Je, ripoti ya Mwakyembe kuhusu Richmond ilificha nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, ripoti ya Mwakyembe kuhusu Richmond ilificha nini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mag3, Jan 29, 2009.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  Jan 29, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Kuna wakati Dk. H. Mwakyembe, mbunge wa Kyela alimtaka Spika avunje kanuni na kurejesha suala la Richmond bungeni ili aweze kuyaanika hata yale ambayo walibaki nayo moyoni kwa ajili ya kuinusuru serikali. Hii kauli aliitoa katika hali ya kujikosha baada ya ripoti yake kushutumiwa na baadhi ya watuhumiwa kuwa ilifanyiwa ukarabati nje ya muda wake. Kuna sisi wengine tuliokuwa na duku duku moyoni wakati ule lakini watetezi walikuwa wepesi kutuita wabishi, wasioambilika, wakorofi na walio na lao jambo.

  Siri ya wizi mkubwa Richmond - Mwandishi Wetu, Raia Mwema - Januari 28, 2009.
  Watimka na mabilioni ya walipa kodi - Walichotewa kabla hata ya kazi !!!


  WAKATI Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akisubiriwa na wabunge kuwasilisha taarifa ya Serikali kuhusu utekelezaji wa mapendekezo ya Bunge kuhusu kampuni ya Richmond Development, kampuni hiyo iliyorithiwa na kampuni ya Dowans, ilitokomea na zaidi ya Sh. bilioni 23, Raia Mwema imebaini.

  Kinyume cha maelezo yaliyowahi kutolewa na baadhi ya viongozi wakuu serikalini katika Bunge, kwamba Richmond haikuwahi kupewa fedha za Serikali, ukweli ni kwamba kampuni hiyo ilichotewa zaidi ya Sh. bilioni 30 (Dola 30,696,598 za Marekani).

  Kiasi hicho ni sawa na asilimia 35 ya gharama ya kodi ambayo msingi wake ulikuwa kufanikisha mchakato wa ufunguaji wa hati ya muamana (letter of credit) kati ya kampuni hiyo na Benki ya Biashara.

  Malipo hayo ya asilimia 35 ni utekelezaji wa makubalino yaliyofikiwa awali, kati ya Serikali na wawakilishi wa kampuni ya Richmond Development.

  Uchunguzi wa Raia Mwema umebaini kuwa baada ya kupewa kitita hicho cha zaidi ya Sh bilioni 30, Richmond ilipewa masharti ya kurejesha fedha hizo serikalini katika malipo ambayo yangefanyika kwa awamu tatu.

  Hesabu zilizofanywa ni kwamba Richmond ilitakiwa kurejesha serikalini dola 1,279,044 za Marekani (zaidi ya Sh bilioni 1.3), kila mwezi, lakini katika mikupuo (awamu) mitatu.

  Hesabu hizo zinabainisha kuwa kama makubaliano hayo yangefanyika bila ukorofi au kasoro yoyote, Richmond ingefanikiwa kurejesha serikalini fedha ilizopewa katika miaka miwili. Kwa tafsiri nyingine ni kwamba, Richmond ingelipa deni hilo serikalini ndani ya muda wa uhai wa mkataba wake na Serikali, ambao ni miaka miwili.

  Lakini uchunguzi zaidi wa Raia Mwema umebaini kuwa malipo ya awali yalipaswa kuanza kufanyika Novemba, mwaka 2007. Hata hivyo, kutokana na utata wa kampuni ya Richmond hasa kwa upande wa uwezo wake kiteknolojia na utendaji, kampuni hiyo iliuza shughuli zake kwa kampuni nyingine binafsi ya Dowans.

  Imebainika kuwa wakati mchakato wa uuzaji wa shughuli za kampuni hiyo kwa Dowans unafanyika, Richmond ilikuwa haijarejesha fedha ilizopewa na Serikali na kwa kuwa Dowans ndiyo iliyobeba mikoba, ilipaswa kuendeleza urejeshaji huo wa fedha.

  Kutokana na hali hiyo ya fedha za Serikali kubaki kwa 'wawekezaji' hao waliopasiana mpira wa uwajibikaji, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kupitia timu ya watalaamu wa sheria, ilichunguza mkataba kati yake na Richmond ambao ulirithiwa na Dowans.

  Taarifa ya timu ya wanasheria wa TANESCO ilibaini kuwa mkataba huo hauna nguvu za kisheria na kuamuru uvunjwe. Mkataba ukavunjwa rasmi Agosti mosi, mwaka 2008.

