Je, Tanzania bado ni nchi ya Amani?

Advisor

Member
Jan 10, 2008
38
2
Je, nchi yetu bado ni nchi ya amani? Sio watu wameamua kuwa watulivu na ideology ya CCM kuwa Tanzania ni kisiwa cha amani ndo inatawala?

Nini hatma ya Tanzania endapo wananchi watachoka manyanyaso?

================

Tanzania no longer heaven of peace?

IBRAHIM JOHN
Dar es Salaam
ThisDay

WHEN I read our dailies with headings like RC shoots a daladala driver to death; Tanzanian ambassador steals 2bn/-; BoT made false payment of 133bn/-; Tanzania pays 152m/- daily for a fake Richmond power deal; Zanzibar in everlasting political crisis; Overpriced radar from Britain; Controversial Presidential jet; Demolition of houses; Fake TICTS deal; Buzwagi, Kiwira, Tangold, Meremeta, Reception parties for corrupt leaders, and the list goes on and on - I get convinced that there is a very thin line between insanity and whatever we call peace here in the once heaven of peace.

If peace exists in our nation, then this makes me wonder if peace is really a good philosophy of life! I think we are missing something, somewhere. We do need to seriously re-examine ourselves. Someone once said: You should examine yourself daily. If you find faults, you should correct them. When you find none, you should try even harder. Our problem is that we quit examining ourselves many years ago. So we see no fault. We dont even know the last time we experienced peace as a people. Its time we examined ourselves as a nation.

Otherwise I would suggest we get into the Guinness world Book of Records for becoming the first nation in the whole wide world to have co-existence of injustice and peace.

I, however, think that its just confusion of words. What we call peace is the absence of war, which is not necessarily peace, for peace is not a relationship of nations. It is a condition of mind. By the way Im not sure if the Wanchari have stopped fighting the Wakira in Tarime!

But since we need peace I think we need to work for it. Dr Martin Luther King, Jr. was quoted as saying, Those who love peace must learn to organize as well as those who love war. We as Tanzanians need to be honest to ourselves. We need to organize ourselves as peace-loving people as well as war-lovers.

Pope Paul VI said If you want peace, you must work for justice. Justice is our biggest challenge. We need to work for it. But because of lack of functional law enforcement system we need to work even harder for justice and organize ourselves better.

Otherwise Im really afraid of the future of this nation. And until we get a capable partial law enforcement system, I suggest we be creative. I suggest we adopt George Carlins idea of using signs. He said there are a lot of signs for minor offences and infractions. And they seem to work pretty well.

When people read signs like "Thank you for not smoking"; "Please wait in line" etc they do just that.

Why then dont we have signs that say Murder Strictly Prohibited; or No Raping People and something like Thank you for not conducting business in the State House. Signs are good. Im sure we can use those for a while until we have a good law enforcement system.

mailto: ijwerrema@ijwerrema.info
 
Tanzania ni nchi ya amani.Challenge tulizo nazo hazitofautiani na zilizopo nchi nyingine. Tuendelee kujitahidi kuboresha hali yetu ya uchumi na kulinda amani iliyopo kwa kusimamia utawala wa sheria na maadili sahihi kwa manufaa ya taifa.
 
Mimi siioni hiyo amani kwa sababu zifuatazo.
  1. atu vijijini wanalala polini ili kukwepa kukamatwa kwa kuwa hajatoa mchango wa sh.5000 ambazo ndo kipato chake kwa mwaka inawezekana ni sh. 120,000 ambazo anategemea zifanye kila kitu halafu unamwambia achange 5000 kwa ujenzi wa shule wakati wazee wa vijisenti wanaendelea kuchota BOT
  2. Watu wanakula mlo mmoja kwa siku hawanba uhakika wa kuamka kesho asubuhi wakati kuna watu wanavijisenti ambavyo havina kazi mpaka viaifadhiwa nje ya nchi.
  3. Machinga wanakamatwa na kunyanganywa bisdhaa zao pale kariakoo hawapelekwi mahakamani wala nini, ukishindwa kutoa chochote hata 2000 unanyanganywa vitu vyako na utavipata tena
  4. Mtu anakufa kabla ya kupata matibabu hata kama amefikishwa Hopitali kwa kuwa hana sh. 1500

Sioni ni amani ya aina gani tunaongelkea hapa ila tu nibomu linalosubiri muda wake kulipuka especially likiongezewa na njaa inayokuja.
 
