Je Polisi ndio wavurugaji wa amani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je Polisi ndio wavurugaji wa amani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gurtu, Jan 13, 2011.

 1. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #1
  Jan 13, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Jana (12/01/2011) yamefanyika mazishi ya wahanga wa mauaji yalilyofanywa na polisi bila ulinzi wa polisi na hapakuwa na uvunjifu wa amani. Kama wananchi waliweza kufanya shughuli zao bila ushiriki wowote wa polisi na bila uvunjifu wa amani wakati siku chache tu polisi hao waliwaingilia wananchi na kutokea uvunjifu wa amani tafsiri yake ni kuwa polisi ndiyo chanzo cha uvunjifu wa amani.

  Mara nyingi watu wamekuwa wakilalamika kuwa maeneo mengi polisi wamekuwa wakituhumiwa kushirikiana na majambazi kufanya ujambazi. Hili linaweza kuwa kweli kwa sababu kitendo kilichofanyika Arusha tarehe 05/01/2011 kinaonyehsa wazi kuwa watu waliopoteza maisha wengi walikuwa katika shughuli zao za kawaida. Hivyo haiwezi kuingia akilini kwamba watu waliopo sokoni - Kilombero wanaandamana.

  Baada ya kufanya majukumu yao ya kuvuruga amani viongozi wa serikali wakaanza kusikitikia yaliyofanyika Arusha. Jk akiwa ndiye kiongozi mkuu wa serikali alisikika akisema kuwa anasikitika kwa yaliyotokea Arusha na kwamba yalitokea kwa bahati mbaya. Waziri wa Mambo ya nje naye anasema kwamba polisi wametumia nguvu ya ziada. Matamshi hayo yanapotolewa na viongozi wa juu wa serikali yana maana gani?

  Kama ni kwa bahati mbaya ina maana vyombo vyetu vya usalama vinafanya kazi kwa bahati mbaya na/au kwa ubabaishaji. Kwa hiyo tusije kushangaa viongozi wetu siku moja wakashambulia nchi ya jirani kwa sababu inahatarisha usalama wetu lakini baadaye eti kiongozi mkuu wa nchi aseme yaliyotokea ni bahati mbaya.

  Haitoshi kutumia taarifa za kiintelijensia zinasema nini bila kuzichambua. kwani ukiambiwa kuwa fulani anataka kukushambulia wewe utakachofanya ni kutangulia kumpiga yeye bila kujua kama ni kweli au la? au unazifanyia kazi taarifa za shambulio dhidi yako kwa kujiandaa kujilinda. wewe unapoanzisha shambulio kwa sababu tu ya taarifa za kiintelijensia utathibitishaje kuwa zilikuwa taarifa za kweli wakati uliyemshambulia hakuwa na silaha?

  Jeshi la polisi linatakiwa lijirekebishe ili lilete sura yake inayotakiwa kuwa nayo. Hatuihitaji jeshi la polisi lenye taarifa za kiintelijinsia kuhusu uvunjifu wa amani katika suala la maandamano wakati ujambazi unafanyika na huku wananchi wanawajua majambazi kwa majina lakini wao wanashindwa kuwakamata. Hatuhitaji jeshi linatoutmia silaha dhidi ya raia wasio na silaha lakini wanapokutana na majambazi wenye silaha wao hurudisha za kwao.
   
 2. coscated

  coscated JF-Expert Member

  #2
  Jan 13, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 1,500
  Likes Received: 250
  Trophy Points: 180
  polisi ya kibongo ndio chanzo cha kuleta vurugu siku zote.
   
 3. M

  Msharika JF-Expert Member

  #3
  Jan 13, 2011
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Well said
   
 4. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #4
  Jan 13, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,933
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  hawa jamaa yaani ni crap sikuzote..kuanzia kwenye road blocks.., barriers ..., vituo vya polisi.., mahakamani.., mabenki..., uraiani..,... ma defender.... hata majumbani kwao... wanajihisi wapo juu na wananguvu kuliko
   
 5. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #5
  Jan 13, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ni wazi kuwa Dunia sasa imewasuta kina Makamba, Kina Said Mwema,Kina Andengenye na wengineo! Kila mmoja wetu ameona jinsi watu walivyojitokeza kwa wingi kuwaaga marehemu yamkini kuliko hata ile siku ya maandamano lakini bado watu hao hao wamefanya maandamano kwa heshima na taadhima bila uvunjifu wowote wa amani Hii inatupa kuamini kuwa POLISI ndio walikuwa chanzo cha vurugu. Inasikitisha sana kuona viongozi mbalimbali wakuu wakitoa ujumbe na kuzungumzia tukio halisi eti kuwa lilikuwa la bahati mbaya! Haiji akilini kabisa. Bahati mbaya wakati kamanda alishatuambia kuwa kulikuwa na habari za kiitilejinsia kuhusu vurugu! Haiingii akilini kabisa tena kabisa.
  Kama ni kwa bahati mbaya inamaanisha hakuna umuhimu wa kuviamini tena vyombo vyetu vya dola. Inamaanisha kuwa vyombo vyetu vya usalama vinabahatisha katika utendaji wao wa kazi au vinafanya kazi kwa ubabaishaji!!!.
   
Loading...