Je, Twitter wana double standard?

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,889
Hawa Twitter wamemfungia Trump account wakitoa sababu kuwa anahatarisha usalama na kunajisi demokrasia. Lakini Hiyo hiyo Twitter imekuwa inawaacha wanaharakati wa Afrika hata kama watawala wake wanapiga kelele kuwa wanahatarisha amani za nchi zao.

Nani amewapa uwezo wa kuhukumu kuwa huyu ni Mwanaharakati na huyu anahatarisha Usalama?
 
Bwana, Marekani uchaguzi umefanyika na mshindi amepatikana na aliyekuwa analalamika alipewa fursa zote athibitishe hujuma akashindwa, sasa bado mnataka kutuambia nini hapo.

Hapa uchaguzi tu haukufanyika na Magufuli akajitangaza mshindi kwa mtutu wa bunduki na hakuna anayeruhusiwa kupinga kwa njia yoyote ile, sasa hapo mtatuambia nini.

Hivyo Twitter wako sahihi kwa asilimia mia moja. Marekani wanaongozwa na rais kwa kufuata sheria na mfumo wa kidemokrasia, sisi tunatawaliwa na "Warlord", sheria zote zimo mdomoni mwake.
 
Wasiwasi wangu mkubwa ni madikteta wetu kutumia tukio walilofanya Twitter kuweka mbinyo kwenye mitandao kwa kisingizio cha usalama wa nchi.

Hata kama ilionekana wazi Trump anaharibu Twitter hawakutakiwa kujihusisha. Kitendo chao ni pigo kwa uhuru wa kujieleza na demokrasia. Wangekaa kimya kama ambavyo hukaa kimya watu wakiwa na harakati huku kwetu.
 
Twitter siyo mali ya serikali wala haiendeshwi kwa kodi za wanarekani, hivyo wana maamuzi yao.

Kama Founders wa Twitter na wanahisa wao hawaoni tatizo, then it's okay.

Hilo ndio soko huru.
 
Hawa Twitter wamemfungia Trump account wakitoa sababu kuwa anahatarisha usalama na kunajisi demokrasia. Lakini Hiyo hiyo Twitter imekuwa inawaacha wanaharakati wa Afrika hata kama watawala wake wanapiga kelele kuwa wanahatarisha amani za nchi zao.

Nani amewapa uwezo wa kuhukumu kuwa huyu ni Mwanaharakati na huyu anahatarisha Usalama?
Walishafika bei, na tajiri wao kikwazo chake ni Trump, ila Marekani itajuta kumkosa Trump.
 
Twitter siyo mali ya serikali wala haiendeshwi kwa kodi za wanarekani, hivyo wana maamuzi yao.

Jama Founders wa Twitter na wanahisa wao hawaoni tatizo, then it's okay.

Hilo ndio soko huru.
Hata kama ni biashara binafsi lakini wanawajibu wa kuwa na usawa katika utendaji wao kazi. Jamaa mmoja aliwahi sema kuwa, ili kulinda uhuru wa habari hata wazushi wanatakiwa kulindwa. Twitter naona kama walikurupuka kuingilia ile ishu. Halafu twitter wanainfluence kubwa sana. Jambo walilofanya limerudisha nyuma sana uhuru wa kujieleza.
 
KWANZA muelewe haya madude Sijui Twiter..Instagram..Facebook n social media zingine zote ziko kwenye chain moja Establishment....Kikundi Hiki hakimtaki Rais asietii Maelekezo yao.

TRUMP Jeuri hakutii maelekezo ya Kuipiga Syria Wauze Silaha na deal zingine kubwa kubwa...Haijaipiga Iran Wauze Silaha..Kasema Mauaji ya Libya na Huko Kwingine Iraq ilikua ni uongo na Uzushi..anaondoa wanajeshi huko Afghan na kwingineko unadhani watampenda???

BAHATI mbaya hata hawa watu mnaonyeshwa kwamba Wamevamia lile jengo hawajahoji hata mmoja ile ni sanaa..Mbona maandamano ya Black Lives Matter waliwahoji wandamanaji hapa kuna nn wasihoji??.

MEDIA Hii hii iliwahi kuonyesha maandamano ya huko India kwamba ndio yako Libya ni hawa hawa wanaotulazimisha Kwamba tuchanjwe corona hawa watu wabaya sana hawa....

Wanadeal na Trump kwasababu tu hajatii maelekezo yao hamna lingine....Mtu amepata kura mil 76 utasemaje hakubaliki???

Hao mil 76 wote ni wamarekani je ni vichaa???

