Je, siri ya China kupunguza umaskini ni nini?

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
Je, siri ya China kupunguza umaskini ni nini?
-------usawa wa kijinsia katika elimu ni muhimu kufanya umaskini ‘kutorithiwa’.
na Hassan Zhou

Ofisi ya habari ya Baraza la Serikali la China hivi karibuni ilitangaza waraka uitwao “Kupunguza Umaskini: Uzoefu na Mchango wa China”. Waraka huo umeeleza jinsi Chama cha Kikomunisti cha China CPC kilivyoongozana na watu wa China kupambana na umaskini katika miaka 100 iliyopita, haswa baada ya mkutano mkuu wa 18 wa CPC, kutokana na juhudi kubwa zilizodumu miaka minane, mwishoni mwa mwaka jana, China ilikuwa imetimiza lengo kuu la kutokomeza umaskini uliokithiri kama ilivyopanga, na kwamba katika kiwango cha sasa ambacho ni juu ya kile cha Benki ya Dunia, watu karibu milioni 100 waishio vijijini wameondokana na umaskini. Je, siri ya China ni nini? Wacha tuangalie jinsi familia kadhaa za kichina zilivyofanikiwa kuondokana na umaskini, ili upate jibu la siri.
QQ图片20210409080658.jpg


Mwalimu Julius Nyerere alisema, “Ukitaka kumsaidia masikini, somesha watoto wake”. Lakini katika juhudi za kuondoa umaskini kwa njia ya elimu, ukosefu wa usawa wa kijinsia ni moja ya vizuizi mbalimbali.
Mwaka 2018, mwalimu wa sayansi Peter Tabichi wa shule moja katika kijiji kilichopo eneo la Bonde la Ufa, Kenya alishinda tuzo ya mwalimu bora duniani. Wanafunzi wote wa shule hiyo walitoka familia maskini, na matukio ya wasichana kuacha masomo kwa sababu mbalimbali ni ya kawaida. Mwalimu Peter alitembelea familia ya wasichana hao mara kwa mara na kuwasihi wazazi wao wasiotaka watoto wao kwenda kusoma na kuwaozesha, wakubali waendelee na masomo yao shuleni.
QQ图片20210409080707.jpg


Ukosefu wa usawa katika kupata elimu kutokana na ubaguzi wa kijinsia pia upo katika baadhi ya sehemu maskini nchini China. Bibi Zhang Guimei aliyefundisha wanafunzi katika sehemu maskini kwa miaka 40 siku zote ana matumaini ya “kuwawezesha watoto wa sehemu maskini waingie katika vyuo vikuu bora”. Baada ya kutafuta michango kwa miaka mingi, mwaka 2008 alifanikiwa kuzindua shule ya kwanza ya wasichana ya serikali ambayo wanafunzi hawalipi gharama yoyote. Wanafunzi wanaoandikishwa katika shule hiyo wote ni wasichana walioshindwa kuendelea na masomo yao baada ya kumaliza masomo ya lazima ya miaka tisa kutokana na umaskini. Na katika miaka 12 iliyopita, shule hiyo imewafikisha wanafunzi zaidi ya 1,800 katika vyuo vikuu. Mwaka 2020, mwalimu Zhang alipata tuzo ya kitaifa ili kupongeza juhudi zake katika kuondoa umaskini.

Nchini Tanzania, zaidi ya theluthi mbili za wanawake hawawezi kumaliza masomo ya shule ya sekondari, huku wanawake nchini Kenya wakichukua theluthi moja tu ya watu wanaosoma elimu ya juu. Mbali na umaskini, sababu nyingine muhimu ya kufanya wasichana kuacha shule ni unyanyapaa dhidi ya wanawake, lakini kuacha masomo kwa wanawake nako pia kutafanya umaskini kurithiwa na kizazi kijacho na kusababisha mzunguko mbaya. Ni kwa kuzingatia elimu tu, wanawake wanaweza kubadilisha hatma yao na hata ya familia nzima, na mwisho kupata kiingilio cha kuelekea maisha bora. Kwani “elimu ni ufunguo wa maisha”.
QQ图片20210409080725.jpg


Miaka 28 iliyopita, picha ya “nataka kusoma shuleni” iliwafanya watu wa China tumkumbuke msichana anayeitwa Su Mingjuan pamoja na macho yake makubwa ya kutamani elimu. Kutokana na msaada wa serikali na jamii nzima, msichana huyo alimaliza shule ya msingi, shule ya sekondari, shule ya sekondari ya juu na mwisho kuingia katika chuo kikuu. Sasa anaishi maisha mazuri, na pia ameanzisha mfuko wa kuwasaidia wanafunzi wa vyuo vikuu wanaotoka familia maskini. Kutoka mtu anayepokea msaada hadi mtu anayetoa msaada, kutoka msichana maskini hadi mtu anayeishi maisha yenye heshima, hadithi ya Su Mingjuan imenikumbusha msemo mmoja wa Kiswahili kuwa “ukimfundisha mwanamke mmoja ni sawa na kuelimisha jamii nzima.”
 
"Hali ya umaskini tunapaswa kupambana nayo kutokana na hali ilivyo na si kupambana kwa kuiga kutoka sehemu nyingine" nimekuelewa sana hapa
 
Back
Top Bottom