Je Tanzania tunaelekea wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je Tanzania tunaelekea wapi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MwanaFalsafa1, Apr 30, 2009.

 1. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #1
  Apr 30, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Jamani nataka maoni yenu wana JF. Tanzania inaelekea wapi?

  1.Hali ya ufisadi ni ya mpito tu na itakuja kuisha
  2.Mafisadi watashitakiwa na haki kutendeka
  3.Mafisadi wana nyamazisha kesi
  4.Mapinduzi

  Jamani haya ni baadhi tu ya mambo ninayo dhani yanaweza kutokea je wenzangu mnafikiriaje?

  Maana sasa Tanzania imekua kama igizo, kila wiki watu mna kaa muone nini kitaendelea.
   
 2. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #2
  May 1, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Ni kweli hali inayoendelea inapangwa na wafuasi wa Sultani CCM ,ukiangalia kwa makini mchezo wanaocheza CCM hivi sasa ni tactics za kupangua defence ya upinzani na kupata goli 2010, upinzani usipokuwa makini utajikuta umewekwa katika kambi moja ya Sultani CCM wakiachwa kushangilia mazoezi ya CCM.

  Hali ya ufisadi haiwezi kuondoka ikiwa tutaendelea kijielemeza katika moja ya kambi za Sultani CCM ni lazima tuziepuke kambi hizi kwa bei yeyote ile ,haitakiwi kukingia ubavu kupe yoyote yule ambae yumo ndani ya CCM ,ikiwa ishara na dalili zinaonyesha kuwa fulani na fulani ni mapapasi wa CCM inafaa watu hao kuwaepuka kama wenye ugonjwa swine flu ,maana watatuambukiza na kuwaambukiza wapiganaji wetu kwenye vita hii.
  Core system ya CCM hivi sasa wanatumia style ya wagawe uwatawale na ni namna gani wanawagawa WaTz na kubaki ndani ya himaya ni kutumia mfarakano waliyonayo ndani ya Chama chao na kuhakikisha kuwa wale wote wanaotatizana hawaondolewi ndani ya Chama bali wanaachwa wapambane humo humo ndani ya Chama mpaka mmoja amuheshimu mwenziwe kwa maana atakaeshindwa atakaa kimya na kubaki kubweka kama mbwa koko aliepigwa jiwe.

  Mafisadi hawatashitakiwa bali watashitakiana kwa kuwa wao ndio wanaoongoza vyombo vya sheria na wana mamluki wao wanaojua namna ya kumaliza matatizo ya aina hiyo ndani ya mfumo wanaoujua wao ,kutowana kafara kama walivyozea ,yule dhaifu anaweza kunyamazishwa au kesi kumalizika kwa kufutwa au kutokea ukimya tu ,tusijue kinachoendela ,hivyo hakuna haki yeyote itayopatikana kwa Mtz kuona kuwa haki imetendeka na faida imepatikana kama funzo kwa wengine ,hicho kitu hakitatokea chini ya utawala wa sultani CCM.-Ni kulindana tu mpaka mwisho wa dunia. Na wananchi kupigiwa mpira wa kona kuwa fedha iliyoibiwa inarejeshwa hiyo pokeeni katika mifuko ya mbolea.

  Kunyamazisha kesi kunakuwepo ndani ya system ya Sultani CCM na jinsi ya uendeshaji wa kesi zitakazobahatika kufanyiwa usanii mahakamani ,hizi kesi huenda zikachukua muda mrefu bila ya kuwepo na hukumu ya aina yeyote ile ,watu wanakwenda na kurudi mahakamani na kupewa vichwa vya kuwalaghai watz katika vyombo vya habari ,ukitilia maanani kuwa vyombo hivyo vinamilikiwa na hao hao wafuasi wa Kampuni za Sultani CCM & Co (mafisadi).