Hapa ndio man naamini wamechakachua hizi kura ili Trump atoke...Walikua na lao jambo...
 
MIPANGO yao Miovu dhidi ya Trump Itakuja kujulikana hata Powell alipoongopa kwamba Iraq kuna silaha za maangamizi wakaua watu kwa mamilion kwa uongo kabisa baadae akakiri ilikua uongo lakin yupo na ameshiriki mauaji ya watu wengi achilia mbali kuharibu nchi ile kabisa kwa uzushi tu...walifanya hayo Libya pia..wamefanya kote duniani.
 
KWANZA muelewe haya madude Sijui Twiter..Instagram..Facebook n social media zingine zote ziko kwenye chain moja Establishment....Kikundi Hiki hakimtaki Rais asietii Maelekezo yao.

TRUMP Jeuri hakutii maelekezo ya Kuipiga Syria Wauze Silaha na deal zingine kubwa kubwa...Haijaipiga Iran Wauze Silaha..Kasema Mauaji ya Libya na Huko Kwingine Iraq ilikua ni uongo na Uzushi..anaondoa wanajeshi huko Afghan na kwingineko unadhani watampenda???

BAHATI mbaya hata hawa watu mnaonyeshwa kwamba Wamevamia lile jengo hawajahoji hata mmoja ile ni sanaa..Mbona maandamano ya Black Lives Matter waliwahoji wandamanaji hapa kuna nn wasihoji??.

MEDIA Hii hii iliwahi kuonyesha maandamano ya huko India kwamba ndio yako Libya ni hawa hawa wanaotulazimisha Kwamba tuchanjwe corona hawa watu wabaya sana hawa....

Wanadeal na Trump kwasababu tu hajatii maelekezo yao hamna lingine....Mtu amepata kura mil 76 utasemaje hakubaliki???

Hao mil 76 wote ni wamarekani je ni vichaa???

Hapa ndio man naamini wamechakachua hizi kura ili Trump atoke...Walikua na lao jambo...
Japo mengi hapo sikubaliani na wewe lakini umeongea point moja muhimu. Ni hawa Twitter na wenzao ndiyo huwapa waasi wa Syria, wale wa Libya nk platform ya kusemea lakini leo wamemnyima Trump. Siyo double standard hizi. Wanawaambia nini watu wengine? Kuwa uhuru wakujieleza ni kiini macho tu?
 
Hata kama ni biashara binafsi lakini wanawajibu wa kuwa na usawa katika utendaji wao kazi. Jamaa mmoja aliwahi sema kuwa, ili kulinda uhuru wa habari hata wazushi wanatakiwa kulindwa. Twitter naona kama walikurupuka kuingilia ile ishu. Halafu twitter wanainfluence kubwa sana. Jambo walilofanya limerudisha nyuma sana uhuru wa kujieleza.
Wana wajibu kwa mujibu wa nini ???
 
  • Thanks
Reactions: tyc
Kwa mujibu wa jamii, Corporate social responsibility.
Uhuru wako unaishia pale unapoanza uhuru wa mwenzio.

Sasa wale ni Twitter na uhuru wa maamuzi yao na sioni kama wamevunja sheria yoyote.

Tatizo kubwa la Trump ni ku-radicalise wafuasi wake. Mifumo yote ya kutafuta haki iko wazi na Trump kaitumia yote bila mafanikio.

Anachotaka kufanya ni mapinduzi haramu. Marekani ingekuwa anavyotaka yeye wala hata yeye asingekuwa Rais.

Maana popular votes alishinda Hillary huku yeye akiponea kwenye electoral votes ( kura ambazo kabla hajawa Rais alikuwa anazipinga ) lakini Hillary na Obama walimkabidhi Ikulubkwa amani kabisa bila kinyongo.

Keo yeye kapigwa tena both popular votes na electoral college lakini bado anakaza tu.

Mtu wa hivyo hawezi kuwa na Jema.
 
Bwana, Marekani uchaguzi umefanyika na mshindi amepatikana na aliyekuwa analalamika alipewa fursa zote athibitishe hujuma akashindwa, sasa bado mnataka kutuambia nini hapo.

Hapa uchaguzi tu haukufanyika na Magufuli akajitangaza mshindi kwa mtutu wa bunduki na hakuna anayeruhusiwa kupinga kwa njia yoyote ile, sasa hapo mtatuambia nini.

Hivyo Twitter wako sahihi kwa asilimia mia moja. Marekani wanaongozwa na rais kwa kufuata sheria na mfumo wa kidemokrasia, sisi tunatawaliwa na "Warlord", sheria zote zimo mdomoni mwake.
Mifumo ya uongozi inatokana na kuendana na watu wenyewe walivyo.
 
