Chabruma
JF-Expert Member
- Sep 19, 2013
- 5,660
- 1,777
Naam,
Huu ni wimbo ambao ulikuwa mtamu sana kwenye vinywa vya wabunge na viongozi wa UKAWA. Kila kona walikuwa wanaimba kuwa Magufuli hatekelezi Ilani ya CCM bali ya UKAWA.
Walipita kwa wananchi na kwenye vyombo vya habari ikiwemo social media wakiimba wimbo huo. Kwa bahati mbaya zaidi, vijana wao mitandaoni na wao wakaanza kuuimba bila kutafakari.
Hata hivyo, kwa zaidi ya wiki tatu sasa, wimbo huo sijausikia ukipigwa kwenye media. Sina hakika na kilichotokea. Ila kwa vile watunzi wa wimbo huo hawajatueleza kuwa wimbo umepigwa marufuku, naamini kuwa bado wanaendelea kuuimba japo kwenye kumbi za starehe.
Kama ninachokisema ni kinyume chake, basi na mjitokeze mseme kuwa sasa Rais Magufuli ameachana na Ilani yenu na sasa anatekeleza Ilani ya CCM.