Uchaguzi 2020 Je, taarifa iliyotolewa kwa Umma na Dkt. Mahera wa Tume ya Uchaguzi ni ya uongo?

Nimesoma kitu kinachoitwa TAARIFA KWA UMMA iliyotolewa na Tume ya Taifa ya uchaguzi, iliyosainiwa na Mkurugenzi wake Dkt Mahera, tarehe 27/11/2020, naomba maswali yafuatayo uyajibu Dkt Mahera:-

1. Katika taarifa yako kwa Umma umedai kuwa ulipokea majina hayo ya wabunge wa viti maalum, toka kwa Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, tarehe 19/11/2020, je taarifa hiyo ilikuwaje iwe na jina la Nasrat Hanje, ambaye alitolewa gerezani rumande, usiku wa tarehe 23/11/2020 kwa amri ya DPP, Biswalo Mganga, ambako Jeshi lenu la Polisi lilimbambikia kesi ya kukusanyika bila kibali na kutompa dhamana pasipo halali, ambapo alikaa rumande kwa siku 133?

2. Tunakuomba Mkurugenzi wa uchaguzi, Dkt Mahera uutangazie Ulimwengu "kama ubavu huo utakuwa nao" kuwa kauli tuliyosikia kutoka kwa Katibu Mkuu wa Chadema aliyoitoa kwenye kikao na waandishi wa habari hapo tarehe 25/11/2020 kuwa form zenu za Tume ya uchaguzi, alikuwa nazo ofisini kwake zikiwa hazijajazwa hata kidogo na kuwa form hizo hazijatumwa kwenye Tume yenu ya uchaguzi, kuwa ilikuwa ni kauli ya uwongo?

3. Iweje Bunge la Jamhuri la Muungano, chini ya Spika wake Job Ndugai na Katibu wake, Kigaigai, wakiuke kanuni zake yenyewe na kuwaapisha "kisiri siri" tena kwenye eneo nje ya Bunge wabunge hao wa viti maalum, wakati kanuni zinawataka ni LAZIMA tendo hilo lifanyike rasmi ndani ya Jengo la Bunge, kwa kuwa tendo hilo siyo la unyago, ambalo lingehitaji usiri mkubwa?

4. Iweje Spika wa Bunge, Job Ndugai anukuliwe kwa kutoa taarifa kuwa Bunge lake litawalinda kwa gharama zozote wabunge hao wa viti maalum wa Chadema, kama ambaye anajua kuwa uapishwaji wao ulikuwa batili?

5. Iweje Mkurugenzi wa uchaguzi Dkt Mahera usitoe taarifa hiyo nyeti mapema, hadi ungojee sakata hilo la wabunge wa viti maalum wa Chadema, li-trend sana kwenye social media na usubiri chama kikuu cha upiinzani nchini Chadema, kiitishe kikao chao cha dharura cha Kamati Kuu ya Chama chao kuwajadili hao ambao mmewahalalisha kuwa wabunge wateule wa viti maalum?

Kama Dkt Mahera amethubutu kutupa taarifa za uongo kuhusiana na suala la kuapishwa kwa wabunge wa viti maalum wa Chadema, tunawezaje kumuamini kwa taarifa aliyotupa ya matokeo ya uchaguzi mkuu uliopita, ambayo kwa mujibu wake kuwa Rais Magufuli alipata ushindi wa kishindo wa zaidi ya kura milioni 12 ambayo ni zaidi ya asilimia 84 ya kura zote zilizopigwa nchini?

Naomba hayo maswali machache unijibie Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt Mahera ili kuondoa huu utata mkubwa uliogubika zoezi hili zima la kuwaapisha hao wabunge wa viti maalum wa Chadema.
Huwezi kua na kichwa kikubwa ukawa na akili,hiki kichwa kimejaa topeee
IMG_20201114_193805.jpeg
 
Activity za MATAGA zimepungua ghafla kwenye mitandao baada ya kelele nyingi.
Msukuma alikua na press conference jana, akatukana tuna, mara oh CHADEMA ni wahuni, tuone kama wana ubavu wa kuwatimua wabunge 19! Leo yeye ndo muhuni na hoja zake za kuhalalisha bangi na mirungi!
 