Uhuru wako unaishia pale unapoanza uhuru wa mwenzio.

Sasa wale ni Twitter na uhuru wa maamuzi yao na sioni kama wamevunja sheria yoyote.

Tatizo kubwa la Trump ni ku-radicalise wafuasi wake. Mifumo yote ya kutafuta haki iko wazi na Trump kaitumia yote bila mafanikio.

Anachotaka kufanya ni mapinduzi haramu. Marekani ingekuwa anavyotaka yeye wala hata yeye asingekuwa Rais.

Maana popular votes alishinda Hillary huku yeye akiponea kwenye electoral votes ( kura ambazo kabla hajawa Rais alikuwa anazipinga ) lakini Hillary na Obama walimkabidhi Ikulubkwa amani kabisa bila kinyongo.

Keo yeye kapigwa tena both popular votes na electoral college lakini bado anakaza tu.

Mtu wa hivyo hawezi kuwa na Jema.
Kosa la kutowajibika kwa jamii siyo mpaka uvunje sheria.
Nakubaliana kuwa Trump hana madai ya msingi lakini Twitter walichofanya ni double standards. Na kitapoteza imani ya watu kwao na kuwapa wengine sababu ya kufungia mitandao. Kwa nchi zingine wamewaacha watu waseme hata kama wataitisha maandamano nk, tukaamini hawa wanadimamia uhuru wa kujieleza lakini DT wamemfunga fasta.
 
Nchi nyingine kama zipi ??

Kama unamaanisha Afrika: Huku hakuna mifumo ya kutafuta haki, hata maandamano ya amani yanakatazwa, sasa mfano Tanzania mtu aitafute vipi haki yake akiona kaonewa ???
 
KWANZA muelewe haya madude Sijui Twiter..Instagram..Facebook n social media zingine zote ziko kwenye chain moja Establishment....Kikundi Hiki hakimtaki Rais asietii Maelekezo yao.

TRUMP Jeuri hakutii maelekezo ya Kuipiga Syria Wauze Silaha na deal zingine kubwa kubwa...Haijaipiga Iran Wauze Silaha..Kasema Mauaji ya Libya na Huko Kwingine Iraq ilikua ni uongo na Uzushi..anaondoa wanajeshi huko Afghan na kwingineko unadhani watampenda???

BAHATI mbaya hata hawa watu mnaonyeshwa kwamba Wamevamia lile jengo hawajahoji hata mmoja ile ni sanaa..Mbona maandamano ya Black Lives Matter waliwahoji wandamanaji hapa kuna nn wasihoji??.

MEDIA Hii hii iliwahi kuonyesha maandamano ya huko India kwamba ndio yako Libya ni hawa hawa wanaotulazimisha Kwamba tuchanjwe corona hawa watu wabaya sana hawa....

Wanadeal na Trump kwasababu tu hajatii maelekezo yao hamna lingine....Mtu amepata kura mil 76 utasemaje hakubaliki???

Hao mil 76 wote ni wamarekani je ni vichaa???

Hapa ndio man naamini wamechakachua hizi kura ili Trump atoke...Walikua na lao jambo...
Dah mkuu, yani huwezi amini hakuna raisi ambaye niliwahi kumfatilia nje ya tz zaidi ya Trump, Jamaa alikuwa raisi kweli kweli na kafanya makubwa ila media haitangazi.
 
Unajua mitandao mikubwa ya kijamii imekuja duniani kama miaka 15 iliyopita. Bahati nzuri au mbaya tukaichukulia kama vyombo vingine vya habari mfano magazeti, televisheni na redio. Tukatunga sheria za kudhibiti maudhui (Contents) yake huku tukisahau jambo la msingi sana kuliko yote: Mitandao ya kijamii kama Twitter, Facebook, Instagram, Tik-Tok, Snap-Chat na Telegram haiko kama vyombo vingine vya habari ambavyo huendeshwa na wahariri.