  Mapinduzi kwenye Nchi kama Tz ni tabu sana kutokea kwa maana itabidi nchi kugawika na kuwepo makundi katika sehemu mbalimbali na hivyo kunaweza kusababisha mapigano ya maeneo au mapigano ya wenyeewe kwa wenyewe na ndio utakuwa mwanzo wa mauaji ya paokwa papo.

  Hivyo Mapinduzi makubwa ni kuiangusha Serikali ya Sultani CCM kupitia political ground na hili linawezekana kabisa pale ambapo kitatokea Chama cha upinzani kitakachoweza kujumuisha nguvu za wananchi wa Tanzania nzima ,na hili linawezekana kabisa,iwapo mikakati ya kweli itapangwa kuiteka miji mikuu (Kimikoa na kiwilaya) yote ya Tanzania ,kwa maana unapoamsha hisia za miji mikuu inakuwa rahisi kwa vitongoji kufuata upepo na ndio kazi ya upinzani inapotaka kuelekezwa kuhakikisha miji mikuu yote inapokea na kukubali muamsho wa mabadiliko kwa kasi kubwa ,mahudhurio makubwa ya mikutano ya hadhara ya chama vya upinzani ili kuvuta hisia za mabadiliko kwa wananchi wa vitongoji hali kadhalika unapoandaliwa mkutano kwenye kitongoji cha nje ya mji ,hawa wa mjini ni lazima wavamie kitongoji kwa nguvu za washiriki kutoka mjini hoi vifijo na kuuzunguka kitongoji kwa sherehe na nderemo ili kuwashawishi wananchi wa eneo hilo ,na hili liwe zoezi kwa vitongoji vyote vinavyozunguuka miji mikuu au wilaya zaidi kwa sehemu ile ipo karibu ambayo itakusanya vitongoji vingine bila ya tatizo ,hapa kuna gharama za usafiri na wakati mwengine ikiwa mumefanikiwa kwenye miji mikuu washiriki wataweza kutoa vyombo vya usafiri bure kuhudhuria kongamano hilo linalofanyika nje ya mji.
  Kama mliona harakati za kampeni hapa Marekani kulikuwa na misururu ya magari kuelekea remote areas ,huko nimeona harakati za kuvamia vijji kwa misururu ya magari kupitia Chama cha Wananchi CUF na ni style ambayo CUF walifanikiwa sana katika harakati zao pale Zanzibar na baadhi ya mikoa ya Tanganyika na kuiweka CCM pahali pagumu kiasi ya kukwiba uchaguzi wa 2005.
   
 3. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #3
  May 1, 2009
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,565
  Likes Received: 1,932
  Trophy Points: 280
  Kama kuna kutupiana mipira,mara nyingi namba 4 hufanya kazi.

  Maana sasa nasikia lawama ni DPP,sasa na mimi nauliza DPP nani anamteua?

  JF nzima ni vurugu,wengine wakidai kwanini wanaotoa tuhuma wasiende mahakamani nk, serikali haiwezi kujishtaki na hivyo option ya mwisho ni hiyo namba 4....Namba mbili inategemeana sana na namba nne na moja, kwamba namba nne ikiwa possible,basi namba mbili automatically nayo itakuwa possible.

  Namba moja ni matokeo ya mwisho kama either namba 4 na 2 zitakuwa possible....Isipokuwa hivyo,then itakuwa kinyume cha namba moja ambayo ni namba 3 kwani ina maana mafisadi wakishinda, basi ufisadi hauwezi kwisha, umasikini utaendelea na mwishowe Taifa linaweza ku colapse na hivyo tutakuwa na a "failed state"
   
 4. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #4
  May 1, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hapa tulipo tupo katika hiyo failed state dalili ndio zinaonekana kushamiri.
   