Hiyo Amani Ni Ipi?? Wanatuibia Kweli Kweli. Leo Katika Kanchi Ketu Watu Wamerudi Katika Kutumia Miti Shamba Maana Hiyo Elfu Tano Ya Matibabu Katika Hospital Zisizokuwa Na Dawa hazipatikani kirahisi maana umaskini umejaa vijijini kwa mazao kuwa na soko dogo. Hapo Kuna Amani? Amani Itoke Wapi?
 
IDEOLOGY tulizopandikizwa na CCM ndio zinasema kuwa BONGO kuna amani eti kwasababu hakuna mapanga wala vita vinavyoendelea kati yetu watanzania.

Ukweli wa mambo, HAKUNA AMANI yeyote kutokana na sababu zilizotajwa hapo juu. Kama wagonjwa mahospitalini wanakosa hata vitanda vya kulalia au kulala wawili wawili, hakuna dawa, kupata mlo shida, wanafunzi wanafukuzwa vyuo kwa sababu ya sh. 10,000 wakati huohuo kuna viongozi wa nchi wana mabilioni nje ya nchi, hiyo haina maana yeyote na haileti amani yeyote kwa wananchi waliowapa dhamana ya kuwa madarakani.

IT IS A TIME BOMB!!!! PEOPLE WILL TAKE TO THE STREETS ONE DAY AND THERE WILL BE NO MORE LUXURY SUV GOING BEFORE THEIR EYES.
 
Amani hipi yiho unayozungumzia iliyopo Tanzania??

HAkuna Amani yoyote Tanzania, tusidanganyane hapa, amani ya kulazimisha. Tena ndo mamambo sasa hivi yako hovyo kinoma

mkuu unakubali kama amani ipo, ikiwa ya hiari au ya kulazimisha.

nyie wapinzani si mlisema mtanunua amani kwa bei yeyote au mlisahau kuwa pia bei ya kulazimisha ipo?


Tanzania amani tunajivunia kwa sana ukiacha vijimambo vidogo vidogo
 
mkuu unakubali kama amani ipo, ikiwa ya hiari au ya kulazimisha.

nyie wapinzani si mlisema mtanunua amani kwa bei yeyote au mlisahau kuwa pia bei ya kulazimisha ipo?


Tanzania amani tunajivunia kwa sana ukiacha vijimambo vidogo vidogo

Mtu wa Pwani hiyo amani ipi unayosema ikiwa maalbino wanachinjwa kila siku? unadhani hawa wanajua habari za amani yako hiyo? hizi ni siasa tu. Waulize wale vikongwe wa Shinyanga na Mwanza kule kama wana amani. Tuulize tuliokutana na majambazi kila siku njiani. Inabidi tusafiri na askari ambao hata wao maisha yao na familia zao zinazowategemea hawana amani. Njoo kwangu uangalie jinsi nilivyojaza vyuma milangoni na madirishani huku nikiwa nimeweka hata waya za umeme kwenye ukuta mreeeeeefu niliojenga kwangu. Sina amani. Ninaye baba ambaye anaumwa ugonjwa wa kisukari na nahitaji kulipa sh. 5000 kila aki attend hospital na kununua dawa zake maana mara nyingi hosp hawana dawa za kutosha. hapo usihesabu mke, watoto, na wanajamii tegemezi nilionao. Je hapo kuna amani? we unadhani amani lazima nchi nzima i riot? hapo ndio tuseme hakuna amani? kwa ku conclude ni kwamba hii amani inayohubiriwa is just a political slogan used to fool us. Si lolote wala haipo katu.
 
Mtazamo! Mtazamo! Kwa wale ambao wanaitafsiri amani kuwa ni kutochinjana barabarani basi ndio hao wanaowasikiliza CCM na bango lao na kutaja sababu zote zilizoelezwa humu na katika hiyo makala kuwa ni majambo madogo madogo(Mtu wa Pwani), lakini jambo dogo tu linaweza kutoa hitimisho kuwa Tz hakuna amani ukijiuliza ni Wtz wangapi wana hakika ya mlo wao wa wiki moja na ukipata jibu utajua kama kweli kuna amani au hakuna.

