Je, ripoti ya Mwakyembe kuhusu Richmond ilificha nini?

Je, ripoti ya Mwakyembe kuhusu Richmond ilificha nini?

Watanzania sijui ni wasahaulifu au vipi? Hussein Bashe alitueleza kuwa ameiona ripoti halisi ya richmond na ile aliyosoma Mwakyembe pale mjengoni Dodoma ni ya kughushi tu. Je Bashe alikuwa anatafuta ukuu wa wilaya? (kama ilivyo desturi ya CCM, kada "msumbufu" hupewa "zawadi" ya ukuu wa wilaya). Au kweli Bashe anayo? Basi tumuulize kaiona wapi?, imeandikwa na nani? Au naye anatumwa "kusafisha njia?"
 
Kama ile ingekuwa feki ingekuwa imekanushwa na muhusika mkuu na kutomsababishia mkewe kutoa machozi mbele ya watu.
 
unaitaka na nani? by the way we ni nani? jadili mambo ya msingi.
 
Huku kukiwa na uvumi kuwa huenda Dr Harrison Mwakyembe anateswa na mzimu wa ripoti ya Richmond kwa kile kinachodaiwa alificha baadhi ya madudu ili kumlinda rais na serikali ya CCM naam! tuhuma hizi si za kupuuzwa hata kidogo tena zinapewa nguvu zaidi kwa maana zipo zile zinazotoka ndani ya CCM.

Kwa wachambuzi na wafatiliaji wa siasa za ndani ya CCM watakuwa wameshaona maandishi ukutani na bilashaka wanatambua hii ya sasa ya Dowans ni ushahidi kuwa mzimu wa Richmond ungalipo na zaidi watakuwa wanafahamu kuwa ripoti halisi ya Richmond ipo njiani inakuja, iwe kwa kusemwa na mtu, iwe kwa kujitetea mtu au iwe kwa kutangazwa rasmi, au kupitia bunge lakini yatosha kusema ipo njiani ile inakuja.

Na hapa ndipo kunakolala chimbuko la haya makundi ndani ya CCM, nasema ole wake ripoti hiyo itakapotoka, ole wao wahusika wote wa sakata hilo, maana ndiyo tutajua mbivu na mbichi na hii yaweza kuwa ni bakora ya kuchapana wao kwa wao ndani ya CCM , lakini ikiwa huu ndiyo mtiririko wa mantiki kwanini tusiamini kuwa Ripoti halisi ya Richmond ndiyo itaamua mgombea urais kwa tiketi ya CCM 2015?
 
Ripoti iamue vipi wakati ASHAROSE MIGIRO hakuwa hapa nchini?.Hivi ndan ya CCM mbona wapo wengi wanaweza URAIS hata mama TIBAIJUKA naye hakuwepo.Kati ya hao tuchague mmoja awe Rais wetu ila awe CCM sio vuvyama vwingine vyenye mahabusu.
 
Kanawe uso kwanza ndipo uingie humu jamvini. sh.w.ine.
 
Hii thread niliianzisha tarehe 29 January mwaka 2009 nikimtuhumu Raisi Jakaya Mrisho Kikwete kama mhusika mkuu katika sakata la Richmond na kuiponda ripoti ya Mwakyembe kama mbinu ya kuficha ukweli kwa lengo la kuisetiri serikali ya CCM. Alitokea mchangiaji moja msomi kwa jina Ijabu Issa aliyedai anafanya utafiti ili imsaidie kuandika paper "dissertation" kuhusu hiyo ripoti.

Nadhani sasa muda mwafaka umefika kwa Mkuu huyo Ijabu Issa kujitokeza tena na kutupa angalau kidogo kuhusu matokeo ya utafiti aloufanya kwani muda mrefu umepita na bila shaka hiyo paper yake tayari itakuwa imekamilika. Kulingana na mambo yanavyozidi kuifumka, ripoti inaweza kusaidia kutupa mwanga kuhusiana na usiri uliyoigubika hiyo ripoti ya kamati teule ya Bunge.
 
uTEKELEZAJI WA MAPENDEKEZO YA TUME ULIISHIA WAPI?
 
