Je, Papa ndiye mrithi wa mtakatifu Petro?

Je, Papa ndiye mrithi wa mtakatifu Petro?

Kwenye biblia hakona hesabu za Calculus ama Genetics kiasi chakuwatisha watu kwamba ili waisome ni lazima wawe na Phd..
Unachekesha sana...Paulo mwenyewe alikuwa mwanafunzi wa Gamalieli.....Na alijifunza kweli kweli neno la Mungu

Endelea kushangaa feri shilingi ikizama angali meli inaelea
 
elimu ni gharama kwa nchi za kiafrica sasa m2 kulipata neno la Mungu mpaka awe na Phd huko
Yani wewe ndio kenge maji kweli..naongea hivi unajibu unavyoona wewe..

Yani nakufundisha Baoloji mtihani unanipa majibu ya history...

"Nimesema Biblia watu wanajifunza mpaka wanapata Phd na Uprofesa".....sijui unanielewa...???

Au umekunywa gongo..?
 
Nimesoma biblia nzima sijaona mahali YESU au Petro kaanzisha kanisa kaliita jina CATHOLIC
pole sana
hayo ndo matokeo ya kuvamiavamia mambo usiyoyajua na kuvamiavamia lugha za watu......

unashangaa kulikosa neno "catholic" kwenye biblia yako wakati hilo neno "catholic" ndilo agizo la mwisho kutolewa na yesu kwa mitume wake kabla ya yeye kupaa mbinguni. we endelea kushangaa acha waliomuelewa yesu waendelee kuchanja mbuga na neno lake.

kwa nyongeza tu ndani ya hiyo biblia yako kuna nyaraka saba za kikatoliki yaani "catholic letters" sasa natumaini ushindwe hata kushangaa.
 
Hivyo wewe inakuuma sana sio...

Kwani kutoa hitimisho kwa Yakobo ndio kuna mfanya mmoja asiwe kiongozi...hahahaha

To know the History is to cease to be a protestant .


Oh oh.ih....Wasabato kumbe sio Wakristo
Hahaha hongera kwa mchango . Unadhani kwa nini askofu wa rumi alikuwa mkuu wa maaskofu wenzake na baadae papa. Unadhani kwa nini kitendo hicho kilipingwa na maaskofu wenzake akiwemo Yule wa Syria.
Rudi kwenye books mkuu.
" The only new thing in this world is the history that you do not know".

Haya yameandikwa na wasiowasabato kwa kina wala sio kazi ya wasabato mkuu.
Wasabato wanaujumbe wa kueleza Dunia uache uovu na mafundisho yote na Hadith za kibinadamu zilizonje ya bibilia wajiandae kumpkea Yesu akirudi. Wabaikumbusha Dunia kumuamini Yesu kunakuhitaji utii na amri zake kumi ikiwemo na ya sabato ambayo Dunia imeijumapilisha.
 
Wasabato bhana.bila kulisema kanisa katoliki mnaona hamjakamilika... Ndugu zangu kanisa halimpeleki mtu mbinguni.... Dini iliyoyakweli ni hiii, kutembelea wagonjwa, kusaidia yatima na kuwajali wajane.....

Sent using Jamii Forums mobile app
Acha uongo wewe ikiwa kanisa linakwambia kuwa shoga ni baraka, utaenda mbinguni vipi na ulipokea na kuamini,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu yangu kuna udhaifu mkubwa sana kwenye maelezo yako.Nimeshindwa hata nikusaidieje.Kwanza tujikumbushe.

JE,UNAFAHAMU ALIYEANZISHA DHEHEBU LAKO?

Kabla ya Mwaka 1517,Kila Mkristo aliuwa Mkatoliki.

Tunafahamu leo ukristo uko hivi:

1.Kama wewe ni Mlutheri ufahamu kwamba Kanisa lako lilianzishwa na Baba Martin Luther,Ujerumani Mwaka 1517 akiwa na Daraja la Upadre Katoliki.

2.Wewe kama ni Mennonite,Fahamu kuwa Kanisa lako lilianzishwa na ndugu Grebel,Mantz na Blaurock mwaka 1525

3.Wewe kama ni Anglikana,Kanisa lako lilianzishwa na Mfalme Henry XIII Mwaka 1534.

