Tufanye nini kuweka utamaduni wa uchapa kazi kwa vijana?

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,609
8,749
Imefika wakati wa kuwauliza vijana ukikutana nao, wewe unafanya nini kama ilivyokuwa zamani.

Vijana wetu tena wadogo ni zaidi ya 70% ya watanzania. Ni lazima tuweke utamaduni tofauti kwa vijana wetu ili waweze kushindana na vijana wenzao kwenye nyakati hizi za ushindani.

Nchi zinaungana na dunia inaendelea kuwa ndogo hivyo pamoja na elimu utamaduni wa ubunifu na uchapa kazi ni muhimu sana.

Tanzania hasa kwa wazee wetu bado kuna utamaduni wa udanganyifu, rushwa, ulalamishi na utegemezi kwa serikali. Tunatakiwa kuongeza utamaduni wa ushindani kwa vijana ambao ni wa kimaendeleo.

Wote tuna jukumu hili. Tunaweza kuwapa vijana elimu, vitendea kazi, pesa lakini bado walisifanye chochote kama ni wavivu au hawana mawazo endelevu.

Mfano Mo alianzisha fungu la kuwapa pesa wajasiriamali na mafunzo. Alikuja kulifunga kwasababu ya udanganyifu, yaani vijana wetu ni bora waibe mtaji kuliko kujiendeleza na kuwa na biashara kubwa. Raisi Mama Samia na Bashe wanataka kuwaingiza vijana kwenye kilimo lakini kilimo hakiitaji uvivu hata trekta linataka uendeshaji.

Mimi naona kuna tatizo kubwa la kiutamaduni ambalo badala ya kulaumu inabidi tuwasaidie hawa vijana.
 
Serikali ianze kutoa kwa pesa za mikopo ya halmashauri na iache urasimu na visingizio visivyo na maana.
 
Back
Top Bottom