Mwakyembe hapa naye sijui kama kashtuka alitumika tu kutimiza azma za watu wengine. Kwa maana nyingine naye alitumika kama bangusilo tu. Time will tell.
 
yakitekelezwa mapendekezo ya report ya Richmond navua nguo hadharani
 
Hii thread niliianzisha tarehe 29 January mwaka 2009 nikimtuhumu Raisi Jakaya Mrisho Kikwete kama mhusika mkuu katika sakata la Richmond na kuiponda ripoti ya Mwakyembe kama mbinu ya kuficha ukweli kwa lengo la kuisetiri serikali ya CCM. Alitokea mchangiaji moja msomi kwa jina Ijabu Issa aliyedai anafanya utafiti ili imsaidie kuandika paper "dissertation" kuhusu hiyo ripoti.

Nadhani sasa muda mwafaka umefika kwa Mkuu huyo Ijabu Issa kujitokeza tena na kutupa angalau kidogo kuhusu matokeo ya utafiti aloufanya kwani muda mrefu umepita na bila shaka hiyo paper yake tayari itakuwa imekamilika. Kulingana na mambo yanavyozidi kuifumka, ripoti inaweza kusaidia kutupa mwanga kuhusiana na usiri uliyoigubika hiyo ripoti ya kamati teule ya Bunge.

Kaazi kweli kweli.
 
Duh, watu mnajua kupekua!
 
Huyu ndugu ni mwalimu wa sheria anayetumikia tumbo katika mambo ya kitaifa.

Bunge liliwatuma kufanya uchunguzi,leo unasema uliacha sehemu ya ripot hiyo,ilikuwa kwa manufaa ya nani? huu ni unafiki kufanywa na mtu kama wewe.

Ni vema pia ungejibu shutuma zinazokuja kwako za juzi tu badala ya kuleta story za upumbafu wako ktk kisoma ripoti.

Mmekuwa serikali isiyojali haki na utaratibu wa sheria. Kama unatambua ilikuwa jinai,kweli mtu hapaswi kufikishwa mahakamani kama akikaa kimya tu. Umetia aibu taaluma ya sheria.
 
Kwanini mwakyembe alihamishwa kutoka kwenye wizara ya usafir??
 
Mwakyembe atueleze yale yaliyofichwa kwenye ile ripoti ili serikali isianguke asituletee porojo
 
Mwakyembe mnafki sana ndio maana kyela hatumtaki tena.
 
sasa kama mlificha baadhi ya mambo ili kuinusuru serikali ndo kusema ccm haistahili kuongoza nchi? mimi bado sijamuelewa mwakyembe
 
Mwenyezi Mungu amemuumba binadamu kama kiumbe bora kabisa dunia na kutenganisha kati ya Mwanaume na Mwanamke, na katika imani zilizonyingi zinatambua uhalisia huo.

Sasa basi ukiona jinsia moja inakuwa na kigeugeu katika jambo fulani mpaka kujitoa ufahamu wa kutokuwa sasa na jinsia yake halisi basi hapa si Mwenyezi Mungu ndiyo kakosea kumuumba binadamu huyu bali tu ni binadamu mwenyewe kutaka kupambana na tamaa za maisha yake ya kidunia, na adhabu kuwa utakuwa juu yake kama si duniani hapahapa basi itakuwa huko ahera ama kotekote.

Sakata la Richmond, hii ni moja kati ya Kashfa nyingi katika kumbukumbu ya Taifa letu na itaendelea kuwaandama Chama Tawala katika kipindi chote cha utawala wao mpaka pale wale wote wahusika wawekwe wazi na si kupiga kelele tu Mtaani kama Daktari wa sheria anavyopiga kelele popote pale asimamapo baada ya kuona kivuli cha mtu furani.

Mimi ninamuomba huyu Daktari wa sheria atoe yote hadharani, je ilikuwaje, nani alihusika, nani alikula pesa, kiasi gani nakadhalika. Ni aibu sana kama kweli mtu furani anasemwa alihusika lakini mpaka sana bado hajafikiswa mahakamani. Hii inamaanisha kwamba vile wanavyoubiri kwenye majukwaa si ya kweli kabisa.

Daktari wa Sheria kama kweli huyu mtu unaamini ni mtuhumiwa wa kashfa hii basi wewe kama mtalaamu wa sheria basi pigania juu chini kabla hata ya uchaguzi kuisha ufikishe mahakamani huyu Mtuhumiwa, KINYUME na hapo basi tulio wengi tunashaangaa na ulijari wako.
 
Back
Top Bottom