Je, Polisi mkoani Mara, wanamuonea Kijana huyu?

Je, Polisi mkoani Mara, wanamuonea Kijana huyu?

Cosovo

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2018
Posts
667
Reaction score
1,822
Ni kijana mkoani Mara ambaye anashikiliwa na jeshi la polis baada ya kutokea mauaji ya aliyekuwa mke wake

Iko hivi,Kijana baada ya kushindana kuishi na mke wake ,walifikisha suala hilo kwa mtendaji wa kijiji ambapo mwanamke aliapa kuwa hataweza kamwe kuishi na huyo mume wake ni bora akaishi mwenyewe

Baada ya hapo Kijana aliendelea na maisha yake huku mwanamke akichukuliwa na Kijana mwingine kama hawara

Kijana aliyemchukua huyo mwanamke alimpeleka mjini kumpangishia na baada ya siku kadhaa Kijana akiwa anarudi kwa mpenzi wake huyo baada ya shughuliza za mchana alikutana na mwanaume mwingine ndani na huyu Kijana alikasirika na kuanza ugomvi uliopelekea mwanamke kupoteza maisha baada ya kunigwa shingo

Hata hivyo Kijana huyo alikimbia,kesi ikaja mwanamke azikwe wapi

Nyumbani kwa mwanamke wanadai binti yao alikuwa alishaolewa na hivyo azikwe alikokuwa ameolewa na mila za kabila hilo haziruhusu mwanamke aliyekwisha olewa azikwe kwao na huku ndugu wa mwanaume wa kwanza wanakataa kuwa huyo mwanamke alikuwa alisha achika hivyo hawezi kuzikwa nyumbani hapo,

Mvutano huo ulipelekea aliyekuwa mume ashikiliwe na polisi wakimshinikiza akubali mwili wa marehemu uzikwe kwake kwa hoja kuwa alikuwa mke wake hapo nyuma ,

Mwili wa marehemu upo mochwari kwa siku 5,hakuna mwafaka unaopatikana wapi azikwe marehemu

NB: Nawashauri wanawake ukiolewa tulia,mnaenda kujitafutia vifo wenyewe,badala ya kutulia na waume zenu,mnawapa taabu watu mwili wa marehemu uzikwe wapi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nawajua watu wa Mara, hii ngoma msiichukulie simple,
Wanaamini kuwa kumzika marehemu aliyeolewa kwenye makaburi yao ni machukizo kwa mizimu ya mababu, hivyo kukubali kitendo hicho kufanyika kunaweza kusababisha ukoo kuandamwa na mabalaa,,

Pia kwa upande wa aliyekuwa mume wake nako pia ni tatizo zaidi kwani tayari hakuwa mke wao na ndoa ilivunjika automatically baada ya kiongozi wa selikari ya kijiji kushindwa kuisaidia, hivyo kumzika marehemu ambaye amefia kwenye ugoni ni mkosi na mizimu haitakaa iwaache salama,,

Tabu iko,, wanawake wa kileo acheni viburi na ujuaji ulipitiliza..
 
Kweli kabisa.
Kwa Mara hii ngoma bado mbichi kabisa. Yaani hapo lazima Wazee wa ukoo pande mbili wakae wakubaliane. Kama atazikwa kwa Mume wa zamani mila zitafanyika halafu ruksa itolewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hapo ziandaliwe kuni mwili uchomwe moto, atakae lalama kuwa mwili usichomwe moto akabidhiwe mwili akauzike, sidhani Kama mama yake au kaka zk watakubali mwili wa ndugu yao utiwe moto, ila nasisi wanawake jamani
Ushauri mzuri lakini sio rahisi kutekelezeka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom