Je tuhahitaji tena Ze Utamu?

Status
Not open for further replies.
Ndugu wana JF,
Nimesikitishwa sana na mapicha machafu katika website hiyo ya zeutamu. Leo hii ni mara yangu ya kwanza kuisikia na kuitembelea, ukweli nimesikitishwa kupita kiasi. Mantiki sioni kwanini inaitwa zeutamu bali nadhani inapaswa kuitwa zeuchafu.

Kama Mtanzania na Mwafrica niliyelelewa kwa kufuata mila na desturi sikubaliani hata kidogo kuwepo kwa website hiyo kwani iko kinyume kabisa na maadili ya kikwetu.
Pamoja na uhuru wa vyombo vya habari lakini kwa hii website naona tumekwenda mbali sana na ninaiomba serikali itumie kila njia kuifungia website hiyo mara moja na muhusika achukuliwe hatua za kisheria kwa kuwachafua watu mbali mbali ndani na nje ya Tanzania.

Kwa utaalamu wangu mdogo wa computer nitajaribu kusaidia kumwaanika muhusika ikiwa ni pamoja kutafuta IP address yake, na anuani yake kamili ili aweze kushughulikwa mara moja.

Nimesikitishwa kupita kiasi na uchafu huo.
 
LOL!!! Eti kinyume na maadili ya mtanzania.... wake up my bro this is not the TZ of 1960, waTZ hawana maadili anymore and by inlarge this has been coz'd by the very same ppl who this photos potray, acheni unafiki, eti maadili... madili ya mTZ ni kuwa na nyumba ndogo, kushinda kwenye ma-guesthouse, kuua kwa ushirikina, kutafuta au kutoa hongo na rushwa au shortcut za maisha kama EPA, Richmond, etc, hao tulio wategemea nakuwaweka madarakani kulinda "maadili" ya kiTZ ndiyo wametufikisha hapa...halafu leo tunakaa tunasikitika hii picha...acheni unafiki bwana!!!!
 
Mwanakijiji na Wana JF.

nILISHAWAHI KUCHANGIA HAPA JF NIKASEMA TATIZO LETU NI UHURU USIOKUWA NA MIPAKA TUKIO HILI NI LA AIBU NA LAKUSIKITISHA KWA MARA YA KWANZA NIMEPATA TAARIFA HIZI JANA SAA 12 JION MPAKA KUFIKIA LEO SAA 4 ASUBUHI USHENZI HUO ULIKUWA BADO UPO HEWANI,MIMI SI MTAALAMU WA IT,NAILICHUSHINDWA KUELEWA WATU WA USALAMA WAMESHINDWA KUIHARIBU BLOG HIYO?NA KUENDELEA KUICHA MPAKA MUDA HUO ZAIDI YA MASAA 16?

HILI NI TUKIO LA AIBU MARA YA KWANZA ULIPO POST HAPA KUHUSU MAGAZETI YA UDAKU NILIWEZA KUONA HATARI HII LEO RAIS WETU AMEDHALILISHWA NAMNA HII ANASIKITISHA,KUNA UMUHIMU WAKUANGALIA UPYA SERA,SHERIA ZETU ZA HABARI NA MAWASILIANO SI AJABU UTAKUTA KESHO NA KESHOKUTWA KUNA MTANZANIA ANTUMIA PICHA HIYO KATIKA SCREEN YA SIMU YAKE NA ANAONA SAWA TU KAMA WENGI WALIVUKUWA WANAWEKA PICHA YA AINA HIYO ILIYOKUWA INAMUONYESHA RAIS BUSH NA OSAMA KTK HALI KAMA HIYO.

