Je serikali kuipa BAKWATA hati miliki ya taasisi zote za waislamu ni haki?

Mroojr

Member
Nov 15, 2010
65
8
Sote tunajua walio waislam na wasio waislam kuwa kuna taasisi nyingi za kiislamu na madhehebu mengi ya kiislam kama ilivyo kwa wakristo.

Kuna Makadiani,Mabohora,Washia,Ahamadia,Ismailia,Sunni,Shafiiya(Bakwata) na wengi wengine ambao pengine sikuwataja hapa.

Kwa nembo yao wote hawa wanajiita waislam lakini wametofautiana kiitikadi mambo mengi tu kama ilivyo kwa wakristo wapo wakatoliki,waprotestant,wapentekoste,wasabato nk pia nao wanatofutiana kiitikadi lakini wakatoliki au wapentekoste au wengineo hawajamilikishwa hati miliki ya wakristo wote.

Kwa nini Bakwata wamilikishwe usemaji mkuu na utoaji wa maamuzi ya waislamu wote wakati hawa wote wanatofautiana kiitikadi na pengine kiibada kabisa? We kwa maoni yako unaona inafaa?
 
Bakwata ndio serikali, Kwani waislam walishawahi mchaguwa mufti wao kama wafanyavyo madhebu ya kikristo wachaguavyo viongozi wao. Tanzania ni nchi ya mfumo kristo CC Yericko Nyerere
 
Last edited by a moderator:
Hivi Bakwata ni ya serikali? Ina katiba? kama ipo inasemaji kuhusu wanachama? Je ni kweli serikali ya CCM inazuia hayo madhehebu mengine kuunda mabaraza yao? Kama inazuia, ni kwa nini? Serikali inapata wapi nguvu za kisheria/kikatiba ya kufanya hivyo?
 
Ujinga si tusi bali ujinga ni kutoju sasa huyu jamaa ni mjinga anataka kujua ingawa sio muislam na chokochoko zake Mkuu ukimtukana mzazi wa mwenzako, usitegemee wazazi wako waendelee kupata heshima toka kwa wenzio.
 
Wewe Mroojir upo kwenye taasisi gani kati ya hizo ulizotaja?
Ni vyema ukatoa hoja na kuitetea hoja yako ili wadau wapate pa kushikilia kuliko kuuliza kama mpita njia ktk kesi ya mke na mmewe.
 
Fungua kesi ya madai mahakamani acha kulalamika!!!!!!!
Mkuu huyu sio Muislam huyu ni moja ya hawa wanaotupambanisha hapa, hakuna Muislam wala Mkristo, anaehitaji kujua jambo juu ya imani yake alafu aulizee hapa huku akijua wengi watakamjibu hawana ufahamu na mada husika.
 
Sisi waislamu elimu akhera imetufanya tuishi kwa kuwaamini majini. Elimu dunia imetupiga chenga tumebaki kama wakiwa. Serikali kila kukicha inatubemenda. Tumebaki wakiwa
 
Mimi ni mwislamu.Nimeyasema haya kwa sababu mara kwa mara inatokea migongano katika maswala mbali mbali ikiwema maswala ya kufunga kufungua ramadhani,kuswali idd na mambo mengine kama haya.Miaka ya nyuma kidogo bakwata ilishawahii kuutangzia umma hawa wanaofunga kabla ya wenzao si waislam na hao wanaosali idd mapema sio waislamu na waliomba vyombo vya dola kuwatawanya wasisali idd wakasahau hata katiba ya nchi inamruhusu kila mtu kuabudu anachotaka alimradi asivunje sheria ya nchi. Mpaka sasa bado hali hiyo inaendelea ya kuwasemea waislamu wote bila kujali itikadi zao.
 
Au ktk kumbukumbu zenu mlishawahi kusikia wakatoliki wanaiomba serikali kuwazuia wasabato wasisali jumamosi? Au huu ni upungufu tu wa elimu walionao masheikh
 
Wakristo kuna makundi ma4 tu ya madhehebu: 1.ROMANI KATORIKI(LIMO KUNDI DOGO LA WAKALIZIMATIKI WANAOFUATA MFUMO WA KILOKOLE) 2. WALOKOLE( NA WAKUNDI YAKE WAKIWA WAMETEKA BAADHI YA MADHEHE YA KIPROTESTANTI YALIYOKOSA MWELEKEO WAO WA ZAMANI. HAWANA SINGI AU NGUZO YOYOTE YA IMANI YAO) 3.WAPROTDSTANTI(WAPINGAJI WA MAFUNDISHO YA MKATORIKI HASA YASIYOTKANA NA BIBLIA, mfano. angalikana, lutherbn/kkt, wasabato, babtisim, pentekoste, othodox, waldensia ambamo walitokea wasabato, prestelia, methodist n.k) 4.MADHEBU/MAKUNDI YALIYO TOKA NDANI YA UPROTESTANTI AU ULOKOLE aidha kwa sababu fulani.
 
