Japhari Shabani (RIP)
R I P
- Jan 16, 2007
- 721
- 176
Mimi nadhani hapa JK anakosea kitu kimoja. Watu wa kuwaonya ni viongozi wa serikali ambao kila siku hukimbilia vyombo vya habari kuzungumza ulevi wao kana kwamba pale ni mahala pa kuuzwa mchemsho..
Ni busara kwa JK kuwaonya viongozi wake kwanza kuheshimu wadhifa waliopewa na kutumia maneno ya busara wanapowakilisha hoja laa sivyo vyombo vya habari vitaendelea kuchimba zaidi kutafuta ukweli wa vita baina ya wahusika..ambao kwa bahati mbaya ni viongozi wetu na toka chama kimoja.
JK Kwake yeye vyombo vya habari vibaya ni vile vinavyofichua maovu ya viongozi,vinavyopambana na rushwa,mafisadi n.k.Hapa wa kulaumiwa ni yeye mwenyewe na kama kutatokea machafuko uko mbeleni mtu wa kulaumiwa ni yeye kwa kukaa kimya na kutochukua hatua kwa maovu yanayofichuliwa na vyombo hivyo vya habari Kama sio vyombo vya habari tusingejua mikataba mibovu Richmund,Buzwagi,bandari,Reli ,Rada,Mereremeta,EPA mpasuko iliomo CCM n.k.Kwa mtu makini kawa mh.Rais JK ningelipenda kabla ya kutamka mambo hayo angelitoa pongezi kwa vyombo vya habari na waandishi wa habari kwa kazi kubwa walio ifanya na waendelea kuifanya kupambana na maovu hayo kabla ya kulaumu.Ndiyo kunavyombo vya habari ambavyo ni vya hao hao mafisadi vinatumika kupakana matope.Najua ni vigumu kwa JK kuvipongeza vyombo vinavyopigana na ufisadi kwa sababu maovu yote vilivyoyafichua JK hajachukua hatua yoyote kuyatatua.Mh JK vyombo vya habari ni kioo cha jamii ni mahala ambapo wewe na viongozi wote mjitazame na mjione mlivyo Kuvunja kioo hicho sio suluhisho.Mfichaficha maradhi kilio kitamfichua!MUNGU IBARIKI TANZANIA.