  Hata hivyo, wakati mkataba huo unavunjwa uchunguzi wa Raia Mwema umebaini kuwa fedha zilizopaswa kurejeshwa Serikali hazikuwa zimerejeshwa zote.

  Imebainika kuwa fedha zilizorejeshwa hadi mkataba unavunjwa ni jumla ya dola 7,674,186 za Marekani (zaidi ya Sh bilioni 7.7), huku dola za Marekani 23,022,412 (zaidi ya Sh. bilioni 23) zikibakia kwa Richmond na mrithi wake Dowans.......................................................................................
  .................................................................................................
  Katika mkutano wa Bunge ulioanza wiki hii, Serikali inatarajiwa kuwasilisha taarifa yake kuhusu utekelezaji wa mapendekezo hayo. Taarifa hiyo inatarajiwa kuwasilishwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.


  Duh, sh. 23,000,000,000/= je kuna uwezekano kuwa tulipewa changa la macho na kuna zaidi kuhusu Richmond. Hivi nchi yetu ilipata hasara gani kwa ujumla wake kutokana na mkataba wa Richmond na kukosekana kwa umeme kwa karibu mwaka mzima. Kuanzia na hili tujiulize - ni siri ngapi Dr. Mwakyembe alizificha kuisetiri serikali ?? Je ni haki bunge kufichwa taarifa muhimu zinazohusu maslahi ya taifa ??
   
 2. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #2
  Jan 30, 2009
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Vema wakuu mmelileta hata ninyi wenye kuheshimiwa sana humu. Tulihoji awali juu ya kauli ya mkuu wetu mwakyembe
   
 3. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #3
  Jan 30, 2009
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,203
  Trophy Points: 280
  Hawa watu wanaosema wanataka Mkapa aondolewe kinga ndio ambao wanachelewesha Justice.
  Wapo watu wengi hapa hawana kinga ya Bunge,lakini we do not see them getting roundly rounded up and taken to Court.
   
 4. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #4
  Jan 30, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu umenena la maana sana. Sijuini kwanini macho yetu yanaelekezwa kwa Mkapa zaidi wakati kila jambo linatakiwa kwenda kwa hatua. Mkapa yuko hatua ya tano, tunatakiwa kwanza tupite hatua nne ili tufike ya tano. Kina EPA wakamatwe kwanza wakifikishwe mahakamani waseme wanayotakiwa kusema ya yajulikane, na kuwekwa wazi yanayotakiwa kuwa wazi, hapo hatua itapigwa na kumfikia Mkapa.
   
 5. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #5
  Jan 30, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Sh.. sh ! Angalia wakuu wenyewe wasikusikie wasije wakakushukia kama mwewe - kwao mimi ni kifaranga tu.

  Hizo sh. 23,000,000,000/= hazikuwa na umuhimu kwa bunge. Je katika kipindi kama hicho mkuu wa kaya aliwahi kutembela Houston, Texas ? Je, ripoti ya tafrija aliyofanyiwa balozi wetu huko Texas na heshima ya mji aliyopewa, Mwakyembe na timu yake waliipata? Je mwenyeji wa hao waheshimiwa Houston, Texas alikuwa nani ? Maswali, maswali - na yapo mengi tu.
   
 6. M

  Mkandara Verified User

  #6
  Jan 31, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Wakuu,
  Sielewi swala hili linaingiliana vipi na kauli ya Mwakyembe ambayo sote alituacha solemba.. Lakini kwa report hii ambayo inazungumzia fedha zilizobakia baada ya Richmond kuondoka inahusiana vipi na ile report ambayo ilikuwa kutazama Uhalali wa mkataba huo.. Licha ya yote haya wakati report inatengenezwa ama kuchunguzwa hao Richmond walikuwa bado ktk mkataba na kama mnakumbuka kuna viongozi waliokuwa wakipiga vita hata upelelezi wake. Jamani through process hiyo ndio tumejua mengi kuhusiana na mkataba ule haikuwa swala la kutafuta wachawi..

  Yes, kutokana na report yoyote ile kuna vitu ambavyo hutakiwi kuvisema ikiwa havihusiani na report hiyo isipokuwa vinaweza kutumika kama ushahidi iwapo kutakuwepo na mahakama au bunge teule kwa ajili ya shitaka litakalo wekwa mezani..Ni rep[ort kama hii inakupa picha ya kufungua mashtaka iwe kwa uzembe wa kuliingiza taifa hasara ama hujuma za uchumi na kadhalika..