Mitandao ya kijamii hutofautiana kabisa na vyombo katika yafuatayo:
-Mitandao ya kijamii iko kwenye mikono ya ummah (They Belong to public domain),

-Mitandao ya kijamii huwezesha mawasaliano ya papo kwa papo (Enables Prompt and Instantaneous communication),

-Mitandao ya kijamii ni bahari ya mawazo na maudhui isiyo na mwisho (It's an infinite sea of ideas and contents)

-Mitandao ya kijamii kwasababu ya TEHAMA haina mipaka ya kijiografia (ICT enables the Social Media to have no geographical boundaries)

-Mitandao ya kijamii huwakikishia watumiaji kutofahamika kirahisi (Users Privacy is dully guaranteed)

Hivyo mitandao ya kijamii ikiendeshwa na TEHAMA, mbali kabisa na kuwasiliana imetengeneza ulimwengu mpya kabisa ambao sehemu kubwa ya maisha ya wanadamu hufanyika. Naweza kusema kwenye ulimwengu huu mpya (Cyberspace) asilimia 70% ya maisha ya vijana wa leo (millenials) huendeshwa huko: Iwe ni elimu, burudani, biashara, kazi za kiofisi au maisha ya nyumbani. Hivyo katika hii mitandao hutakuta mawasiliano tu, bali ramani nzima ya maisha ya watumiaji(An Entire life Puzzle of Users), mitandao kama Twitter, Instagram, Facebook, nk ni vyombo muhimu sana ambavyo vina nguvu iliyomithirika (They posses an Unprecedented Power).

Sasa palipo na watu wengi hapakosi kuwa na matukio mengi: Hivi vyombo vinaweza kutumika vibaya hata kuhatarisha amani na usalama wa dunia nzima. Wataalamu wa Propaganda wa karne zilizopita kama Sir Alfred Tennyson, George Orwell, Joseph Goebbels na Mao Zedong wangepata vyombo muhimu kaa mitandao ya kijamii basi nadhani wangefanya mambo ya ajabu kuliko hata yale ambayo tunayasoma kwenye vitabu. Mashirika ya kijasusi kama The Gestapo, The K.G.B, The Stasi na The S.S, yangekuwepo kipindi hiki basi nadhani maisha ya mamilioni ya watu wengi yangekuwa rehani.

Kusema kwamba vyombo kama Twitter, Facebook, Instagram, Telegram nk havihusiki sana na maisha ya wanadamu kwasababu vyenyewe hutoa tu Platform lakini maudhui ni ya watumiaji, nadhani tutakuwa tunajidanganya sana na kuna siku tutakuja kuangalia nyuma na kusema laiti tungejua. Hili suala linaathiri maisha ya dunia nzima, hivyo ni lazima dunia nzima ijipange kulikabiri: Tutengeneze sheria za kudhibiti matumizi ya hivi vyombo, tusiwaachie wamiliki kujifanya wanachokitaka (They are in a position of power), tusiziachie serikali zikaamua kujifanyia zinavyotaka na pia tusiwaachie raia watumie wanavyotaka. Mpaka leo hakuna mkataba wowote mkubwa wa kimataifa au kikanda ambao unazungumzia matumizi salama ya TEHAMA na Mitandao ya kijamii. Hili ni ombwe kubwa ambalo inabidi lijazwe na wataalamu hasahasa kutokea Afrika kwasababu sisi ndiyo wahanga wakubwa.

Twitter, Facebook na WhatsApp zinageuzwa kuwa silaha kama ambavyo vyombo vikubwa kama The Washington Post, The New-York Times, The Economist, The Pravda, Radio Free Europe nk vilitumika kuwa silaha za kufanyia uhandisi wa jamii (Weapons of Social Engineering) kipindi cha vita baridi. Nadhani ifike mahali viangaliwe kwa undani na vidhibitiwe, bila hivyo kuna kilio kikubwa sana huko mbeleni.

The Harvard Business Review mwaka jana waliandika Article nzuri sana na kusema kwamba kila mtumiaji wa mitandao ya kijamii anayetumia TEHAMA ni lazima amiliki kifaa maalum ambacho kitakuwa kimesajiliwa na kinafahamika kwamba ni chake kwasababu kitakuwa na saini yake mtu huyu ambayo iko kielekronikali (Virtual Signature). Hivyo hata umiliki akaunti mia ukiandika kitu fulani lazima tutajua wewe ni nani. Lakini wameandika jinsi ya kuzuia uhalifu wa mtandaoni, hawakuandika jinsi ya kudhibiti hawa wamiliki wanaouuza taarifa za watumiaji kwa serikali na makampuni ya kibiashara. Wamiliki wanawajibika kwenye suala za maudhui tu, kitu ambacho mimi nadhani siyo sawa kabisa.
 
Dah mkuu, yani huwezi amini hakuna raisi ambaye niliwahi kumfatilia nje ya tz zaidi ya Trump, Jamaa alikuwa raisi kweli kweli na kafanya makubwa ila media haitangazi.
Trump ni mtu...Amefanya kazi nzuri sana..Ngoja muone kale kazee kanakuja kuharibu balaa
 
Back
Top Bottom