 5. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #5
  May 1, 2009
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Kuisha kwa ufisadi ni mpaka chama cha mafisadi kiondoke madarakani.Kwa mazingira tuliyonayo,hilo si la kutokea leo au kesho.Mapinduzi yanawezekana lakini again hilo nalo sio la leo au kesho kwa sababu Watanzania wamezowea kuonewa....(anaebisha ajiulize kuhusu wale walioandamana kuwapokea Chenge na Lowassa majimboni mwao)
   
 6. Novatus

  Novatus JF-Expert Member

  #6
  Nov 30, 2010
  Joined: Jul 28, 2007
  Messages: 331
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  sio siri hospitali zote za serikali hazina dawa na watumishi wametishiwa wasitoe kauli yoyote juu ya hili vinginevyo hatua kali zitachukuliwa juu yao. Cha kushangaza hospitali za wilaya hapa Mwanza zinatoa rufaa kwa wagonjwa kwenda Bugando kwa matatizo yaliyo ndani ya uwezo wao. Fikiria toka Magu kwenda Mwanza Ambulance inatumia lita 20 za diesel sawa na takribani Tshs 34,000 na huenda kwa siku wanaweza kufanya safari 5. ukizidisha gharama hiyo ni sawa na Tshs 170.000 ambazo zinaweza kununua nyuzi za operation za kuwahudumia wajawazito wanaohitaji kupasuliwa (ceasar) 15. Na wengi wanaopewa hizo referral ni wajawazito. Athari za kumsafirisha mjamzito umbali kama huo wakati anahitaji huduma immediately nadhani kila mmoja anweza kuzijua,

  hivi tumekosa kiongozi wa kuchukua maamuzi sahihi ili kutumia hata hiyo raslimali ndogo kuokoa maisha ya watanzania??? Au tuna viongozi wanaotii amri bila kutumia akili.

  wana Jf jadili hili
   
 7. Quinty

  Quinty JF-Expert Member

  #7
  Dec 14, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 463
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Habari za asubuhi great thinkers...! Leo nimetoka nyumbani saa 12 kamili naelekea town...njiani kukawa kuna jamaa watatu wanaongea. Maongezi Yao ni juu ya mtu flan ofisini kwao wanamsema vibaya. Kufika kwenye Daladala hapo ndo kubaya zaidi maana wamama wanamsema pia mwenzao...nimeshuka naelekea jengo flan refu hapa town nimepanda lifti nako pia Maongezi ni hayo hayo../ sasa Nashindwa kuelewa kwamba tunaelekea wapi badala ya kuongea ufanisi wa kazi tunaanza kuangalia mapungufu na kuwa kigezo cha kupoteza muda...kwanini Hata tusijifunze kusoma walau hata gazeti tutapata jambo la maana kuliko kuongelea watu. Ona sasa mpaka sasa saa mbili na robo na hakuna ofisi zimefunguliwa huku town c benki wala ofisi za serikali...Nashindwa kuelewa kama kwa style hii tunaweza boresha maisha yetu kama Watanzania tunaopenda kazi maana ndo msingi wa maisha... Inabidi tubadilike tuache kujadili watu na tujadili maendeleo.. Tuache tabia ya kufungua ofisi saa tatu kwenda kunywa chai mpaka saa nne kwenda lunch saa sita na nusu kurudi saa nane na kufunga ofisi saa tisa na nusu.
   
 8. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #8
  Dec 14, 2010
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Plentiful of small minds around....
   
 9. Quinty

  Quinty JF-Expert Member

  #9
  Dec 14, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 463
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Yeah so bad
   
 10. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #10
  Dec 14, 2010
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Tuache tabia ya kufungua ofisi saa tatu kwenda kunywa chai mpaka saa nne kwenda lunch saa sita na nusu kurudi saa nane na kufunga ofisi saa tisa na nusu.
   
 11. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #11
  Dec 14, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Ni alama kwamba mahusiano ya kikazi maofisini na ya kijamii mitaani yamekwenda mrama. Kuna kirusi!
   