  Kama mnakumbuka hata ile scandal ya Watergate, Iran -Iraq Contra na kadhalika kuna baadhi ya maelezo hayakutolewa hadi kesi hizo zilipofika mbele ya sheria (bunge lao teule).. Na Nixon kama Lowassa alikuwa jeuri akifikiria kwamba hawajui kitu lakini siku ukweli ulipobainika na nyaraka (tapes) kutolewa ndipo alipokubali na kuabika vibaya vibaya..kabla ya hapo sote tulikuwa kizani kabisa tukijua tu machache yanayohusiana lakini sio key players!
  Sasa hatuwezi kumhukumu Mwakyembe hata kidogo ndio utaratibu wa report zote.. Warioba na ile ya Corruption kuna mambo kibao (pamoja na list ya wakulu) hakuyaweka mle isipokuwa nyaraka alikuwa nazo kuthibiti baadhi ya dondoo zake..

  Kwa hiyo, nadhani hakuna haja kabisa ya ku jump the gun wakati bunge letu bado kabisa halijafikia maamuzi ya kuwasimamisha wahusika..why? hata sielewi! lakini siku ya siku itakapofika Mwakyembe ataitwa na kupekuliwa zaidi ktk kila kipengele cha report yake na hapo ndipo mtajua mganga nani..
  Kitu cha kujiuliza leo hii - Ni kwa nini bunge letu pamoja na serikali inakawiza swala hili kufika mbele ya sheria!..

  Je, inaweza kuwa changa la macho kama lile l report ya Warioba!..Kumsakama Mwakyembe wakati kawakilisha kile mlichomtuma kuchunguza ni kutafuta mchawi..na kibaya zaidi tunatumia ramli na kuunganisha vitu badala ya kusoma picha nzima kuwa matatizo yetu hayakuanza na Kikwete ila CCM kwa ujumla na ndio maana sisi wananchi tunataka toka Mkapa hadi hawa kina Lowassa wafikishwe mbele ya sheria..Laukama tutakazania tu Lowassa bila kumtaja Mkapa basi utawasikia watu wa Lowassa wakisema mbona Mkapa hazungumzwi..

  Jamani issue ya Richmond ktk magazeti yote nchini ndiyo imechukua nafasi ya kwanza kwa mwaka 2007-8 wote... iweje leo tukimzungumzia tu Mkapa mnakuwa wakali na kuanza kupima mabaya ya mhusika badala ya kuwa hawa wote ni criminals hakuna mmoja mwenye nafuu hapa. Nyie zungumzieni Richmond tutachangia, nasi tutazungumzia Mkapa tunawaomba mchangie kwani uwanja ni mkubwa sana ktk sheria na mahakama sio moja tu..
   
 7. I

  Ijabu Issa Member

  #7
  Jan 31, 2009
  Joined: Apr 29, 2008
  Messages: 56
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mag3

  Mkuu Mag3,
  Hoja yako ni nzito na inastahili utulivu kuichambua kwa undani. Mimi mwenyewe ni mdau wa suala hili la Richmond kwani kashfa ya Richmond ni sehemu ya utafiti wangu wa shahada ya uzamili kwenye chuo kimoja hapa nchini. Nimeipitia taarifa ya kamati ya Dk. Mwakyembe yenye jumla ya kurasa 574 (juzuu ya viambatisho yenye kurasa 382 na juzuu ya uchambuzi wa kina yenye kurasa 165). Natumaini Bunge lina mpango wa kuchapisha (publish)taarifa hiyo yote kuwa vitabu vinavyoweza kuuzwa madukani na kuweza kusomwa na Watanzania wote.

  Mbali na taarifa hiyo ya kina, nimezungumza kwa nyakati tofauti na Dk. Mwakyembe, Eng. Manyanya, Eng. Mnyaa, Mhe. Selelii na Mhe. Mntangi (wajumbe wa kamati teule) na nilihudhuria mhadhara (lecture) ya Dk. Mwakyembe pale Mlimani mwaka jana mwishoni kwa wanafunzi wa somo la Sheria ya Katiba (Constitutional Law). Hivyo nawezajaribu kujibu baadhi ya maswali na kufichua "kidogo sana" matokeo ya utafiti wangu maana hapa JF kuna vichwa vinavyoweza kutumia matokeo ya utafiti wangu kujipatia digrii ya masters elsewhere kabla yangu! WanaJF hapa natania tu, msinisulubu kwa hii light touch!