Kama tunasubiri mambo makubwa ndio tuseme hakuna amani na tuendelee na haya tunavyofanya na si kitambo kila mmoja atakiri bila mjadala kuwa Tz hakuna amani.

Tukubali tatizo na tuanze kujirekabisha - kama umlevi na ukisema unataka kuwacha n lazima ukubali kuwa wewe ni mlevi na una tatizo bila ya hivyo hutoacha milele.
 
AMANI na mshikamano uliopo Tanzania hivi sasa vipo kaika hatari ya
kuuzwa na kisha Watanzania kununua migogoro, kutokusikilizana na hata
vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Dalili zote za uwezekano wa hilo zipo na hasa ukizingatia yale
yaliyotokea Amerika ya Kusini na kati au Latin Amerika miaka sio
mingi iliyopita.

Nchi hizo zilizokuwa zinafanya vizuri hadi wakati huo zilikosea pale
ziliporuhusu wanasiasa, watumishi wa umma na wafanyabiashara
[asilimia ndogo ya watu] kuzitumia nafasi zao kujitarisha hadi
kukufuru wakati asilimia kubwa ya wananchi wakielea katika umasikini
wa kutisha na kukatisha tamaa.

Katika kulitafiti hili nimegundua yapo mambo kadhaa ambayo
yasipoangaliwa yataihakikisha Tanzania kugura toka kwenye amani na
kuingia kama nchi nyingi za Kiafrika zilizokosa uongozi makini kwenye
medani ya ghasia, uvunjaji sheria wa waziwazi, mauaji na hatimaye
vita vya wenyewe kwa wenyewe. Mambo hayo ni pamoja na:

  1. . Kubinafsisha mali za umma na kisha mangimeza na viongozi wa chama
  2. tawala kula chote kilichopatikana.
  3. . Wajanja wachache kujitajirisha kinamna kutokana na mali ya umma,
  4. vyeo walivyo navyo na fursa walizonazo.
  5. . Tofauti kuongezeka mno kati ya kipato cha chini na kipato cha juu.
  6. Wanaofanya kazi sana na kuvuja jasho kusota wakati wasiofanya la
  7. maana kutajirika kirahisi mno.
  8. . Wenye uwezo kutumia lugha za kigeni badala ya lugha asili ili
  9. wazilinde fursa zao za kiuchumi, kijamii na kisiasa. Ikiwemo na
  10. mangimeza na wanasiasa kuipiga vita lugha ya Kiswahili na kukumbatia
  11. Kiingereza bila ufanisi wowote wa maana kwa kizazi chao wala kwa
  12. faida ya baadaye ya nchi.
  13. . Chama tawala kupora fedha hazina na mifuko ya hifadhi za jamii, pensheni afya, hazina na kadhalika.
  14. . Kukaribisha Wamarekani bila ya kutafakari hofu za msingi za waliotutangulia ikiwemo hayati baba wa Taifa.
  15. . Kuuza kwa bei sawa na bure madini ya nchi na kushindwa kutambua kuwa thamanai ya Watanzania na madini yao ni kubwa zaidi kuliko mitambo ya aina yoyote duniani-iliyopo na itakayogunduliwa.
  16. . Mangimeza na wanasiasa kukubali mgawa wa teni pasenti na kuuza mabilioni kama sio trilioni au zilioni za ukwasi asili wa taifa lao. Na hivyo, wachache kujitajirisha na kuwahukumu wengine kwenye umasikini wa milele.
  17. . Watoto wa wa matajiri na viongozi kwenda shule kwenye magari ya fahari na watoto wa makabwela kunyanyaswa na daladala.
  18. . Kuachia chakula kidogo kuuzwa nje na kukosa hifadhi ya chakula, mafuta, maji ya uhakika.
  19. . Kuwa na tume za uchaguzi zisizo huru na zenye vibarakala wa chama tawala.
  20. . Chama tawala kutumia rasilimali za taifa kuleta mgawanyiko miongoni na ndani ya vyama vya upinzani kwa faida za chama tawala na sio kwa manufaa ya Watanzania.
  21. . Mawaziri, makatibu wakuu na mangimeza wizarani kupora nafasi za masomo ya nje na kuwapa watoto wao hata kama hawana sifa wala uwezo.
  22. . Wastaafu kunyimwa haki zao na kupigwa danadana za kisiasa bila huruma wala aibu.
  23. . Kuwalipa madakrari sawa na maboi nchi za nje na kisha wakubwa kwenda kutibiwa Afrika Kusini, India na Ulaya na kuachia wananchi msabalaba wa rushwa na unyanyaswaji na uchangiaji ambao usingelikuwa wa lazima kama wachimba dhahabu wangetozwa asilimia 13 ya mrahaba
  24. badala ya asilimia 3.
  25. . Polisi wa usalama barabani kuwa ni donda kwa wananchi na wachangiaji wakubwa wa maafa barabanni. Baadhi ya askari hao wamejenga dola zao kwenye njia wakubwa wasikopita sio kwa ajili ya kulinda usalama wa watumiaji barabara bali kwa ajili ya kujilipa mishahara ya ziada kupitia rushwa.
  26. . Polisi na mahakama kushtaki na kuadhibu wanaostahili kushtaki na kuwaachia na kutowaadhibu wanaostahili kushtakiwa.
  27. . Polisi kujali usalama wa magari, nyumba na mali nyinginezo kuliko maisha ya watoto, wazee, walemavu, watembea kwa miguu na wanyonge wengine kwenye jamii.
  28. . Mamlaka husika kujali kuwakamua wananchi bila kuangalia upande wa pili kwa maana ya kuhakikisha vyombo na huduma vina kiwango kinachokubalika kimataifa.
  29. . Viongozi kujali zaidi mambo ya nchi za nje [kushughulikia migogoro ya wengine kama vile Kenya, Darfur, Zimbwabwe lakini kupuuza matatizo ya ndani [albino, pemba].
  30. . Viongozi wetu kuwa wanafiki kama viongozi wa nchi nyingine za Kiafrika na kula sahani moja na wauaji, madikteta na viongozi kachala.
  31. . Kupanda kiholela kwa bei ya vyakula, mafuta na gharama za maisha na kutokuwepo kwa mifumo yoyote ya maana kuhakikisha mabadiliko katika. Kushindwa kuendeleza vipaji vya vijana katika michezo, muziki na sanaa ili waondokane na umasikini.
  32. . Kuruhusu sheria za barabarani kuvunjwa na wale wanaostahili kuzilinda tokana na kamata kamata zisizo na mwisho na zinazoathiri maisha ya Mtanzania kila kukichwa. soko la dunia hayawatesi sana Watanzania.
  33. . Serikali kuwa goigoi katika kushughulikia shida, dhiki na matatizo ya wananchi ikiwa ni maji, barabara, usalama na kadhalika.
  34. . Tabia ya kuchukua muda mrefu mno kushughulikia matatizo ya watu pengine hadi watu wafe ndio matatizo yapatiwe ufumbuzi.
  35. . Viongozi wa zamani wa taifa hili kujiingiza katika mambo yasiyochangia umoja wala mshikamano wa kitaifa.

Huu ni mchango wangu mdogo katika jukwaa hili la wazi na muhimu na
matarajio yangu ni kuwa kila aliye na lake atalibainisha na sote
tuyajadili bila woga wala wasiwasi ili kuweza kunusuru hatima ya nchi
yetu na kizazi chetu.
 
Last edited by a moderator:
TAZAMA MFANO HUU hapa chini:


HIVI kweli hii minara ya simu na njia nyinginezo za mawasiliano ilipokuwa ikijengwa huko Manzese, Kigogo, Kariakoo na sehemu nyingine za walalahoi Baraza la Mazingira nchini halikuona umuhimu wa kutafiti na kuzuia ujenzi wake ili kulinda afya za walalahoi.

Ila kwa kuwa sasa mnara umeanza kujengwa MSASANI ndio NEMC wanazinduka na kutuambia yote ya kutisha kuhusu minara hiyo.