4.Kama wewe ni Presbyterian,Kanisa lako lilianzishwa na ndugu John Knox Mwaka 1960.

5.Kama wewe ni Congregationist(Kanisa la Mtaa) Kanisa lako lilianzishwa na ndugu Robert Brown,Uholanzi Mwaka 1583.

6.Kama wewe ni Baptist(Kanisa la Ubatizo),Fahamu kuwa Kanisa lako lilianzishwa na ndugu John Smith,Amsterdam,UholanziMwaka 1606.

7.Kama wewe ni Methodist,Kanisa lako lilianzishwa na John Murray,New jersey,Marekani mwaka 1770.

8.Kama wewe ni Mormo au Malaika Wajao Kanisa lako lilianzishwa na ndugu Joseph,New York,Marekani mwaka 1829.

9.Kama wewe ni Seven Day Adventist(Sabato) fahamu kuwa kanisa lako lilianzishwa Willium Miller Mwaka 1831.

10.Kama wewe ni Jeshi la Wokovu(Salvation Army),Kanisa lako lilianzishwa na ndugu Willium Booth Mwaka 1865.

11.Kama wewe ni Mashahidi wa Yehovah(Jehovah Witness) Kanisa lako lilianzishwa na Charles Russel Mwaka 1872.

12.Kama wewe ni Redeemed Christian Church of God(Marejeo ya Kikristo ya Kanisa la Mungu) unatakiwa kufahamu Kanisa lako lilianzishwa Mwaka 1952 na Josiah Akinayomi.

13.Kama Muumini wa Deeper Lige Bible Church,Kanisa lako lilianzishwa na Pastor William Kumuyi,Lagos Nigeria Mwaka 1973.

14.Kama wewe ni Mountain of Fire(Mlima wa Moto) Kanisa lako lilianzishwa na Daniel Olokoya Mwaka 1952.

15.Kama wewe ni Muumini wa Makanisa ya Askofu Zakaria Kakobe,Mtume na Nabii Josephat Mwingira,Mchungaji Hernandes,Askofu Gwajima nk,ujue kwamba Makanisa hayo yameanzishwa Dar es Salaam miaka ya hivi karibuni.

16.Hapa unaweza kuendelea na kuendelea mpaka Makanisa 43,000 yaliyopo leo.

17.Lakini kama wewe ni Mkatoliki unafahamu kabisa Imani na Kanisa lako vilianzishwa na Yesu Kristo mwenyewe Mwaka 33 kabla ya kupaa kwenda Mbinguni soma Mathayo 16:18 na kuliacha chini ya wanafunzi wake wakiongozwa na Mtume Petro na kutokea kipindi hicho kumekuwa na ukasimishaji wa Baba Watakatifu 266 wa kwanza akiwa Mtume Petro(soma Matendo ya Mitume 2:1) mpaka Yesu atakaporudi tena kadiri ya Maandiko Matakatifu.
Nimeorodhesha historia hii si kudharau Imani yoyote ila kufundisha Historia ya Imani ya Kikristo na kuweka Kumbukumbu sawa.
Kanisa Katoliki linabaki kuwa lilelile aliloanzisha Yesu Kristo na kuliwekea Ekaristi Takatifu kama Baraka ya Mwisho.Tunaendelea kufanya alichoagiza Bwana wetu Yesu Kristo kama alivyoyatoa maneno haya Matakatifu juu ya Mkate na Divai,kuwa tuule Mwili wake na Kuinywa Damu yake na aliagiza kufanya haya kwa kumkumbuka yeye mpaka atakapokuja tena(Mathayo 26:26).
Neno Katoliki maana yake kitu kizima au chote au wote.
Eneza Upendo,Eneza Utengamano na Umoja wa Kiroho aliotuacha nao Yesu Kristo na sio Mgawanyiko.
Akawaambia bikra Maria ndiyole poster wake?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
pole sana
hayo ndo matokeo ya kuvamiavamia mambo usiyoyajua na kuvamiavamia lugha za watu......

unashangaa kulikosa neno "catholic" kwenye biblia yako wakati hilo neno "catholic" ndilo agizo la mwisho kutolewa na yesu kwa mitume wake kabla ya yeye kupaa mbinguni. we endelea kushangaa acha waliomuelewa yesu waendelee kuchanja mbuga na neno lake.