Uniona serikali inafanya kitendo cha uhuni kwa kughushi sahihi ya Katibu Mkuu wa CHADEMA na kusema uongo ulio wazi katika mchakato wa kuteuliwa na kuapishwa kwa wabunge wa Viti Maalum wa CHADEMA. Kitendo hiki cha serikali kufanya uhuni kama huu kinathibitisha uhuni mkubwa uliofanyika kwa uchaguzi mkuu uliopita.
Nilikuwa najiuliza, kitengo cha Utawala Bora kinafanya nini?
 
Kwa taarifa hii uliyotoa Dkt Mahera, umetugeuza watanzania wote kuwa ni wajinga, hivi unawezaje kutoa taarifa tarehe 27/11/2020 wakati unajua wazi kuwa mjadala wa wabunge hawa wa viti maalum ulikuwa "so hot" kwenye mitandao yote ya kijamii?

Kila ulipotafutwa Dkt Mahera ili utolee ufafanuzi utata huu wa uteuzi wa wabunge wa viti maalum wa Chadema, ulikuwa ukipiga chenga!

Hadi uliposikia kuwa Kamati Kuu ya Chadema inaenda kukutana ili ifikie maamuzi ya "kuwachinjia baharini" wabunge hao akina Halima Mdee, ndiyo unastuka na kutuletea taarifa hiyo ya uongo kabisa, ambapo hadi mtoto mdogo anayesoma chekechea huwezi mdanganya kirahisi hivyo!
Ninaamini amelishwa hayo maneno na mhutu. Ambaye huwa anajimwabafai kwamba yuko juu ya sheria.
 
Jamani watanzania wenzangu. Kwanini huyo Rais amekuwa vurugu kila mahali? Kuna Nini? Tanzania hatuna wasomi au na wasomi wanaingia kwenye mkumbo huo wa kugushi? Tatizo ni katiba au Sheria za maelekezo na ujanja ujanja. Wasomi na wanasheria hawaoni Kama wanadalilisha taaluma yao?

Kumbuka dhambi au kudhalilika huyaiona wakati huo huo Ila inakuja yenyewe baadae.
 
Nimesoma kitu kinachoitwa TAARIFA KWA UMMA iliyotolewa na Tume ya Taifa ya uchaguzi, iliyosainiwa na Mkurugenzi wake Dkt Mahera, tarehe 27/11/2020, naomba maswali yafuatayo uyajibu Dkt Mahera:-

1. Katika taarifa yako kwa Umma umedai kuwa ulipokea majina hayo ya wabunge wa viti maalum, toka kwa Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, tarehe 19/11/2020, je taarifa hiyo ilikuwaje iwe na jina la Nasrat Hanje, ambaye alitolewa gerezani rumande, usiku wa tarehe 23/11/2020 kwa amri ya DPP, Biswalo Mganga, ambako Jeshi lenu la Polisi lilimbambikia kesi ya kukusanyika bila kibali na kutompa dhamana pasipo halali, ambapo alikaa rumande kwa siku 133?

2. Tunakuomba Mkurugenzi wa uchaguzi, Dkt Mahera uutangazie Ulimwengu "kama ubavu huo utakuwa nao" kuwa kauli tuliyosikia kutoka kwa Katibu Mkuu wa Chadema aliyoitoa kwenye kikao na waandishi wa habari hapo tarehe 25/11/2020 kuwa form zenu za Tume ya uchaguzi, alikuwa nazo ofisini kwake zikiwa hazijajazwa hata kidogo na kuwa form hizo hazijatumwa kwenye Tume yenu ya uchaguzi, kuwa ilikuwa ni kauli ya uwongo?

3. Iweje Bunge la Jamhuri la Muungano, chini ya Spika wake Job Ndugai na Katibu wake, Kigaigai, wakiuke kanuni zake yenyewe na kuwaapisha "kisiri siri" tena kwenye eneo nje ya Bunge wabunge hao wa viti maalum, wakati kanuni zinawataka ni LAZIMA tendo hilo lifanyike rasmi ndani ya Jengo la Bunge, kwa kuwa tendo hilo siyo la unyago, ambalo lingehitaji usiri mkubwa?