Je, amri ya KUIONDOA minara hiyo sehemu za walalahoi inafuatia nyuma au watazibwa mdomo. Ila ninajua baada ya miaka sio mingi tutaanza kuzaa watoto wasio na pua wala masikio huku Manzese,
 
AMANI na mshikamano uliopo Tanzania hivi sasa vipo kaika hatari ya
kuuzwa na kisha Watanzania kununua migogoro, kutokusikilizana na hata
vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Dalili zote za uwezekano wa hilo zipo na hasa ukizingatia yale
yaliyotokea Amerika ya Kusini na kati au Latin Amerika miaka sio
mingi iliyopita.

Nchi hizo zilizokuwa zinafanya vizuri hadi wakati huo zilikosea pale
ziliporuhusu wanasiasa, watumishi wa umma na wafanyabiashara
[asilimia ndogo ya watu] kuzitumia nafasi zao kujitarisha hadi
kukufuru wakati asilimia kubwa ya wananchi wakielea katika umasikini
wa kutisha na kukatisha tamaa.

Katika kulitafiti hili nimegundua yapo mambo kadhaa ambayo
yasipoangaliwa yataihakikisha Tanzania kugura toka kwenye amani na
kuingia kama nchi nyingi za Kiafrika zilizokosa uongozi makini kwenye
medani ya ghasia, uvunjaji sheria wa waziwazi, mauaji na hatimaye
vita vya wenyewe kwa wenyewe
. Mambo hayo ni pamoja na:
. Kubinafsisha mali za umma na kisha mangimeza na viongozi wa chama
tawala kula chote kilichopatikana.
. Wajanja wachache kujitajirisha kinamna kutokana na mali ya umma,
vyeo walivyo navyo na fursa walizonazo.
. Tofauti kuongezeka mno kati ya kipato cha chini na kipato cha juu.
Wanaofanya kazi sana na kuvuja jasho kusota wakati wasiofanya la
maana kutajirika kirahisi mno.
. Wenye uwezo kutumia lugha za kigeni badala ya lugha asili ili
wazilinde fursa zao za kiuchumi, kijamii na kisiasa. Ikiwemo na
mangimeza na wanasiasa kuipiga vita lugha ya Kiswahili na kukumbatia
Kiingereza bila ufanisi wowote wa maana kwa kizazi chao wala kwa
faida ya baadaye ya nchi.
. Chama tawala kupora fedha hazina na mifuko ya hifadhi za jamii,
pensheni afya, hazina na kadhalika
. Kukaribisha Wamarekani bila ya kutafakari hofu za msingi za
waliotutangulia ikiwemo hayati baba wa Taifa.
. Kuuza kwa bei sawa na bure madini ya nchi na kushindwa kutambua
kuwa thamanai ya Watanzania na madini yao ni kubwa zaidi kuliko
mitambo ya aina yoyote duniani-iliyopo na itakayogunduliwa.
. Mangimeza na wanasiasa kukubali mgawa wa teni pasenti na kuuza
mabilioni kama sio trilioni au zilioni za ukwasi asili wa taifa lao.
Na hivyo, wachache kujitajirisha na kuwahukumu wengine kwenye
umasikini wa milele.
. Watoto wa wa matajiri na viongozi kwenda shule kwenye magari ya
fahari na watoto wa makabwela kunyanyaswa na daladala.
. Kuachia chakula kidogo kuuzwa nje na kukosa hifadhi ya chakula,
mafuta, maji ya uhakika.
. Kuwa na tume za uchaguzi zisizo huru na zenye vibarakala wa chama tawala.
. Chama tawala kutumia rasilimali za taifa kuleta mgawanyiko miongoni
na ndani ya vyama vya upinzani kwa faida za chama tawala na sio kwa
manufaa ya Watanzania.
. Mawaziri, makatibu wakuu na mangimeza wizarani kupora nafasi za
masomo ya nje na kuwapa watoto wao hata kama hawana sifa wala uwezo.
. Wastaafu kunyimwa haki zao na kupigwa danadana za kisiasa bila
huruma wala aibu.
. Kuwalipa madakrari sawa na maboi nchi za nje na kisha wakubwa
kwenda kutibiwa Afrika Kusini, India na Ulaya na kuachia wananchi
msabalaba wa rushwa na unyanyaswaji na uchangiaji ambao usingelikuwa
wa lazima kama wachimba dhahabu wangetozwa asilimia 13 ya mrahaba
badala ya asilimia 3.
. Polisi wa usalama barabani kuwa ni donda kwa wananchi na
wachangiaji wakubwa wa maafa barabanni. Baadhi ya askari hao
wamejenga dola zao kwenye njia wakubwa wasikopita sio kwa ajili ya
kulinda usalama wa watumiaji barabara bali kwa ajili ya kujilipa
mishahara ya ziada kupitia rushwa.
. Polisi na mahakama kushtaki na kuadhibu wanaostahili kushtaki na
kuwaachia na kutowaadhibu wanaostahili kushtakiwa.
. Polisi kujali usalama wa magari, nyumba na mali nyinginezo kuliko
maisha ya watoto, wazee, walemavu, watembea kwa miguu na wanyonge
wengine kwenye jamii.
.. Mamlaka husika kujali kuwakamua wananchi bila kuangalia upande wa
pili kwa maana ya kuhakikisha vyombo na huduma vina kiwango
kinachokubalika kimataifa.
. Viongozi kujali zaidi mambo ya nchi za nje [kushughulikia migogoro
ya wengine kama vile
Kenya, Darfur, Zimbwabwe lakini kupuuza matatizo ya ndani [albino, pemba].
. Viongozi wetu kuwa wanafiki kama viongozi wa nchi nyingine za
Kiafrika na kula sahani moja na wauaji, madikteta na viongozi kachala.
. Kupanda kiholela kwa bei ya vyakula, mafuta na gharama za maisha na
kutokuwepo kwa mifumo yoyote ya maana kuhakikisha mabadiliko katika
. Kushindwa kuendeleza vipaji vya vijana katika michezo, muziki na sanaa ili waondokane na umasikini.