Bakwata iliundwa na serikali baada ya kuona waislam hawana baraza la kuwasemea. Uliza utaambiwa. ndio maana Sheikh mkuu analipwa na serkali. na siku zote Bakwata inaitetea serkali na serkali nayo haiitupi Bakwata ndio maana Bakwata ishapewa viwanja vizuri sana na serkali
 
Sote tunajua walio waislam na wasio waislam kuwa kuna taasisi nyingi za kiislamu na madhehebu mengi ya kiislam kama ilivyo kwa wakristo.

Kuna Makadiani,Mabohora,Washia,Ahamadia,Ismailia,Sunni,Shafiiya(Bakwata) na wengi wengine ambao pengine sikuwataja hapa.

Kwa nembo yao wote hawa wanajiita waislam lakini wametofautiana kiitikadi mambo mengi tu kama ilivyo kwa wakristo wapo wakatoliki,waprotestant,wapentekoste,wasabato nk pia nao wanatofutiana kiitikadi lakini wakatoliki au wapentekoste au wengineo hawajamilikishwa hati miliki ya wakristo wote.

Kwa nini Bakwata wamilikishwe usemaji mkuu na utoaji wa maamuzi ya waislamu wote wakati hawa wote wanatofautiana kiitikadi na pengine kiibada kabisa? We kwa maoni yako unaona inafaa?

Sasa chama gani ni cha kidini?
 
Yap, nakuunga mkono, kwani Nyerere alifanikiwa kuziweka baadhi ya jumuia za kidini ndani ya ccm ili kumsaidia utawala
 
Bakwata iliundwa na serikali baada ya kuona waislam hawana baraza la kuwasemea. Uliza utaambiwa. ndio maana Sheikh mkuu analipwa na serkali. na siku zote Bakwata inaitetea serkali na serkali nayo haiitupi Bakwata ndio maana Bakwata ishapewa viwanja vizuri sana na serkali

Kwa maana hiyo Serikali yetu inaendeshwa(kimfumo na utekelezaji) katika misingi ya Udini?(Uislamu)
 
Sote tunajua walio waislam na wasio waislam kuwa kuna taasisi nyingi za kiislamu na madhehebu mengi ya kiislam kama ilivyo kwa wakristo.

Kuna Makadiani,Mabohora,Washia,Ahamadia,Ismailia,Sunni,Shafiiya(Bakwata) na wengi wengine ambao pengine sikuwataja hapa.

Kwa nembo yao wote hawa wanajiita waislam lakini wametofautiana kiitikadi mambo mengi tu kama ilivyo kwa wakristo wapo wakatoliki,waprotestant,wapentekoste,wasabato nk pia nao wanatofutiana kiitikadi lakini wakatoliki au wapentekoste au wengineo hawajamilikishwa hati miliki ya wakristo wote.

Kwa nini Bakwata wamilikishwe usemaji mkuu na utoaji wa maamuzi ya waislamu wote wakati hawa wote wanatofautiana kiitikadi na pengine kiibada kabisa? We kwa maoni yako unaona inafaa?

Mkuu hakuna dhehebu la wakristo linaloitwa "Protestant" labda kama unapenda kuicheza ngoma ya Wakatoliki, hapo sawa. Kwa taarifa yako dhehebu lolote nje ya Wakatoliki wao wanawaita Protestant kwa maana wanakwenda kinyume na matakwa na mafundisho ya wakatoliki.

Tiba
 
Ok fanya Bakwata ndio iwe mwakilishi wa taasisi na madhehebu haya,uwakilishi wake unafaa? Nasena hivi kwa sababu haichukui rai au maoni au mapendekezo ya taasisi zingine ili kuleta uwakilishi mzuri badala yake itakalo taka Bakwata ndio liwe la taasisi zote. Je huo sio udikteta?
 
Wakristo kuna makundi ma4 tu ya madhehebu: 1.ROMANI KATORIKI(LIMO KUNDI DOGO LA WAKALIZIMATIKI WANAOFUATA MFUMO WA KILOKOLE) 2. WALOKOLE( NA WAKUNDI YAKE WAKIWA WAMETEKA BAADHI YA MADHEHE YA KIPROTESTANTI YALIYOKOSA MWELEKEO WAO WA ZAMANI. HAWANA SINGI AU NGUZO YOYOTE YA IMANI YAO) 3.WAPROTDSTANTI(WAPINGAJI WA MAFUNDISHO YA MKATORIKI HASA YASIYOTKANA NA BIBLIA, mfano. angalikana, lutherbn/kkt, wasabato, babtisim, pentekoste, othodox, waldensia ambamo walitokea wasabato, prestelia, methodist n.k) 4.MADHEBU/MAKUNDI YALIYO TOKA NDANI YA UPROTESTANTI AU ULOKOLE aidha kwa sababu fulani.

kwanza hujui pili sijui unamweleza nani
 
Back
Top Bottom