kwa nyongeza tu ndani ya hiyo biblia yako kuna nyaraka saba za kikatoliki yaani "catholic letters" sasa natumaini ushindwe hata kushangaa.
😂😂😂😂😂 kwahiyo katika hizo barua do Yesu kaagiza kuwa mama yake ndiyo secretali wake so mmwombapo yeye mpitie kwa mama yake.....duh!.....biblia nzima hakuna mahala kuna maagizo msali rozali mbusu msalaba ama mkaungame dhambi zenu kwa binadamu wenzenu kama ipo hiyo mistar iweke humu sasa hiv tunakwenda kwa ushahid wa maneno ya Yesu sio ya papa
 
hakuna mahali popote pale katika biblia Yesu kasema usipokuwa mkatoliki sikutambui
ukikosa cha kuandika ni bora ukakaa kimya kuliko kujichumia dhambi ya kuwalisha watu maneno au kuwasingizia sio vizuri ivo mkuu.

hakuna kitabu chochote cha kanisa katoliki wala waraka wa kanisa katoliki unaoleza kwamba "yesu hawatambui wote wasiokuwa wakatoki" haupo duniani popote.

zaidi ya hayo wewe pamoja na kejeli zako zote sisi wakatoliki bado tunakuita "taifa la Mungu"

nenda katafute hati namba moja ya vatcan II iitwayo HATI JUU YA KANISA "lumen gentium" mwanga wa mataifa sura ya pili, kipengele cha "kanisa na wokovu" kakisome vizuri ukimaliza ndo urudi hapa kudai ulichoandika hapo juu

AHSANTE
 
Wasabato wameshagawanyika, wapo makundi matatu, Kuna wasabato masalia, Kuna wale wasabato watunza sabato. Na Kuna wasabato maboresho.
Ni sheeeeeeddaaaa. Muda sio mrefu utawasikia wamesambaratika. Walichobakiz ni kutukana wakatoliki. Baaass yaani kwao adui wao mkubwa ni katoliki kuliko hata shetani.
Mahubiri yao kutukana ukatoliki na siyo kumtukuza Mungu. Na kumkana shetani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wanaukosoa ukatoliki kwa hoja za kwenye bible but wakatolik badala ya kujibu kwakutumia hoja za kwenye bible wao wanaleta reference za vitabu vya kikatolik 😄😄😄😄😄 mimi c msabato ila sijawah kuona sehem wasabato wametukana wakatolik kama ipo nioneshe
 
ukikosa cha kuandika ni bora ukakaa kimya kuliko kujichumia dhambi ya kuwalisha watu maneno au kuwasingizia sio vizuri ivo mkuu.

hakuna kitabu chochote cha kanisa katoliki wala waraka wa kanisa katoliki unaoleza kwamba "yesu hawatambui wote wasiokuwa wakatoki" haupo duniani popote.

zaidi ya hayo wewe pamoja na kejeli zako zote sisi wakatoliki bado tunakuita "taifa la Mungu"

nenda katafute hati namba moja ya vatcan II iitwayo HATI JUU YA KANISA "lumen gentium" mwanga wa mataifa sura ya pili, kipengele cha "kanisa na wokovu" kakisome vizuri ukimaliza ndo urudi hapa kudai ulichoandika hapo juu

AHSANTE
Yesu
 
Hizi dini za wazungu hiz ni bure kabisa ona hii nini sasa.....na hawa ni wakristo wakatolik
downloadfile-148.jpg
 
ukikosa cha kuandika ni bora ukakaa kimya kuliko kujichumia dhambi ya kuwalisha watu maneno au kuwasingizia sio vizuri ivo mkuu.

hakuna kitabu chochote cha kanisa katoliki wala waraka wa kanisa katoliki unaoleza kwamba "yesu hawatambui wote wasiokuwa wakatoki" haupo duniani popote.

zaidi ya hayo wewe pamoja na kejeli zako zote sisi wakatoliki bado tunakuita "taifa la Mungu"

nenda katafute hati namba moja ya vatcan II iitwayo HATI JUU YA KANISA "lumen gentium" mwanga wa mataifa sura ya pili, kipengele cha "kanisa na wokovu" kakisome vizuri ukimaliza ndo urudi hapa kudai ulichoandika hapo juu

AHSANTE
downloadfile-148.jpg
 
Je, Papa Ndiye “Mrithi wa Mtakatifu Petro”?

