Mgeni wa Jiji
JF-Expert Member
- Jul 27, 2017
- 10,484
- 19,987
Habari za muda wana JF
Nimefuatilia kwa muda matukio mbali mbali yanayoendelea kwa sasa nchini kwetu na nimeona niweke uzi huu kujadili athari chanya au hata hasi inayoweza kuletwa na matukio haya. Kwa leo nitajadili suala la kuwepo kwa mgombea binafsi.
Turudi kwenye yaliyojiri kwa siku za hivi karibuni kisiasa.
Katika siku za hivi karibuni, tumeshuhudia maelekezo yanayoelekeza kuenguliwa Mbunge wa Kisesa, Mh. Luhaga Mpina, kwenye mchakato wa kura za maoni ndani ya chama chake cha CCM. Hili si tukio la kwanza kushuhudia mgombea maarufu mfano Askofu Gwajima au kiongozi aliyewahi kushika nafasi ya juu ya uongozi akiondolewa katika hatua za awali za uteuzi wa chama kama ilivyotokea kwa baadhi ya wanasiasa mwaka 2020. Lakini tukio hili linaibua mjadala mpana kuhusu haki ya raia binafsi kushiriki katika uongozi bila kupitia vyama vya siasa. Swali kuu linabaki: je, sakata hili linaamsha tena hitaji la mgombea binafsi?
Tuiangalie kwa kifupi sana historia ya Mgombea Binafsi;
Katika historia ya Tanzania ya kisiasa, suala la mgombea binafsi lilishika kasi zaidi mwaka 2006 baada ya mwanasheria maarufu, Ndugu Christopher Mtikila, kuibua hoja hiyo mahakamani. Mahakama ya Rufaa iliamua kuwa kuzuia mgombea binafsi ni kinyume na Katiba. Hata hivyo, kwa muda mrefu, Tume ya Uchaguzi na serikali zilishikilia msimamo wa kutoiruhusu kwa sababu za kiutendaji na kisiasa.
Muktadha wa Kisasa juu ya hoja ya mgombea binafsi
Katika mazingira ya sasa ya kisiasa, ambapo malalamiko kuhusu mchakato wa ndani wa vyama yameongezeka ikiwemo madai ya upendeleo, rushwa, au kutokuaminika kwa vikao vya maamuzi haya yakiwa kwa vyama vyote vilivyopo. Wananchi wengi wameanza kuhoji iwapo vyama vya siasa bado ni njia pekee ya haki na uwakilishi wa kweli. Sakata la Mh. Mpina linatoa mfano hai wa hali hiyo. Wafuasi wake na baadhi ya wachambuzi wanadai kuwa aliadhibiwa si kwa sababu ya kutokuwa na sifa, bali kwa sababu ya msimamo wake binafsi.
Sasa ni upi umuhimu wa Mgombea Binafsi ili tujadili kama suala hili ni hoja ya msingi kwa sasa nchini kwetu.
Kuwepo kwa mgombea binafsi kunaweza kusaidia:
1. Kuongeza ushindani na uwajibikaji miongoni mwa wanasiasa.
2. Kutoa fursa kwa watu wenye maono lakini wasiokuwa na maslahi ya vyama.
3. Kuzuia ukiritimba wa vyama katika maamuzi ya uwakilishi wa wananchi.
Mbali na umuhimu wake pia hatuwezi kukataa wala kubishania kuwa pia kuna changamoto zinazoweza kuja na uwepo wa mgombea binafsi
Pamoja na faida, mgombea binafsi pia anakabiliwa na changamoto kama:
Hitimisho
Kwa kuzingatia matukio mbali mbali ya kisiasa yanayoendelea kutokea ni wazi kuwa mjadala wa mgombea binafsi unazidi kupata nguvu mpya. Je, hii ni dalili kuwa umefika wakati Tanzania kuwa na mfumo unaotoa fursa pana za ushiriki wa kisiasa usiofungwa na makundi au miiko ya vyama?
Wasalimu.
Pascal Mayalla
Mshana Jr
johnthebaptist
Lucas Mwashambwa

- Kukosa mtandao wa kisiasa au kifedha.
- Kutojulikana kitaifa kama wagombea wa vyama.
- Changamoto za kisheria na kimfumo kuhusiana na usimamizi wa uchaguzi.