 12. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #12
  Dec 15, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  :A S embarassed::A S embarassed::A S embarassed::A S embarassed::A S embarassed::A S embarassed:

  Haya bana
   
 13. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #13
  Dec 15, 2010
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  ndio mfumo tuliojijengea huwezi kuukwepa,
   
 14. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #14
  Mar 12, 2011
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Jana nilitaka kununua matairi ya gari langu Landrover na nikatembelea maduka ambayo huwa nanunua vitu vya aina hiyo. Maduka hayo ni ya wenzetu WaTZ wenye asili ya India.

  Nilitamani kulia pale ambapo nilikuta bei ya matairi hayo ya YANA yamepanda kwa karibu asilimia 100! Januari mwaka 2010, nilinunua matairi manne kwa shilingi laki tano na kidogo, moja liligharimu kama shilingi 150,000/-. Jana nilipoenda maduka yaleyale, nimekuta tairi moja linauzwa shiling 230,000/-! Nilisikitika sana na kujiuliza nchi yetu inaenda wapi? Hali imebadilika ghafla mno!

  Kuna uvumi niliuzisikia mwanzoni mwa mwaka ati CCM ilikopa mapesa mengi kwa waanyabiashara wa Kiasia kwa ajili ya kugharimia Kampeni za Uchaguzi,( kila mmoja anajua jinsi CCM ilivyotumia mapesa mengi ili kushinda Uchaguzi wa 2015). Uvumi huo ulidai kuwa matokeo ya bidhaa kupanda bei kiasi kikubwa baada ya uchaguzi ni kutimiza makubaliano baina ya wafanyabiashara hao na CCM kuwa baada ya uchaguzi, ati Wafanyabiashara wapandishe bei za bidhaa ili kufidia mapesa yao waliyoichangia CCM.

  Kwa hali ilivyo, ya mfumuko huu mkubwa wa bei za bidhaa kiasi cha Tanzania kuongoza kwa mfumuko wa bei katika Afrika Mashariki ni wazi; HUENDA KUNA UKWELI!
   
 15. Jilanga

  Jilanga JF-Expert Member

  #15
  Mar 13, 2011
  Joined: Feb 13, 2011
  Messages: 254
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Usishangae sana ndo mbinu zinazowapa ushindi Sisem! Kama uko makini kila Baada uchaguzi mkuu Serikani huwa ina adopt contractionary monetary policy ili kupunguza mapesa mengi waliyomwaga kipindi cha kampeni!

  Mf. Jan 2006 kubadili plate no za Gari, pikpk pamoja na viza {passport za kusafiria} ilikuwa ni mpango kabambe wa kuchukua hela mikononi mwa raia nahs hii sekeseke lilikupitia!

  Inasemekana Rostum Aziz {MP} Igunga alifinance CCM Uchaguzi Mkuu 2005 kwa mashart ya kupewa tenda kubwa kubwa za ki-serikali na matunda yake kushindia Richimond ambayo Ccm walijitoa ufahamu baada ya Wapinza kugundua ni compun hewa! Ambayo ndo inasumbua mpaka leo kwa Jina la Dowans! Hii si sawa na kuuza nchi? MUNGU IBARIKI TANZANIA!
   
 16. MUREFU

  MUREFU JF-Expert Member

  #16
  Jun 22, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 1,230
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Habari zenu wanaJF kusema ukwel binafsi ninachoshwa na habari za kilasiku kwenye radio mana nikisikiliza taarifa ya habari au nikisoma magazet lazima nitakutana na habar kama sio mtoto kamuu baba yake bas baba ameuwa au kambaka mwanae. Hv mbona kila kukicha haya yanatoke? Je ndio maendeleo au nini? Na kama ndo maendeleo inakuwaje mahovu yanakuwa meng hv mana utasikia ajali mara utasikia maandamano yan kila kukicha lazima jipya liwepo. Et wana jamii hii ni dalili ya kuchokana au ni nini? Nawakilisha
   