. Kuruhusu sheria za barabarani kuvunjwa na wale wanaostahili kuzilinda tokana na kamata kamata zisizo na mwisho na zinazoathiri maisha ya Mtanzania kila kukichwa.
soko la dunia hayawatesi sana Watanzania.
. Serikali kuwa goigoi katika kushughulikia shida, dhiki na matatizo
ya wananchi ikiwa ni maji, barabara, usalama na kadhalika.
. Tabia ya kuchukua muda mrefu mno kushughulikia matatizo ya watu
pengine hadi watu wafe ndio matatizo yapatiwe ufumbuzi.
. Viongozi wa zamani wa taifa hili kujiingiza katika mambo
yasiyochangia umoja wala mshikamano wa kitaifa.

Huu ni mchango wangu mdogo katika jukwaa hili la wazi na muhimu na
matarajio yangu ni kuwa kila aliye na lake atalibainisha na sote
tuyajadili bila woga wala wasiwasi ili kuweza kunusuru hatima ya nchi
yetu na kizazi chetu.

Asante Shariff,

Inatia moyo kuona kwamba wapo watu wanaojali na kuelewa kwamba hayo yote uliyoorodhesha yanahatarisha Amani ambayo waasisi wa Taifa hili walifanya kazi kubwa kujaribu kutujengea Watanzania.

Hii ni changamoto nzuri sana kwa vijana na wazee wanaojadili juu ya hatma ya Tanzania yetu.
 
JK siyo malaika kila kitu kitajengwa taratibu na siyo kwa kudhani kuwa ni commitment ya mtu mmoja

Tunajua siyo malaika ndo maana tupo hapa kumkosoa anapo kwenda mrama! Tatizo alilo nalo ni nyie wapambe nuksi manao mwambia ambo shwari wkati anazidi boronga!

Yaani mmeshindwa kumwambia aache sheria ichukue mkondo wake kwa wahujumu uchumi ambao vidhibitisho vyake vi wazi kabisa badala yake mnamwambia awabembeleze?


Hakika JK si malaika bali ni MVURUGA NCHI YA TZ
 
Sijawahi kusoma mada nzito kama hii kwa muda mrefu.

Ninaamini kwamba alichokiandika bwana/bibi huyu hakika kinastahili kuwa ni dokumenti ya kufanziwa kazi na viongozi wote Tanzania-ikiwemo upinzani na CCM yenyewe.

