Je, soko la HISA ni utapeli?

HIMARS

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2012
Posts
72,994
Reaction score
102,833
Soko la hisa huendeshwa na mwenendo wa kampuni husika.

Iweje hisa za CRDB zisiyumbe baada ya CRDB kukosekana hewani na kuleta shida kwa watumiaji wa huduma zake?

Iweje Vodacom imepata faida ya 90bil ila hisa zake imebaki 580 ile ile?

Tumezoea kuona masoko ya nje kama nasdaq, nyse, lse, hangseng zote hizo ikitokea kampuni imefanya vibaya au vizuri basi athari zinaonekana moja kwa moja (hasi na chanya).

Je DSE wanacheza kwa kuongeza thamani na kushusha wajisikiavyo?

Juzi ORACLE imeongezeka thamani kwa 41% baada ya faida kubwa kuliko matarajio, iweje voda thamani yake ibaki vile vile?
 
Hisa za crdb mbona ziko kwenye downtrend wiki ya pili hii kiongozi! Zilifika all time high hapo mwishoni mwishon wa august na sasa zinafanya correction.

Pili DSE hawapangi bei bali bei inakuwa drived na law ya demand na supply. Wanaozitaka hisa za voda ni wachache kuliko waliotayari kuziuza (wengi wako tayari kucompromise) so bei haiwezi panda kwa minajiri hiyo. Ile inayoonekana pale ndo uhalisia hasa wa bei ya hisa ya voda, achana na ile ya IPO
 
HISA TANZANIA NI UTAPELI KWA ASILIMIA 99%
 
Hakuna utapeli , sema aina ya wateja waliopo ndio wanasababisha wengi wateja wadogo wananunua for long term investment kwahiyo hizi issues ndogo hazina impact , sababu kwa report ya half year iliyotoka june , CRDB inaweza kuongezeka by half or double profit ya mwaka jana ifikapo mwisho wa mwaka, sasa system kuleta issues kwa hizi wiki tena taarifa ilitolewa haitakuwa na impact kubwa sababu wameupgrade waweze kufungua matawi nchi nyingine, kitu chenye faida zaidi
 
CRDB ina matatizo mengi sana, this is just the tip of the iceberg.

Watu wanapoteza tens and hundreds of millions of shillings unaita jambo dogo?

Kuna familia imepoteza zaidi ya shilingi milioni 250 huu sasa ni zaidi ya mwaka wa tatu.

Wewe unasema jambo dogo hili?
 
Hapo nimeelezea upande wa investors , kwasababu wao hawako sensitive na hivyo vitu na vingine hawavijui ndio maana kilichotokea hakijareflect kwenye soko la hisa, ukija upande wa wateja hayo matatizo ni makubwa , sasa kusema tatizo ni dogo au ni kubwa unaangalia tu upande uliopo
 
Investors wanaowekeza pesa nyingi sana CRDB hawajui haya matatizo?

Charles Kimei katoka openly kasema anamuogopa sana rais Magufuli, that alone was a red flag for a sane investor, hawakuona hilo kama tatizo?

Hatuna utamaduni wa investment tu na watu hawajali, na shares haziuzwi kwa kufuata information iliyo kwenye market.

Zingeuzwa kwa kufuata information iliyo kwenye market shares za CRDB zingeshuka sana.

CRDB ikiwapa nafasi watu kuhamisha pesa zao watahamisha sana. Huu si upepo utakaopita tu. Hiki si tati,o la mara moja tu. CRDB imekuwa na matatizo mengi kwa miaka sasa. Hiki la sasa halijatokea ghafla ni matokeo ya mfululilzo wa matatizo mengi ya awali.

How is that good for an investor?
 
Sorry soko kwenye investment Ila Niko kwenye trading thus I've some ideas on another side if coin.
Kampuni kupata faida na kupanda kwa shares Kuna relationship kweli. Kampuni inaweza ikapata faida wanahisa wakapewa gawio Ila price ikabakia Ile Ile Mana hakuna mtu wa kununua hizo hisa regardless ya kuwa kampuni inafanya Vizuri. Ama nakosea hapa. Yaani kupata faida kampuni sio kuwa ndio hisa price zitapanda. Zinaweza zikapanda Bei pamoja ya kuwa kampuni bado hata haipati faida. Mana kupanda kwa value ya shares ni Ile hali ya watu kutaka kununua ama kumiliki hisa za kampuni husika in long term wealth generational.
Nitoe tongotongo
 
bongo dariselama bongo

kuwekeza kwenye financial market ya bongo ni dalili ya ushamba wa kifedha
 
Niliacha kuifuatilia DSE na makampuni yaliyosajiriwa humo baada ya channels na page rasmi za DSE kuifanyia promo ile kampuni ya kilimo ya kitapeli JATU PLC iliyokuwa inauza hisa moja shilingi 5,000.

Kampuni hiyo ilikuwa inalipa wasanii mmojawapo kama sikosei alikuwa Mrisho Mpoto, walikuwa wanapanda kwenye Canter na wanenguaji wakitangaza kushawishi watu wanunue hisa. Nikajua hamna kitu pale, wewe tangu lini mwekezaji akashawishika kwa kutumia wanenguaji. Sasa DSE ndio ilikuwa inapigia promo JATU iliyokuwa sijui ndio inatoa I.P.O muda ule.

Tangu lini TFF regulator wa kandanda ikahamisha Watanzania washabikie Namungo kwenye ligi kuu.
 
Ng'ombe wewe
 
Akili huna
 
Umeongea kitu kikubwa sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…