HII NI HATARI AMABAYO ILIANZA KATIKA MAGAZETI YA UDAKU KUWEKA WATU UCHI KWA HOJA KUWA WANAREKEBISHA TABIA,LEO UNAWEZA KUKUTA MPUMBAVU HUYU ALIKUWA ANATAFUTA UMAARUFU ILI BLOG YAKE IPATE JINA BILA KUJUA ANADHALILSHA TAIFA NA WATU WAKE,MTU HUY AKIPATIKA ANYONGWE NA MSHENZI ASIEFAA KTK JAMII
 
Pamoja na kwamba ile picha inatia kinyaa, itakuwa ni kupoteza wakati na resources kuwatafuta ili washughulikiwe. Labda atafutwe host wa ile website ili amuamrishe mwenye website aifute. Lakini sidhani kama kuna namna ya kuwachukulia hatua. Ndiyo ukweli wa www. It is a jungle na tutakutana na mengi tusiyopendezwa nayo. Dawa ni kuwadharau ili mradi yanabaki huko huko kwenye www. Sasa hao wanaodownload na kutumiana kwenye simu.........

Amandla.........
 
Duh yaani hata kama angekuwa amekosea kimaadili namna hiyo si vizuri wala adabu kumfanyia hivi. Huyu ni mzazi wetu, kiongozi wetu hastahili haya. Ni viongozi wangapi wenye maskendo machafu na hatujawahi kuona wakiadhibiwa namna hii? Hivi mzazi wako (baba, mama) afanye madudu unaweza kumwadhibu kwa staili hii?achilia mbali kumwadhibu?. Maadili yetu kama watanzania yako wapi?

Wanadai ni mtambo wa kurekebisha Tabia, ni tabia gani wanazorekebisha?. Ni picha ya kutengeneza ndio lakini bado inamdhalilisha huyu kiongozi wetu ambaye pia ni baba wa wenzetu, mume wa mama yetu, ndugu wa watu.

Achukuliwe hatua amevuka mipaka, minyau na mipusi yote.
 
Actually jamaa anaturudisha enzi za Mzee PUNCH. Lakini hii ni too much! Kwanza ni kinyume na maadili ya kiafrika na kitanzania kwa ujumla pili ni kitendo cha udhalilishaji ambao ni kinyume na haki za binadamu tatu ni kumkosea heshima mkuu wa nchi ambapo jamaa akikamatwa nadhani hata mkuu wa kaya mwenyewe atamfanya asusa achilia mbali hao makachero. Ze Utamu hii inashabikiwa sana na akina dada na akina baba ambao hawajatulia. Ni mtandao ambao kama mitandao mingine miovu inamsifia na kumwabudu shetani.
 

Nakubaliana na we kabisa hatuna maadili lakini nafikiri inapaswa pia kukumbuka kuwa mtu huadhibiwa kulingana na kosa alilofanya. Tunaequate uhuru na democrasia za Marekani na nchi nyingine lakini tunasahau kuwa wao pia wana limit kwa maana ya kwamba unaadhibu with evidence. Mf. Issue ya Clinton na Monica Lewinsky vikatuni, picha zilichorwa kupotray issue ile kwa maana ya kwamba walimchora akiwa katika lile tukio au lolote lingine linalopotray issue ile but kwa huyu je amefanya lolote kufanana na picha hiyo? lolote ambalo tuna proof nalo? Nisingeumia wala kusema lolote kama ningekuta ametolewa akibebwa na mtu aliyelabiwa kama fisadi au kitu kama hicho akiwa na nguo zake but not vile.

Jiweke wewe kwenye nafasi ya mtoto wake, mkewe, mjukuu wake au hata mzazi wake kama kujivika utanzania kumekushinda.
 

Gembe, nimeona kwa macho yangu hiyo picha hiyo CHAFU! Ingawa kuna wanaopenda picha za ngono, binafsi nachukia picha za namna hiyo kwa vile zinavunja heshima na maadili. Na kwa hii, kwa kweli inasikitisha. Inaonyesha ni jinsi gani uhuru wetu umegeuka kuwa wendawazimu!
 
Wana JF!

Hii inasikitisha!

Jamani heshima iko wapi kwa Mkuu Wetu?

