri nyakati hizi ingelikuwa vema kama huamini katika Mungu utafute kitu kingine cha kuamini kama mbadala wa Mungu, kisha unatengenezea sifa na utukufu kisha unavivika katika huyo mungu wako, vinigne ni Dogmatic haviwezi badilika ama badilisha mtizamo wa yule alieamua kufuata njia yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vit
Kitabu kipi ni kitakatifu kati ya hivi viwili?
Kimoja kinasema Yesu Kristo alisulubiwa kingine kinasema hakusulubiwa.
Kimoja kilisema Ngamia ni najisi kingine hakikuwahi kusema hivyo.
Kimoja kinasema hata majini wako wazuri kingine hakikubali hivyo
Tofauti ziko nyingi sana,hizi ni baadhi tu

Kwa nini pia umechagua hivi viwili tu na kuviita vitakatifu wakati kuna vitabu vingine vya dini nyingine?

Sent using Jamii Forums mobile app
vitabu viko vingi tu, hata unaweza andika chako ukakipa utakatifu wako kupitia mungu wako unayemwamini na ukawa unakisalia, nimetumia dini hizo mbili kama kielelezo cha mada yangu na unaweza tumia na vingine kama kielelezo cha mada yako, mtoa mada Aligusa engo hizo nami nikamjibu kupitia engo hizo hizo.
Na Kuwepo wa Dini na miongozo tofauti ni hiyari ya mtu katika kipi akiishi na akifuate, ukishindwa unasimama katikati hakuna atakayekuhoji, ukizidiwa shika mawili, moja likikuponyoka okota endelea nalo maadam kwako linakufaa endelea nalo tu. Wakati mwingine hutakiwi ku complicate maisha kijana, unadhani huelewi ama dini hizi zinakuchanganya, unaachana nazo tu unatengeneza njia yako ktk kumwamini anayekupa nguvu, maarifa na kukubariki Unaweza Abudu Mbuzi, ng'ombe, kondoo, nyoka, chuma na hata Jua yote kwa yote ni majibu na msimamo wako katika kile unachokiamini na maisha yanaenda fresh tu kama mvua inavyonyesha katika paa za wachawi, wazinzi, na wema bila kubagua wala kuchagua.

"EVERY BELIEF HAS ITS PRICE, SO BE READY TO PAY FOR IT, DIRECTLY OR INDIRECTLY."
 
Back
Top Bottom