  Kwa nini Dk. Mwakyembe alimwomba Spika atengue kanuni ili wamwage ----- zaidi wa kuifedhehesha Serikali? Kufuatana na Dk. Mwakyembe na wenzake, walichukizwa na kitendo cha watuhumiwa wa Richmond kuanzisha magazeti mapya na kutumia mengine ya zamani (wanayomiliki) kuanza kujisafisha kwa lengo la kuuthibitishia umma kuwa kamati teule iliwaonea. Wapambanaji hawa wanasema walikerwa zaidi na kitendo cha uongozi wa Bunge kuwaangalia tu watuhumiwa hawa na "wafuasi wao" wakitamba ndani na nje ya Bunge bila kukemewa. Hiyo ndiyo sababu iliyomfanya Dk. Mwakyembe, kwa niaba ya wenzake, kuliomba Bunge kutengua kanuni ili waseme hata yale ambayo hawakuyasema ambayo yangeiweka Serikali kwenye fedheha kubwa.

  "Kwa nini hayo masuala nyeti hamkuyasema toka mwanzoni?", niliwauliza wabunge hawa watano. Majibu yao wote yalifanana. Nitamnukuu Dk. Mwakyembe kutokana na nafasi yake ya kuongoza kamati na ujuzi wake wa sheria. Alisema, unapofanya uchunguzi, unakusanya ushahidi mwingi sana ili mtuhumiwa akikana, abanwe na ushahidi huo. Kwa suala la Richmond, walikusanya ushahidi mwingi sana wakitegemea kuutumia ikiwa Lowassa, Karamagi na Msabaha wangekataa kujiuzulu. Lakini wakakiri makosa haraka haraka na kujiuzulu. Fursa ya kamati kutoa ushahidi ikapotea! Dk. Mwakyembe alijieleza polepole kuwa hata mahakamani, mtuhumiwa akikiri kosa, huendelei kutoa ushahidi na kuita mashahidi!

  "Ushahidi gani nyeti mlikuwa nao ambao mliuficha kwa wabunge?" Dk. Mwakyembe na wenzake wanasema hawakuficha ushahidi wowote, ila mazingira ya suala lenyewe yaliwanyima fursa ya kutoa ushahidi wote. Aidha kulikuwa na ushahidi wa ziada ambao hakika ungeiaibisha Serikali kama wangeutoa. Wanatoa mfano wa mtuhumiwa wa kosa la jinai la kubaka. Wanasema mnaweza kuwa na ushahidi wa msingi na wa ziada dhidi yake. Kwa mfano, kwamba mtuhumiwa alikuwa na chupi iliyotoboka matakoni alipotenda kosa hilo. Huo si ushahidi wa msingi, ni ushahidi wa ziada. Akijidai mbishi, ushahidi wa aina hiyo ni muafaka kutolewa kuthibitisha kuhusika kwake na kosa!

  Wanakamati wa Richmond wanasema walikuwa na ushahidi mwingi wa aina hiyo: Mawaziri wakiwa wamevaa kapelo kwenda nyumbani kwa mmiliki wa Richmond (sehemu za Upanga) usiku wa manane; viongozi kwenda Houston Texas "kupumzikia kwa Bw. Gire", n.k. ni ushahidi ambao akina Lowassa wangejifanya ngangari wangeutoa kwa furaha kubwa. WanaJF mengi mtayasoma kwenye Masters Dissertation yangu ambayo hakika nitaichapisha kuwa kitabu nikifaulu!

  Niliona niwamegee pande hili kwa sasa. Kazi waliyoifanya wabunge hawa watano ni kubwa, ya kihistoria, ya kujitoa mhanga, ya kizalendo na imebadilisha kabisa mwelekeo wa siasa, utawala na demokrasia nchini.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #8
  Jan 31, 2009
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ijabu Issa

  Mkuu heshima kwako.
  Hapo umenigusa sana na huu uchambuzi. . .nafurahi kwamba unachukua shahada ya uzamili ( na kwa mwelezo yako i guess ni sheria).

  Tunahitaji watu kama wewe katika maendeleo yako. Hope utafanya vyema kwa maendeleo ya taifa. Ila huoni kauli ya mwakyembe ilileta utata hasa baada ya watu kumwamini?