4. Iweje Spika wa Bunge, Job Ndugai anukuliwe kwa kutoa taarifa kuwa Bunge lake litawalinda kwa gharama zozote wabunge hao wa viti maalum wa Chadema, kama ambaye anajua kuwa uapishwaji wao ulikuwa batili?

5. Iweje Mkurugenzi wa uchaguzi Dkt Mahera usitoe taarifa hiyo nyeti mapema, hadi ungojee sakata hilo la wabunge wa viti maalum wa Chadema, li-trend sana kwenye social media na usubiri chama kikuu cha upiinzani nchini Chadema, kiitishe kikao chao cha dharura cha Kamati Kuu ya Chama chao kuwajadili hao ambao mmewahalalisha kuwa wabunge wateule wa viti maalum?

Kama Dkt Mahera amethubutu kutupa taarifa za uongo kuhusiana na suala la kuapishwa kwa wabunge wa viti maalum wa Chadema, tunawezaje kumuamini kwa taarifa aliyotupa ya matokeo ya uchaguzi mkuu uliopita, ambayo kwa mujibu wake kuwa Rais Magufuli alipata ushindi wa kishindo wa zaidi ya kura milioni 12 ambayo ni zaidi ya asilimia 84 ya kura zote zilizopigwa nchini?

Naomba hayo maswali machache unijibie Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt Mahera ili kuondoa huu utata mkubwa uliogubika zoezi hili zima la kuwaapisha hao wabunge wa viti maalum wa Chadema.
Inaonyesha dhahili kuwa madai ya CDM kuwa waliiba Kura na kujaza Kura fake kwenye mabox, maana time hi ya Dr Mahera hawana aibu wanaiba Hadi wabunge wa vitimaalum ili kuharalisha dhuluma zao!!
Watanzania wanahitaji majibu sio ubabe na Udikteta, Kama walivyo zoea, dhuluma wizi na mauwaji!!
 
CCM wanakutumia alafu wanakuacha unashangaa, ndivyo itakavyokuwa kwa hao akina Halima na wenzake
Mimi nina mashaka kuwa hawa Wamama kuna uwezekano wameshinikizwa kwa vitisho dhidi ya uhai wao kuyatenda waliyoyatenda. Haingii akilini eti wameshasahau Watz walivyochanga buku buku zao na kuwanusuru kwenye kifungo. Mbaya zaidi eti wamekwenda kuungana na wale waliowabambikizia kesi.

Wamekuwa wakidhalilishwa na hata kutolewa nje ya Bunge na huyu anaewaona leo kuwa wanafaa na atawalinda.
 
Ccm wanalinda maslahi yao, hawana muda na maisha ya hao wamama. Ndugai alisema atakuwa nyuma ya mdee, mdee ageuke nyuma kama ndugai bado yupo au ameshasepa
 
Mtu unakuwa phd holder alfu uchezewenawana siasa Kama wan yomcheze dkt mahela ....naye bila aibu anakimbia kuwaita wahadishi wa hbr kuzungumzia upuuzi namzarau Sanaa. Hyu mzeee
 
Hili Mahera ni POPOMPO LA KISHINDO KUTOKEA NCHINI MWETU TOKA UHURU WA TANZANIA, SIJUI HATA KANISANI ANASALI WANAMCHUKULIAJE WAKIMWONA IBADANI JINGA KWELIKWELI
 
Awamu hii Ina vichaa wa Hali ya juu sana , yaani Chadema ambao hawana dola walipeleka Jina la Nusrat Hanje aliyekuwa jela kwa makosa yasiyokuwa na dhamana ? Kama vile wanajua atatoka ? Mkuu Mahera na udokta wake Hana uwezo wa kujibu haya maswali .
Ni ajabu na kweli!

Ndiyo utendaji wa serikali hii ya kishindo cha awamu ya tano!
 
Back
Top Bottom