*MNAMO 2002,* Papa Yohana Paulo wa Pili alimwandikia barua askofu wa Limburg, huko Ujerumani, akifutilia mbali uamuzi uliofanywa na askofu huyo kuhusu suala la kutoa mimba. Papa alianza kutoa maagizo yake kwa kusema kwamba anawajibu wa kuhakikisha kuwa “makanisa yote yako katika hali njema na yana umoja kulingana na mapenzi ya Yesu Kristo.” Alidai kuwa ana mamlaka ya kufutilia mbali uamuzi uliofanywa na askofu huyo kwa sababu akiwa papa, yeye ndiye “mrithi wa Mtakatifu Petro.”
Kulingana na tafsiri fulani ya Kanisa Katoliki, “Kristo alimweka rasmi Mt. Petro kuwa mkuu wa mitume wote.” Kanisa Katoliki linaendelea kudai kwamba “Kristo alisema kwamba Petro anapaswa kuwa na watu watakaomrithi katika cheo hicho; na kwamba maaskofu Waroma ndio warithi wake. _”—New Catholic Encyclopedia (2003), Buku la 11, ukurasa wa 495-496._

Hayo ni madai mazito. Je, wewe mwenyewe umewahi kuchunguza ukweli wa madai hayo? Ona majibu ya maswali haya matatu: *(1) Je, Biblia inaunga mkono dai la kwamba Petro alikuwa ndiye papa wa kwanza? (2) Historia inaonyesha nini kuhusu chanzo cha mfuatano wa mapapa? (3) Je, mwenendo na mafundisho ya mapapa yanaunga mkono dai lao la kwamba wao ni warithi wa Petro?*

*Je, Petro Ndiye Aliyekuwa Papa wa Kwanza?*

Ili kuthibitisha kwamba kanisa limejengwa juu ya Petro, kwa muda mrefu Wakatoliki wametegemeza madai yao katika maneno ya Yesu kwenye Mathayo 16:18: “Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu.” (Union Version) Hata maneno hayo yameandikwa kwa Kilatini chini ya dari la kanisa linaloitwa St. Peter’s Basilica huko Rome.

Agustino, Baba wa Kanisa aliyeheshimiwa sana, wakati fulani alisema kanisa limejengwa juu ya Petro. Hata hivyo, mwishoni mwa maisha yake alibadili maoni yake kuhusu maana ya maneno hayo ya Yesu. Kwenye kitabu kinachoitwa Retractations, Agustino alisema kwamba kanisa, yaani, kutaniko la Kikristo, limejengwa juu ya Yesu na si juu ya Petro.*

Ni kweli kwamba mtume Petro anatajwa sana katika vitabu vya Injili. Yesu aliwachagua mitume wake watatu—Yohana, Yakobo, na Petro—wawe pamoja naye kushuhudia matukio kadhaa ya pekee. (Marko 5:37, 38; 9:2; 14:33) Yesu alimkabidhi Petro “funguo za ufalme wa mbinguni,” ambazo alitumia kufungua njia ya kuelekea kwenye Ufalme—kwanza kwa Wayahudi na watu waliogeuzwa imani, kisha Wasamaria, na hatimaye Watu wa Mataifa. (Mathayo 16:19; Matendo 2:5, 41; 8:14-17; 10:45) Kwa sababu Petro alikuwa mchangamfu na alipenda kuongea na watu, mara kwa mara alitumika akiwa msemaji wa mitume wote. (Matendo 1:15; 2:14) Hata hivyo, je, mambo hayo yalimfanya Petro kuwa kiongozi wa kutaniko la kwanza?

Ni kweli kwamba mtume Paulo aliandika kuwa Petro alikabidhiwa “utume kwa wale waliotahiriwa.” (Wagalatia 2:8) Hata hivyo, muktadha wa maneno hayo unaonyesha kwamba Paulo hakuwa akimaanisha kuwa Petro ndiye kiongozi wa kutaniko. Maneno ya Paulo yalihusu jukumu la Petro katika kazi ya kuwahubiria Wayahudi.