  Nafikiri ni vyema akatoa maelezo kuweka sawa mambo yake.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. I

  Ijabu Issa Member

  #9
  Jan 31, 2009
  Joined: Apr 29, 2008
  Messages: 56
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ahsante Mkuu Calnde. Hata mimi niliona kuwa Dk. Mwakyembe na wenzake walikuwa na mambo mengi mazuri sana ambayo wangeyatolea ufafanuzi kwa wananchi. Lakini kuongea nao kumenisaidia sana kuelewa mambo ya Bunge.

  Bunge lina ukiritimba wa ajabu sana. Wanadai kuwa madaraka yao kufafanua suala lolote kuhusu Richmond yaliisha siku Bunge lilipopitisha maazimio yake 23, tarehe 15 Februari, 2008. Msemaji anakua Spika, Naibu Spika au Katibu wa Bunge.

  Hiyo ndiyo hali yenyewe. Kwenye kazi yangu ya uzamili, naongelea vilevile Kanuni za Bunge kama hizi ambazo hazisaidii kupanua demokrasia ila zinakuza ukiritimba. Asante Mkuu.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. M

  Mtu wa Kawaida JF-Expert Member

  #10
  Jan 31, 2009
  Joined: May 2, 2008
  Messages: 217
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Mkuu,
  Kweli umegonga kwenyewe, Kama mtu umepewa tume ya kuchunguza kitu na umemaliza kufanya kazi na kupeleka ripoti, ni vyema ukasema vyote na sio kutoa kauli kwamba hautaongea maengine kwa kuifichia serikali aibu.

  Mwakyembe na kamati yake walipaswa kusema yote waliyotumwa na sio kuficha habari nyingine ili kulinda serikali. Kwa kuficha baadhi ya mambo kunaleta ulakini fulani.

  Kama walikuwa wanautegemea wakati muafaka kuleta hizo taarifa nyingine si hawaoni kwamba hakuwatendea haki wapigakura wao kwa kuwanyima taharifa kamili?

  Je adidu za rejea ziliwapa mwanya wa kutokusema mambo yote kwa wananchi/bungeni. Je hayo ambayo hawayakusema waliyafikisha kwa Spika aliyewapa hii kazi?
   
 11. F

  Fataki Senior Member

  #11
  Jan 31, 2009
  Joined: Aug 28, 2008
  Messages: 151
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu,
  ukisoma vizuri maoni ya mtaalamu Ijabu Issa utagundua kuwa Lowassa na wasiri wake Msabaha na Karamagi walilizidi Bunge maarifa kwa kujiuzulu kwanza halafu wakaanza kulalamika baadaye. Kujiuzulu, Ijabu Issa anasema, kuliimaliza kesi papo hapo!

  Mwakyembe na wenzake wasingeweza kuomba waendelee na ushahidi ili tu sisi tufaidi madataz waliyoyapata wakati wa uchunguzi!

  Kama Lowassa na wenzake wangeendelea kung'ang'ania madaraka, Dk. Mwakyembe na timu yake wangetakiwa kutoa ushahidi wote bila kuficha chochote ili kuwawajibisha watu hao!

  Kulaumu leo kuwa Mwakyembe & Co. walificha ushahidi, si sahihi kwani watuhumiwa waliamua kuwajibika! Mbali na hayo, nani kati yetu kasoma hizo kurasa 547 za Kamati ya Mwakyembe?

  Waliosoma taarifa hiyo yote wanadai kuwa maswali yote ya msingi yanapata majibu!
   
 12. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #12
  Jan 31, 2009
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  Hapo umezidi kunigusa...

  Japo spika anajitahidi lakini kuna namna amekuwa akizima mambo katika namna ambayo siipendi.Na kuhusu sheria nafikiri kuna haja ya sheria za bunge zilizopitwa na wakati zibadilishwe. Kwa ujumla hata sheria zetu nyingi na katiba yetu which is GRUND NORM vinahitaji mabadiliko.

  Mfano wakati Ibara ya 107 inaipa mahakama uwezo wa kuwa chombo cha mwisho in administration and provision of justice katiba hiyo hiyo inaipa tume ya uchaguzi nguvu kubwa kuliko hata Mahakama yarufaa juu ya uchaguzi wa raisi kwamba tume ikishamtangaza no other court of law can Question him.

  Binafsi hili ni Tatizo. Kwa Tanzania and I think in most African countries Executive is too powerful and this in one way or another it may account for long time experienced coups in Africa. I believe unaandika dissertation.

  Hivi wanazifanyia kazi kweli au ndo zinajazwa vumbi kwenye library za vyuo vyetu?
   
