Je, Programu ya Elimu Bure imefutwa na Serikali kimyakimya?

Habar za muda huu ndugu wanajamii

Sote tunafahamu ya kwamba Kuna chama kilijinadi kuwa kitatoa elimu Bure kuanzia elimu ya Msingi Hadi Sekondari kwenye campeni za uchaguzi wa mwaka 2015 na 2020.

Baada ya hapo Kuna fedha zilianza kutolewa kwenye Shule za Msingi na na Sekondari kwa kuzingatia wingi/idadi ya wanafunzi kwenye kila Shule.Fedha hizi zilizingatia vipengele muhimu vitano kwenye matumizi ambavyo ni;

I. Utawala (10%)
II. Vifaa vya kufundishia na kujifunzia (30%)
III. Mitihani (20%)
IV. Ukarabati (30%)
V. Michezo (10%)

Fedha hizi japo zilikuwa zinatoka kila mwezi lkn,hazikuweza kukidhi mahitaji kwa kila kituo kutokana na uhitaji mkubwa kwenye kila kifungu mfano,fedha za michezo zilipaswa kununua vifaa vya michezo pamoja na kuendeshea mashindano ya Umtashumta;

Kwa kifupi ni kwamba kila kifungu hakikuweza kujitosheleza...kituo X mwaka huu (2023) kiliapswa kuendeshea mashindano ya Umtashumta kwa kutumia Shilingi 1,520,000/= (Million Moja laki Tano na Ishirini Elfu) lkn,fedha iliyokuwepo kwenye kifungu Cha michezo ni chino ya laki Tisa za Kitanzania kwa mwaka mzima.

Lengo la kuandika Uzi huu ni kutaka kuwafahamisha michache viongozi wa vyama na Serikali pamoja na Watanzania wote wanaosoma Jamii Forum.Fedha hizi za elimu bure hazijatolewa na Serikali kwa zaidi ya miezi miwili Sasa ambazo ni fedha za mwezi Octoba na Novemba hali hii imepelekea Walimu Wakuu na Wakuu wa shule kuingia kwenye madeni kwa sababu Walimu wamelazimika kuendesha shughuli zote za shule ikiwemo Mitihani ya mwisho wa mwaka kwa kutumia mishahara Yao pamoja na kukopa kwa watu mitaani.

Wito wangu kwa Serikali,kama mmeshindwa kugharamia elimu kwa utaratibu wenu wa elimu bure toeni taarifa kwa umma wa Watanzania;kuwabebesha Walimu madeni siyo jambo zuri hata kidogo pia,mnawasababishia Walimu msongo wa mawazo kwa kuwabebesha majukumu yasiyo wahusu

Pamoja na yote hayo viongozi mjifunze kuwaheshimu walimu hata kama wapo chini yenu kutokana na umasikini wao.Siku chache zilizopita palikuwepo na zoezi la unyweshaji wa dawa za kichocho kwa wanafunzi (Prazquantel na Albendazole) kwenye kila shule mwalimu wa afya na mwalimu Mkuu walihudhuria seminar ya mafunzo ya namna ya kugawa dawa lakini, hakuna hata mmoja aliyelipwa fedha za seminar hadi hivi Sasa na hata fedha za unyweshaji dawa za minyoo na kichocho na zenyewe bado hazijatoka mpaka hivi Sasa.

Pia, kuna seminar ya mafunzo ya ESS, PEPMIS na PIPMIS ambalo limeanza kufanyika kwenye Wilaya ninayofanyia kazi tangu muda kidogo lakini, hakuna mwlm hata mmoja ambaye amelipwa hata mia ya nauli zaidi ya kununuliwa chakula mbaya zaidi kuna Walimu wanatoka interior/remoteness areas hakuna mtu anayejali wamesafiri vipi kutoka huko kwenye vituo vyao na watarudi vipi tena kwenye vituo vyao.

Enyi Serikali mbona mmeufanya ualimu kuwa ni kazi ya watu wenye laana na waliokosa jambo la kufanya?
Erythrocyte tunahitaji elimu bora ya vuwango yenye unafuu kwa shule za umma.

CCM wameshindwa kusimamia ahadi zao. Na hawaaminiki kila wanachokisema maana walisema elimu bure ikatolewa elimu mbovu na isiyomuandaa mtoto kukabili na kubadili mazingira ya maisha yake
 
Hakuna kitu kama hicho, Elimu bure! Ukiona unapewa bure, ujue gharama imebebwa na mwingine, Ukilipiwa, chakula hotelini, sio, kwamba huo msosi ni bure, gharama hujabeba wewe,imebebwa na mwingine, Serikali ikisema elimu bure, hapo ujue, inabidi ibebe gharama kwa kutoza Kodi zaidi ili kufidia Hilo hitaji,
 
Kwani hyo mitihani isipofanyika kwa sababu za msingi kama hyo ya kukosa pesa huyo mwalimu mkuu na mkuu wa shule ataathiriwa vipi?
Atakuwa anaupenda ukuu wake kweli? Mabosi wake watambinua kama lifanyavyo gari la mchanga
 
Natamani hii posho ya madaraka Kwa wakuu wa shule ife kabisa Mungu saidia ipotee isiwepo
Kwanini ndugu, majukumu ya walimu wakuu ni mengi sana, Wana kazi ya kusimamia walimu na wanafunzi lakini pia suala lolote linalohusu shule wanawajibika nalo, mkuu wa shule anatakiwa kuwa na bando masaa 24, kipindi wewe umesinzia kwako yeye huwa anawajibika na wakati mwingine kufanya kazi zako.
Una mawazo ya kimasikini na roho mbaya

Wewe ni masikini nambari wani na unadaiwa mikopo kila kona.
 