Ingawa Petro alipewa majukumu makubwa, hakuna mahali popote katika Biblia ambapo anadai kuwa yeye ndiye kiongozi wa kutaniko, na hivyo kufanya maamuzi kwa ajili ya mitume wale wengine wote. Katika barua zake alijiita “mtume” na “mwanamume mzee,” naye hakuongeza jambo lingine lolote.—1 Petro 1:1; 5:1.

*Historia Inaonyesha Nini Kuhusu Chanzo cha Upapa?*

Wazo la kuwa na mapapa lilianza jinsi gani na wakati gani? Wazo la kwamba ilikuwa sawa kwa mtu mmoja kuwa na madaraka juu ya waamini wenzake lilianza wakati mitume walipokuwa wangali hai. Mitume walikuwa na maoni gani kuhusu jambo hilo?

Mtume Petro mwenyewe aliwaambia wanaume waliokuwa wakiongoza katika makutaniko wasiwe ‘wakipiga ubwana juu ya wale ambao ni urithi wa Mungu’; walipaswa kuwa wanyenyekevu kwa mmoja na mwenzake. (1 Petro 5:1-5) Mtume Paulo alionya kwamba katika kutaniko, watu wangesimama ambao ‘wangesema mambo yaliyopotoka ili kuwavuta wanafunzi wawafuate wao wenyewe.’ (Matendo 20:30) Mwishoni mwa karne ya kwanza W.K., mtume Yohana aliandika barua ambamo alimshutumu vikali mwanafunzi aliyeitwa Diotrefe. Kwa nini? Sababu moja ni kwamba mwanamume huyo ‘alipenda kuwa na mahali pa kwanza’ kutanikoni. (3 Yohana 9) Shauri kama hilo kutoka kwa mitume lilikuwa kama kizuizi, likizuia kwa muda tamaa ya wale waliotaka kuwa na madaraka.*2 Wathesalonike 2:3-8*.

Muda mfupi baada ya mtume wa mwisho kufa, watu mbalimbali walianza kupata mamlaka. Kitabu The Cambridge History of Christianity kinasema: “Huenda hakukuwa na askofu aliyekuwa na nguvu au mamlaka huko Roma mwanzoni mwa karne ya pili.” Kufikia karne ya tatu, askofu wa Roma alijifanya mwenyewe kuwa ndiye mamlaka kuu, kwenye makanisa fulani.* Ili kuongezea uzito lile dai la kwamba askofu wa Roma ana mamlaka kubwa, watu fulani wamekusanya orodha ya mapapa waliomrithi Petro.

Hata hivyo, orodha hiyo haiwezi kuthibitisha dai hilo. Kwa nini? Kwanza, baadhi ya majina kwenye orodha hiyo hayawezi kuthibitishwa. Zaidi ya hilo, msingi wa orodha hiyo una makosa. Jinsi gani? Hata ikiwa Petro alihubiri jijini Roma, kama baadhi ya vitabu vya kilimwengu vya karne ya pili na ya tatu vinavyodokeza, hakuna uthibitisho wa kwamba alikuwa kiongozi wa kutaniko huko.

Uthibitisho mmoja wa kwamba Petro hakuwa kiongozi wa kutaniko la Roma ni kwamba wakati mtume Paulo alipoandika barua yake kwa Waroma, aliandika orodha ndefu ya Wakristo waliokuwa huko. Hata hivyo, hakumtaja Petro hata kidogo. *(Waroma 16:1-23)* Ikiwa Petro alikuwa kiongozi wa kutaniko, je, tunaweza kuwazia Paulo akimsahau au kumpuuza?

Ona pia kwamba, karibu na wakati ambapo Petro aliongozwa na roho ya Mungu kuandika barua yake ya kwanza, Paulo alimwandikia Timotheo barua ya pili. Katika barua hiyo, Paulo hakusita kutaja Roma. Paulo aliandika barua sita akiwa Roma, na katika barua hizo zote hakumtaja Petro.