 13. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #13
  Jan 31, 2009
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  kurasa 547 zisikutishe sana mkuu maana ujue hotuba nyingi hasa za viongozi wa serikali ( nimebahatika kusoma chache za spika in original copy)huandikwa kwa herufi kubwa na huacha nafasi kubwa kati ya mstari na mstari. (nadhani kurahisisha swala zima la usomaji).Tatizo lililojitokeza ni kitendo cha Mwakyembe kusema kuna mambo ambayo hawakuyasema. Hata hivyo,being a constitutional lawyer, Mwakyembe ameweza kufafanua vizuri kauli yake hasa kupitia mahojiano yake na ndugu ijabu issa, hasa kupitia mfano wa chupi iliyotoboka. Cha msingi watu waelewe kazi ya Mwakyembe ilifanyika vyema and in any way so long walifanya kazi yao as court of inquiry under limited period of time,lets give devil his due.
   
 14. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #14
  Jan 31, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280

  Nafurahi umeipitia taarifa nzima ya Mwakyembe (kurasa 574) na viambatanisho vyake (kurasa 382) - hongera sana. Je baada ya kuisoma ni kitu gani kipya unakipata ndani ya ripoti hiyo ambacho wadau mbali mbali hawakukijua kwamba Richmond, Tanzania, kampuni hewa iliingia mkataba wa mamilioni na serikali ya Jamhuri ya Tanzania. Kumbuka lengo lilikuwa "to leave no stone unturned in getting to the bottom of the saga and to unearth the faces behind Richmond, Tanzania and Dowans".


  Hongera kwa utafiti wako - sasa baada ya kuongea na wajumbe wa kamati ya Mwakyembe, je wote walikubaliana na kila kitu ndani ya ripoti ? Na kama wapo ambao hawakukubaliana na ripoti yote wanatoa sababu zipi ?


  Hivi lengo la kuunda kamati ilikuwa ni jitihada za Bunge kuilinda serikali dhidi ya fedheha ? Ninavoelewa jukumu moja la bunge ni kuisimamia serikali na kuiwajibisha ikiwa ni pamoja kumpigia Raisi kura ya kutokua na imani naye ikitokea akaboronga.


  Hili sasa ni changa la macho. Kamati ilipewa uwezo, muda na nyenzo ikiwa ni pamoja na mamilioni ya pesa ya wananchi kufanya kazi waliyotumwa na kuwasilisha ripoti bungeni. Ninavyojua mimi Lowassa, Karamagi na Msabaha hawakujiuzulu kwa sababu ya ripoti hiyo, walifanya hivyo kuinusuru serikali na kwa hiari yao.


  Haya ni mazingaombwe - eti mazingira ya suala lenyewe yaliwanyima fursa ya kutoa ushahidi wote ! Ushahidi wa msingi wa Mwakyembe na kamati yake ni upi kwa sababu hadi leo sio tu mmiliki wa Richmond hajulikani bali mmiliki wa mrithi wake Dowans bado ni utata mtupu. Je kuwaanika hawa kungeifedhehesha vipi serikali ?


  Listi ya waliomtembelea Bw. Gire Texas ni kubwa, je hii inawatia hatiani ? Naomba uende taratibu na hiyo Masters Dissertation - inaonekana ni simulizi zaidi kuliko utafiti.

  Kazi walioifanya wabunge hao watano iligubikwa na usanii ila kwa leo sina mengi, Mhe. Mwakyembe kaomba tusubiri tarehe 6/2/2009 ila kitu kimoja ki wazi - mapendekezo ya kamati ya kuwajibishwa kwa wahusika katika ngazi mbali mbali yameonekana kupuuzwa. Hasara iliyopata taifa kwa kukosekana kwa umeme, pesa iliyolipwa mapema na iliyoendelea kulipwa kwa kampuni hewa, pesa iliyotumiwa na kamati ya Mwakyembe na hatua mbazo zimechukuliwa baada ya hapo - nabaki najiuliza was it worth it. Tusubiri.
   
 15. I

  Ijabu Issa Member

  #15
  Feb 1, 2009
  Joined: Apr 29, 2008
  Messages: 56
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu Mag3, heshima zako!
  Mchango wako una tatizo moja kubwa: hujaisoma taarifa ya kamati ya Dk. Mwakyembe! You are, therefore, arguing from an ill-informed position na huu ni ugonjwa mkubwa Bongoland! Mkuu, naomba nikuulize: unapata wapi audacity ya kutoa shutuma nzito nzito wakati hujaisoma taarifa husika? Nakuhakikishia kuwa kama utaisoma taarifa hiyo, 99% ya maswali uliyouliza, utayajibu mwenyewe!

