Wanabodi..
Natumai mnaendelea vizuri na kushiriki kikamilifu kwenye zoezi la upigaji kura sambamba na kuwachagua viongozi wetu wapya kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
Nimeamua niandike uzi huu na kwa kuazima mashairi yanayopatikana kwenye wimbo wa kwaya ya AICT MAKONGORO VIJANA CHOIR.
Vijana hawa waliimba huu wimbo ambao ukiusikiliza na kuutafakari vizuri unasadifu kinachoendelea muda huu kwenye zoezi zima la uchaguzi.
Kama mjuavyo,ndani ya zoezi la uchaguzi ndipo mataifa ya nnje yasiyo na nia njema na Tanzania yanapotumia chance (nafasi) kama hii kuvuruga Amani,Umoja na Mshikamano wa Kitaifa.
Naungana na Mamlaka zilizochukua jukumu la kuzima Huduma ya Internet toka juzi na kudhibiti mitandao ya kijamii kama tweeter,Whatsapp,Telegram,Facebook n.k
Inafahamika toka uchaguzi uliopita wa mwaka 2015, mitandao ya kijamii imetumika sana katika kutaka kuvuruga Umoja,Mshikamano na Amani ya nchi.
Tumeona ma-champion wa mtandaoni kina Kigogo na wengineo ambao wametumia mitandao hii kuchochea vurugu kwa kigezo cha kuwahabarisha wananchi.
Kwa namna moja hawa watu walifikia hatua hata ya kuandaa maandamano kwa kutumia mitandao ya kijamii huku wao wakiwa mbali na Tanzania.
Kwa kuangalia mapema kwenye uchaguzi huu unaona kabisa kulikua na uchochezi wa makusudi wa kuvuruga amani na kuchochea vurugu hasa kwenye kipindi hiki cha uchaguzi.
Tumeona ndugu Amsterdam anavyokesha kuandika maandiko na waraka kuhusu uchaguzi wakati haumuhusu,tumeona vibaraka wengi hata wa hapa Tanzania wakitumia mitandao hii hii kuchochea vurugu na chuki kati ya wananchi na serikali yao.
Tanzania kuwa na amani miaka yote mpaka kuitwa "Kisiwa cha Amani" hili haliwafuhishi mabeberu na watu wasioitakia mapenzi mema hii nchi .
Mpaka Serikali kupitia mamlaka zake imeamua kufikia maamuzi ya kuzima huduma hii ya internet ni dhahiri inapenda welfare' (ustawi) wa raia wake hasa kipindi hiki.
Kumbuka siku moja inatosha kabisa kuipoteza Amani..lakini miaka ,miezi itapotea ili KUITAFUTA Amani.
Vikao na vikao vitakaa kuitafuta hii Amani.
Kweli Tupoteze Amani yetu kwa ajili ya uchaguzi wa siku moja??
Tuipoteze Amani yetu na tumwage damu kwa ajili ya Mitandao ya kijamii na Propaganda za chuki toka kwa wasioipendea mema Tanzania??
Kwa hili naungana na serikali katika kusitisha huduma hii ya Internet na ni Uamuzi mzuri katika suala zima la kuitunza Amani..
Jamani,vuruga kwengine lakini usivuruge Amani.
Chezea kwengine lakini Usichezee Amani.
Na watanzania hatuko tayari na hatutakua tayari kuona Amani yetu ikitikiswa na watu wasiotakia mema kama akina Amsterdam.
Najua wengine watasema wamepata hasara kwenye biashara zao au kwenye mambo yao mengine sababu tu huduma hii imesitishwa lakini wakumbuke kama Amani ikiondoka hawataweza fanya hizo biashara zao .
Amani ndo kila kitu na hongera sana Serikali na mamlaka zake kwa kuweka mbele utaifa na kuilinda Amani yetu kwenye kipindi hiki ambacho Mataifa mengi watataka kuivuruga Tanzania.
Lakini hawataweza ivuruga Tanzania maana asilimia 90 ya namna ya kuivuruga Tanzania ni kupitia mitandao ya kijamii ambayo imedhibitiwa hivyo imekula kwao.
Amani yetu tuilinde,Maana kuipoteza Amani ni Rahisi sana na ni Vigumu kuirudisha Amani...
Chezea Pengine lakini usichezee Amani,Vuruga kwengine lakini usivuruge Amani.
Uchaguzi mwema na MUNGU ibariki Tanzania.
Kwa maoni au ushauri :
godjohn8@gmail.com