 17. Tajy

  Tajy JF-Expert Member

  #17
  Jun 22, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 298
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mwisho wa dunia umekarbia
   
 18. T

  The Infamous JF-Expert Member

  #18
  Jun 22, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 719
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  soma vitabu vya dini haya yote yameelezwa mwisho wa dunia ukikaribia,,,jipange bro mrudie muumba wako jitahidi mwili wako uwe hekaru la bwana
   
 19. N

  Nyumisi JF-Expert Member

  #19
  Aug 15, 2011
  Joined: Nov 10, 2010
  Messages: 451
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 60
  Jamani wanaJF, lazima tukiri kwamba tuna tatizo kubwa la msingi kama nchi kwa sasa. Yaani baada ya miaka 50 ya uhuru bado tunakuja na mipango ya dharura ya kuzalisha umeme yenye gharama kubwa namna hiyo? Waziri anajitapa kwamba watazalisha umeme wa kutosha hadi ziada ya zaidi ya 200 MW. Hii ziada ya nini ukizingatia umeme wenyewe ni wa gharama kubwa sana. Yanarudi yaleyale ya richmond, lazima 150 million ilipwe kwa siku wawe wamezalisha umeme au la (wanaita capacity charge). Chanzo cha pesa ni kukopa kwenye mabenki ya ndani na kuongeza bill kwa walalahoi. Sasa cha kujiuliza, hivi miaka yote hakukuwa strategic plans za kutambua kuongezeka kwa mahitaji ya umeme na hivyo kuwekeza mapema kwenye vyanzo vya umeme wa gharama nafuu? Nasikia tuna vyanzo vingi kama makaa, upepo, nishati ya jua, gesi n.k. Pili, hivi hiki chanzo cha maji wanachosingizia kila siku kuna mkakati wowote walioufanya kupanua yale mabwawa ya mwalimu au kuongeza mengine na kuyatumia hayo maji kwa ufanisi zaidi, mfano kufanya recycling?. Tatu, hivi miaka yote hiyo tuliyochimba madini, hatujapata hata pesa za kuwekeza hata kununua mitambo ya kuzalisha umeme hadi tukope kwenye mabenki na kutembeza bakuli? Tuma mifano ya nchi kama South Africa ambao wameendelea sana hata kuzidi baadhi ya nchi za ulaya kwa kutumia dhahabu kama tuliyonayo sisi. Mbona sisi hali ya uchumi inazidi kuwa mbaya pamoja na kuchimba madini kwa miaka yote hiyo? au ndo tuamini kwamba hayo madini yanawanufaisha wazungu na vibaraka wao mafisadi? Nachelea kusema tuna matatizo makubwa katika safu za juu za uongozi wa taifa hili, na hali kama itaendelea hivi kuna wakati watanzania watahitaji kuikomboa nchi yao upya kwa njia zozote zile. Iam sorry.
   
 20. shegaboy

  shegaboy JF-Expert Member

  #20
  Aug 15, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 214
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani watanzania inasikitisha sana inauzunisha sana. ni takribadi wiki tu tangu bei ya mafuta ishushwe tena na serikali kupitia Ewura leo tena bei inapanda sasa napata jibu ni kwanini bei ilishushwa watanzania. ilikuwa kuwezesha bajeti ya nishati na madini ipite then wataturudisha hapa walipo turudisha. sasa naanza kutambua kuwa serikali yetu aina nia njema na wananchi wake kwani unaweza kuona ni kwajinsi gani wana tuyumbisha wananchi ila angalizo langu kwa serikali yetu.
  Wananchi na dhani wako likizo siku watakapo rudi hakika nchi hii itawaka moto kama kweli wanamtambua ili wakae mkao wa kuukumiwa kwani hakuna si serikali hii inayoweza kuleta mabadiliko na maendeleo tena kwa mtanzania.
  nawasilisha jamani
   
Loading...