Mashindano ya Olimpiki yametufungua macho sana. Moja wapo ni katika mashindano ya canoeing tulipoona wanaoshinda ni wale wanaopiga makasia kwa wakati mmoja, pamoja na kwa mtindo mmoja; wakati kwenye riadha baba kama Marekani limeshindwa kwa kushindwa kupokezana vijiti ipasavyo; na kwenye ngumi jinsi mtu anavyoangusha makonde ndivyo anavyopata pointi zaidi na sio katika kukwepa au kurudi nyuma au kucheza cheza ulingoni.

Hasa hili la mtumbwi mmoja wa Tanzania na sisi wote CCM na upinzani tunastahili kupiga kasia kwa pamoja na sio kama ilivyo sasa ambavyo ndani ya baadhi ya vyama kuna wanaotegea au hata kupiga makasia kiupande upande kwa sababu moja au nyingine.

Hata hivyo, subira ina kikomo chake. Ni lazima serikali na viongozi wetu watambue kwamba 'MUDA' nao ni rasilimali. Na rasilimali hii tofauti na nyengine ikiisha bwana imekwisha huna jinsi ya kuipata. Sasa isionekane sisi ni watu wa kuvumilia tu kuondokana na umasikini eti kwa kuwa rais na bunge lake wanashindwa kuzibadili sheria ili tuondokane na umasikini kwa haraka zaidi. Twende tukajifunze China, Guatemala, Venezuela na kwingineko kwamba hili linawezekana ili mradi nia iwe njema. Maana hakuna mabepari na walaji wa ndani wanaotaka sheria zibadilishwe ili kunufaisha wanyonge ingawa haya yote ni kwa faida yao na ya kizazi kijacho.

Mimi kwa kweli ningeomba wana-jamii tuchangamkie mada hii na kuinyambuanyambua ndani nje ili tuweze hatimaye kutoka na kitabu cha msimamo kuhusu JINSI YA KUUZA AMANI NA KUNUNUA BALAA NA MABAA!

Mratibu, je, hili haliwezekani? Ninaamini kuna mada ambazo zikirejelewa uzuri JAMBOFORUMS itakuwa na uwezo wa kuchapisha kitabu kama sio vitabu kila baada ya miezi mitatu. Angalieni wenzenu wa www.poetry.com kuona kwamba hili linawezekana.

HAKUNA kweli malaika miongoni mwetu. Lakini mimi ninadhani ORODHA ya Sharrif kama ina jambo linalomleng amoja kwa moja Rais ni machache sana. Mengi yanalenga wizara na makundi mbalimbali katika jamii.

PENGINE tuangalie ni jinsi gani ambavyo SERA ZA MADARAKA KWA WIZARA NA MIKOA inaweza kurejelewa upya na kuanzwa kwa mfumo wa PERFORMANCE MANAGEMENT ambapo makatibu wakuu, mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya na viongozi wengine wanaweza wakabainisha awali malengo yao na kisha baada ya mwaka wanatathminiwa na hatua zinazofaa kuchukuliwa. Huu mtindo wa mtu anaingiza hasara tu au anaudumaza mkoa au wizara na sisi tunamwachia ndio mambo yaliyotufikisha hapa.

Ninamjua Sharrif kama sikosei maana ni mwalimu wangu wa Menejimenti na pengine tukimpa muda atuingize darasani anaweza kutueleza ni nini hasa anachotaka kutufunza. Kwa upande wangu ninajua Sharrif anaona matatizo yetu makubwa ni DELEGATION, DECENTRALIZATION, COMPETENCY, COMMITTMENT, DEIDICATION na RESOSURCES nyinginezo katika yale tunayotaka kuwafanyia Watanzania. Bwana huyu si mbabaishaji na kila aliyefundishwa naye au kufanya naye kazi akimkosa huona kweli KAPUNGUKIWA. Mzee Sharrif tafadhali tupatie darasa...
 
Wajibu wa kufanyia kazi ni wa watanzania wote,tuko wavivu sana wananchi wa tanzania na hata sisi wananchi hatuko makini na ujenzi wa nchi yetu
 
When faced with poverty, hunger and diseases, peace and tranquility are fairy tales, imaginary things, day dreams and hallucinations. The reality is that pain and suffering, uncertainty, instability and calamities hovers around like a swarm of locust...! Peace, solidarity and tranquility becomes Utopian!
 