Ndio uhuru gani wandugu usiokuwa na mipaka?

Can some one do something ikaondolewa???
 
Uchunguzi wangu wa haraka haraka inanionesha huyu jamaa anayejiita zeutamu
anapatika USA, state ni texas na city ni Houston.
Host IP address ni: 174.132.156.66

IP postcode: 77002
IP address latitude: 29.7523
IP address longtude: -95.3670

Tafadahali ni vyema aache upuuzi na uchafu wake mara moja kwani tunaweza kuanika mpaka jina lake kamili, alisoma wapi na hata ikiwezekana picha zake pamoja na kwamba tulisoma computer migombani.
 
Hizo picha ziko wazi kw akila mtu au kwa wanaotaka?Je zinamdhalisha Mkuu wa Nchi?Je zinahusiana na mtu mwenye heshima na hazipatikani kokote?

Usilete voroja kwa utetezi wako wa kipuuzi!shame on you!
jukwa la dini limefungwa kwa kile ati kinachoitwa kashfa dhidi ya dini ya dini na lilikuwa private...picha za jukwaa lile zinadhalilisha utu wetu na ni kinyume na maadili....

...wewe unajua lakini leo umeona ya utamu wakati na wewe umo kwenye udhalilishaji....waambie hao comrades wako

...pcha chafu ni chafu tu.....iwe ya yangu au yako....acha unafiki...

huyo comrade wako mwanakijiji kamchafua sana jk kunan wakatin alisema ana picha za muungwana akiwa hotelini anakula maraha na kimwana.....hio hukuikemea au inafaa? anatofauti gani na hao zeutamu?

angalia watu makini wanavyooandika
 
mkuu sheria zipo ila wafuatiliaji ndio hamna na watu wanasubiri iundwe tume ya kumtafuta zeutamu hakuna anaye jua majukumu yake mpaka kufuatana nyumanyuma. kwa hali hii tuna kazi haswa!
hebu tuambie sheria ipi itamshitaki mwenye web ile na kwa kosa gani? watz bana msiongee ongee tu.....leo hii ndio mnaona iundwe tume kama tume zishaundwa hazina mafanikio....man njoo na plan b
 
Bado sijajua sheria gani itamshtaki ze utamu,maana katika ile picha hakuna sehemu iliyosema "Rais fulani" au "Fulani bin Fulani" ,kilichotokea ni kufananisha sura ..hmm labda wana sheria watusaidie hapa.
 
Huyu jamaa nimepata jina lake kamili, alisoma chuo gani na lini. Na kizuri zaidi nimepata mpaka picha yake. Sasa naomba aache upuuzi na uchafu wake mara moja kabla sijamweka hadharani hapa jf.
 
Ahahahahahahahaaaa....well...kwa bahati mbaya au nzuri mambo kama haya huwezi kuyazuia. Wangapi wamefanyiwa hivyo?

Heheheheheeee sijui mwenyewe akiiona hiyo picha atasemaje?
 

Kuu hizo ni address za webhost na sio za utamu mwenyewe, kupata data za utamu mpaka webhost atoe ushikiano, na hilo kwa sheria za marekani ni suala gumu sana.
 
Huyu jamaa nimepata jina lake kamili, alisoma chuo gani na lini. Na kizuri zaidi nimepata mpaka picha yake. Sasa naomba aache upuuzi na uchafu wake mara moja kabla sijamweka hadharani hapa jf.

Mhhh unatishia mtu mzima nyau? Wewe weka wala uimwombe idhini yake
 
- kwangu leo ni siku ya huzuni sana kwa sisi wapenda uhuru wa kusema, na hasa watumiaji wakubwa wa internent, na tunaojulikana na wengi kwamba ni magiwji wa mtandao, kinachosikitisha zaidi ni the fact kwamba tunawajua hata hao wahusika wa hiyo kitu, shame on you guys na this time mmefika mbali sana!

Mungu Aibariki Tanzania.

FMES
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…