  Nikupe mfano mdogo tu. Unaanza kwa kusema "Richmond, Tanzania, iliingia mkataba na Serikali..." Ukiisoma taarifa ya Kamati Teule utagundua kuwa kuna kampuni mbili hapa: Richmond Development Company LLC ya Houston, Texas na Richmond Development Company (Tanzania) Ltd. ya Dar es Salaam. Iliyoingia mkataba, ni hiyo Richmond ya Texas na iliingia mkataba na TANESCO, siyo Serikali! Mkuu, isome hiyo taarifa, usitegemee summary za RAI na MAJIRA, utagundua merits za hiyo kazi ya wenzetu.

  Umeuliza kama wajumbe wote watano walikubaliana na yote yaliyoandikwa kwenye taarifa hiyo ya Kamati Teule. Jibu utaliona ukiisoma taarifa yenyewe!

  Mwisho, umenishtua Mkuu kwa statement yako kuwa "ninavyojua Lowassa, Karamagi na Msabaha hawakujiuzulu kwa sababu ya ripoti hiyo, walifanya hivyo kuinusuru Serikali na kwa hiari yao!" Hiyo ni statement nzito na ya uhakika! Usije ukawa Lowassa, Karamagi, Msabaha au mke wa mmoja wa watu hawa unayejificha nyuma ya jina hilo Mag3? Hebu tueleze mwenzetu! Umewezaje kuzijua hisia zao za ndani? Ulikuwa nao wakati wanafanya maamuzi hayo?

  Mag3, mimi kama mtafiti nina dataz za kutosha kuthibitisha kuwa Lowassa, Karamagi na Msabaha walijiuzulu kutokana na kazi ya kina ya Kamati Teule. Wasingefanya hivyo, Kamati Teule ilikuwa tayari imejiandaa kumwondoa Lowassa kwa azimio la kura ya kutokuwa na imani naye chini ya Ibara ya 53A ya Katiba. Sikutaka niliseme hili hapa maana ni moja ya sehemu nyeti ya utafiti wangu.

  Kwa hiyo Mag3 kazi yangu siyo "simulizi zaidi kuliko utafiti" kama unavyodai. Una tatizo la msingi la kurukia mambo bila utafiti wala ushahidi. Hivi, umeisoma kazi yangu au umeiona? Ndiyo maana nakushangaa unaposema kazi ya Kamati Teule iligubikwa na usanii ... usanii unao wewe Mkuu ambaye unatoa shutuma nzito kwa wengine kuhusu kazi ambayo hujaisoma!
  Ijabu
   
 16. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #16
  Feb 1, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Mkuu Fataki, naomba kuongezea one thing, ni kwamba hata ile kusoma ripoti kama alivyofanya Mwakyembe bungeni, ninasikia haikuwa sawa kisheria kwa hiyo sio tu kwamba hakusema mengi ila isingewezekana kusoma ripoti yote, hata ile kusoima kwa saa moja na nusu ilikuwa ni ukiukwaji wa sheria kama nilivyoambiwa na baadhi wa wabunge.
   
 17. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #17
  Feb 1, 2009
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0

  Acha kutuuzia chai!

  Nimeisoma ripoti yote na viambatanisho vyake.

  Mwakyembe na kamati yake wameshindwa kuweka bayana kwamba Richmond ni kampuni ya Rostam Aziz na Lowassa zaidi ya kuzunguka zunguka kuhusu maneno ya Kazaura ndani ya kiapo na nje ya kiapo. Baada ya kupata hiyo clue kubwa kiasi hicho kamati ya Mwakyembe ilipaswa ku-pursue hilo suala further.

  Huu ukweli waliujua na kuamua kumezea, sasa kama kamati ingefunua hilo wazi, Lowassa angejiuzulu kwa aibu na sasa hiyo kesi huko mahakamani zaidi ya Gire wangekuwepo wakina Rostam na Lowassa.

  Kamati ya Mwakyembe imekwepa kuweka bayana Bilioni zaidi ya 20 zilizokwishabebwa na Richmond.

  Labda unachopaswa kutueleza kama mtafiti ni kwanini ripoti ilikuwa vile ilivyokuwa kwenye mfumo wa fumbo mfumbie mjinga!