Wakuu wa shule hawana kazi yoyote, kwanza wengi ni wavivu hata kufundisha hawataki, wanazurura tuu na vikao vyao uchwara na kujiandikia posho
 
Habar za muda huu ndugu wanajamii

Sote tunafahamu ya kwamba Kuna chama kilijinadi kuwa kitatoa elimu Bure kuanzia elimu ya Msingi Hadi Sekondari kwenye campeni za uchaguzi wa mwaka 2015 na 2020.

Baada ya hapo Kuna fedha zilianza kutolewa kwenye Shule za Msingi na na Sekondari kwa kuzingatia wingi/idadi ya wanafunzi kwenye kila Shule.Fedha hizi zilizingatia vipengele muhimu vitano kwenye matumizi ambavyo ni;

I. Utawala (10%)
II. Vifaa vya kufundishia na kujifunzia (30%)
III. Mitihani (20%)
IV. Ukarabati (30%)
V. Michezo (10%)

Fedha hizi japo zilikuwa zinatoka kila mwezi lkn,hazikuweza kukidhi mahitaji kwa kila kituo kutokana na uhitaji mkubwa kwenye kila kifungu mfano,fedha za michezo zilipaswa kununua vifaa vya michezo pamoja na kuendeshea mashindano ya Umtashumta;

Kwa kifupi ni kwamba kila kifungu hakikuweza kujitosheleza...kituo X mwaka huu (2023) kiliapswa kuendeshea mashindano ya Umtashumta kwa kutumia Shilingi 1,520,000/= (Million Moja laki Tano na Ishirini Elfu) lkn,fedha iliyokuwepo kwenye kifungu Cha michezo ni chino ya laki Tisa za Kitanzania kwa mwaka mzima.

Lengo la kuandika Uzi huu ni kutaka kuwafahamisha michache viongozi wa vyama na Serikali pamoja na Watanzania wote wanaosoma Jamii Forum.Fedha hizi za elimu bure hazijatolewa na Serikali kwa zaidi ya miezi miwili Sasa ambazo ni fedha za mwezi Octoba na Novemba hali hii imepelekea Walimu Wakuu na Wakuu wa shule kuingia kwenye madeni kwa sababu Walimu wamelazimika kuendesha shughuli zote za shule ikiwemo Mitihani ya mwisho wa mwaka kwa kutumia mishahara Yao pamoja na kukopa kwa watu mitaani.

Wito wangu kwa Serikali,kama mmeshindwa kugharamia elimu kwa utaratibu wenu wa elimu bure toeni taarifa kwa umma wa Watanzania;kuwabebesha Walimu madeni siyo jambo zuri hata kidogo pia,mnawasababishia Walimu msongo wa mawazo kwa kuwabebesha majukumu yasiyo wahusu

Pamoja na yote hayo viongozi mjifunze kuwaheshimu walimu hata kama wapo chini yenu kutokana na umasikini wao.Siku chache zilizopita palikuwepo na zoezi la unyweshaji wa dawa za kichocho kwa wanafunzi (Prazquantel na Albendazole) kwenye kila shule mwalimu wa afya na mwalimu Mkuu walihudhuria seminar ya mafunzo ya namna ya kugawa dawa lakini, hakuna hata mmoja aliyelipwa fedha za seminar hadi hivi Sasa na hata fedha za unyweshaji dawa za minyoo na kichocho na zenyewe bado hazijatoka mpaka hivi Sasa.

Pia, kuna seminar ya mafunzo ya ESS, PEPMIS na PIPMIS ambalo limeanza kufanyika kwenye Wilaya ninayofanyia kazi tangu muda kidogo lakini, hakuna mwlm hata mmoja ambaye amelipwa hata mia ya nauli zaidi ya kununuliwa chakula mbaya zaidi kuna Walimu wanatoka interior/remoteness areas hakuna mtu anayejali wamesafiri vipi kutoka huko kwenye vituo vyao na watarudi vipi tena kwenye vituo vyao.

Enyi Serikali mbona mmeufanya ualimu kuwa ni kazi ya watu wenye laana na waliokosa jambo la kufanya?
Kuwa mpole, serikali iko Dubai kwenye mkutano wa mazingira hakuna mtu wa kuidhinisha cheque ofisini
 
Back
Top Bottom