Rev,

Utopian at the highest imaginary unit...
manufaa kama tu, dhiki na njaa vipo.
mshikamano unaweza kuwa kwenye malengelenge.
 
hakuna manufaa yoyote, watu wanahitaji wawe na uhakika wa kuishi na sio maisha ya kubahatisha, lakini inawezekana wana amani kutokana na njaa waliyokuwa nayo sio kali sana, la sivyo ungeona damu inamwagika, we unafanya mchezo na njaa bana, haina simile ile
 
When faced with poverty, hunger and diseases, peace and tranquility are fairy tales, imaginary things, day dreams and hallucinations. The reality is that pain and suffering, uncertainty, instability and calamities hovers around like a swarm of locust...! Peace, solidarity and tranquility becomes Utopian!
I does!...'cause most developed countries has risen from poverty, hunger and deseases..innovation usually begins with a Problem, then a NEED come to play..
The big different between them (developed Countries)and us lies on how we Approach the same..It seems that we are driven for Breakdown of the system. Changes means distruction of one system to form another while Problem has always been used in the sense of an ISSUE that need examination not necessarily distruction or breakdown.

We are at the point of breakdown brother..I feel U brother I feel U...Our down fall started with failure to Identify the Problem... that's why we can't even figure out why Tanzania is Poor!..we do have a problem, but we seem blank knowing what is the Problem - other that print out Ufisadi, Povety, hunger and desease..then how can we Identify the Solution!..
We killed Ujamaa to replace with capitalism without contraints becoming the filter. All in the name of distruction...I total believe even the most brilliant ideas are of no use if they are relevant to the specific people and mazingira simply because some redneck told us to, while they on the other hand have their own axes to grid.
The contraint filter vary from country to country, we have local professinal who might have saved the nation then..They have lived our life, faced problem with us, they are among us facing our common enemy..and I assure you they did Identify the problem. Professor Chevji among many other consulted the Government baring in mind what caused all the suffering..both ideas seem off topic, once exposed to the constraints implicit in the gov. mandate of distruction , it prove to be of no values.
We are to blame! us Tanzanians have made up our mind to change Tanzania to become something which we can never be.
it's not about our problem, it's what Tanzania can be in 20 years from now..we aint driven by problem solving (Innovation) since in our case innovation was never designed to improve decaying economic base..and never will, so who U gonna call?
We are doomed brother, we are doomed to fail! - NDIVYO TULIVYO..
 
Kwenye situation kama hii huwa ni kama dormant volcano, kwa hiyo ingawa inaonekana kuna amani na utulivu kwa juu hiyo sio kweli kiuhalisia. kila kundi lina sehemu ya kuegemea na sehemu hiyo ikiondoka basi hiyo volcano hulipuka.

Angalia kundi la wafanyakazi: pamoja na dhiki na njaa kutokana na mishahara kiduchu wana njia zao za kurekebisha maisha kwa mfano warsha, semina, kongamano,kama sio hivyo basi itakuwa siku ya ukoma, siku ya sigara, siku ya sheria serikali za mitaa siku ya macho etc kila kiti tanzania kina siku yake na mamilioni yanatumika siku ambazo hazileti tija hata kidogo, zote hizo zimebuniwa kwenye maofisi ili kurekebisha mifuko yenye utapiamlo. Kundi hili ni mabingwa wa kumantain staus quo hawapendi ibadilike hata kidogo.

Kuna kundi la walalahoi wao hawana warsha wala nini wenye nguvu wanakupiga loba wasio na nguvu wanakaa vijiweni madalali wa nyumba, wapiga debe stendi mishen town etc. Wengine wanagonja tanker la petroli lipinduke ili watoto wale, vinginevyo wanang'oa kingo za madaraja na kuuza kama chuma chakavu na chupa za plastiki kuziuza kwa ajili ya recycling. Hawa wapowapo tuu they have nothing to loose.

Kundi la mwisho ni wanafunzi hawa ni wa kuwaogopa wao wakinyimwa kitu kidogo tu mgomo na maandamano, kundi kubwa la watu discontented na active wako hapa na hawa wakikasirika na kuwa pamoja volcano itakuja kuwa active na matokeo tutayaona, hawa hawana vocabulary ya amani na utulivu. Hawana status quo ya kumantain wao wana future ambayo haiwapi matumaini kabisa.
 
Back
Top Bottom