  Asha
   
 18. F

  Fataki Senior Member

  #18
  Feb 2, 2009
  Joined: Aug 28, 2008
  Messages: 151
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Bi Asha, nimewasoma kwa makini sana akina Mag3, Ijabu Issa, Field Marshall etc kuhusu suala la Richmond. Mwelekeo wa hoja zao unaonekana. Wewe mwenzetu mbona papara? Unadai umeisoma taarifa nzima ya Kamati Teule, mbona huoneshi uelewa mpana wa suala lenyewe? Ulikuwa unaisoma huku ukisukwa nywele nini? Maana kwa wengine ndo muda wa kusinzia!
   
 19. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #19
  Feb 2, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Umeanza vibaya na unaonyesha ulivyo typical mtanzania ninayemfahamu alivyo. Kwanza unaassume mimi sijaisoma ripoti na hivyo eti I am arguing from an ill- informed person, je hiyo jeuri ya kusema hivyo unaitoa wapi ? Pili wewe mwenyewe unapata wapi audacity ya kunihukumu mimi kwa kutoa shutuma bila kusoma taarifa husika ? Nimeisoma na maswali yangu sikuweza kupata majibu yake hata kwa asilimia kumi !! - sasa hapo.

  Kwa makusudi kabisa nilisema Richmond bila qualification yoyote na kwa hiyo hapo umechemsha. Richmond iliingia mkataba na Tanesco kwa baraka na usimamizi wa serikali ya Tanzania na ni serikali hiyo hiyo iliyosisitiza na kuhakikisha mkataba unasainiwa. Hayo mengine ni blah blah.

  Kama huna jibu si ni heri kukaa kimya ? Wewe ama kwa makusudi umeandaliwa kuandika unachoita dissertation kuweka kiwingu kwenye utata ulioigubika Richmond - ningekuwa wewe ningejiuliza mengi kabla ya kuchangamkia hiyo tenda.

  Je unakumbuka siku mkuu wa kaya alipoongea na wazee wa Dar es Salaam ? Unakumbuka alivyomwaga machozi kwa kipenzi chake kujiuzulu na kuelezea hicho kitendo kama cha kishujaa ? Kwa taarifa yako mimi ni moja wa watanzania wanaopata uchungu na hasira isiyo mfano nikiwaona wahujumu uchumi wakiendelea kupeta miongoni mwetu - Lowassa, Karamagi na Msabaha wakiwa miongoni mwao. Unakumbuka Spika wa Bunge alivyomsubiri Lowassa arejee bungeni aweze kumwingiza kwenye kamati fulani ya bunge ?

  Na mimi nakuhakikishia kama Lowassa angegoma kujiuzulu tungekuwa na bonge la kasheshe na wengi tu wangeumia na hiyo kamati ungeshuhudia ambavyo usanii wake ungeanikwa wazi na kamati kubaki uchi. Unaosema wangetumia ibara ya 53A ya katiba ni nani hao -Je, unaowasema ni hao wanaofoka mpaka mapovu yanawatoka lakini ikifika kupiga kura haooo !! Unanichekesha ndugu yangu. Wadanganyika wamezoea kuzugwa lakini taratibu wachache wanaamka na hawatakubali tena sera hiyo.

  Sikushangai wala sikulaumu kwa kutouona huo usanii kwenye ripoti maanake umepata mwanya wa kulipua - ndio wasomi wetu wengi walivyo. Angalia wanavyotetea vitendo vya ajabu ajabu kama unavyojaribu kufanya - well, ndivyo tulivyo. Keep your fingers crossed and watch this space - you are about to get rudely awakened. Anayekurupuka na kurukia mambo bila utafiti na kufuata tu simulizi hataweza tena kujificha nyuma ya dissertation. Good luck !!
   
 20. F

  Fataki Senior Member

  #20
  Feb 4, 2009
  Joined: Aug 28, 2008
  Messages: 151
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  mkuu mag3, ulikuwa una hoja nzuri lakini jazba, overconfidence, arrogance, ubabe wa kishoga unaouonyesha kwenye mkeka ulioutandika hapa bila kuombwa kwa nia tu ya "kujisafisha" au kujibu kila kitu ili tu wewe uonekane huna dosari, vimekufanya wengine tushindwe kuona tofauti kati yako na huyo bwana wa dissertation ambaye anaamini kuwa ni yeye peke yake anayelielewa suala hili. Punguza jazba mkuu, unaharibu track record yako.
   
Loading...