Miaka 30 hivi baada ya Paulo kuandika barua zake, mtume Yohana aliandika barua tatu na kitabu cha Ufunuo. Hakuna mahali popote katika maandishi hayo ambapo Yohana anataja kwamba kutaniko la Roma lilikuwa ndilo maarufu zaidi, wala kumtaja yeyote kuwa kiongozi wa kutaniko hilo ambaye alikuwa na mamlaka kubwa na aliyedai kuwa mrithi wa Petro. Hakuna uthibitisho wowote katika Biblia wala katika historia unaounga mkono dai la kwamba Petro alijiweka mwenyewe kuwa askofu wa kwanza wa kutaniko la Roma.

*Je, Mwenendo na Mafundisho ya Mapapa Yanaunga Mkono Dai Lao?*

Tungetarajia kwamba mtu anayedai kuwa “mrithi wa Mtakatifu Petro” na “Mwakilishi wa Kristo” afuate mwenendo na mafundisho ya Petro na Kristo. Kwa mfano, je, Petro alikubali kutendewa kwa njia ya pekee na waamini wenzake? Hapana. Hakukubali kutukuzwa wala kuitwa majina ya cheo. *(Matendo 10:25, 26)* Namna gani Yesu? Alisema kwamba alikuja kuwahudumia wengine na si kuhudumiwa. *(Mathayo 20:28)* Kinyume cha hilo, mapapa wana sifa gani? Je, wanakataa umaarufu, vyeo vya juu, na kuepuka kuonyesha waziwazi utajiri na mamlaka yao?

Petro na Kristo walikuwa safi kiadili na walichangia amani. Linganisha sifa zao na yale ambayo kitabu kimoja cha marejeo cha Wakatoliki, Lexikon für Theologie und Kirche _(Kamusi ya Theolojia na Kanisa),_ kinavyosema kuhusu Papa Leo wa Kumi: “Alijiingiza katika siasa na mara nyingi aliwapendelea watu wake wa ukoo katika shughuli za biashara na kupenda sana anasa. Kwa kufanya hivyo, Leo wa Kumi alipuuza mambo ya kiroho yaliyokuwa muhimu.” Karl Amon, kasisi Mkatoliki ambaye pia ni profesa wa historia ya kanisa, anasema kwamba habari zilizothibitishwa kuhusu Papa Aleksanda wa Sita zinaonyesha “uovu mwingi, matumizi mabaya ya mamlaka, kununua au kuuza vyeo katika kanisa, na upotovu wa maadili.”
Namna gani mafundisho ya mapapa? Je, yanapatana na mafundisho ya Petro na Kristo? Petro hakuamini kwamba watu wote wema wanaenda mbinguni. Akimrejelea Mfalme mwema Daudi, Petro alisema hivi waziwazi: “Daudi hakupanda mbinguni.” (Matendo 2:34) Wala Petro hakufundisha kwamba watoto wachanga wanapaswa kubatizwa. Badala yake alifundisha kwamba ubatizo ni hatua ambayo mwamini anachukua kwa kuongozwa na dhamiri yake.—1 Petro 3:21.

Yesu aliwafundisha wanafunzi wake kwamba hakuna yeyote kati yao anayepaswa kuwa mkuu kuliko wengine. Yesu alisema: “Ikiwa mtu yeyote anataka kuwa wa kwanza, lazima awe wa mwisho kati ya wote na mhudumu wa wote.” (Marko 9:35) Muda mfupi kabla ya kifo chake, Yesu aliwapa wafuasi wake agizo hili lililo wazi: “Msiitwe Rabi, kwa maana mwalimu wenu ni mmoja, lakini ninyi nyote ni ndugu. Zaidi ya hayo, msimwite mtu yeyote baba yenu duniani, kwa maana Baba yenu ni mmoja, Yule wa mbinguni. Wala msiitwe ‘viongozi,’ kwa maana Kiongozi wenu ni mmoja, Kristo.” (Mathayo 23:1, 8-10)
*Je, unafikiri mapapa wamefuata mafundisho ya Petro na Kristo?*

Wengine wanasema kwamba mtu anaweza kuendelea kuwa papa hata ikiwa haishi kulingana na kanuni za Kikristo. Je, unafikiri hoja hiyo inapatana na akili? Yesu alisema: “Kila mti mzuri huzaa matunda mazuri, lakini kila mti uliooza huzaa matunda yasiyofaa; mti mzuri hauwezi kuzaa matunda yasiyofaa, wala mti uliooza hauwezi kuzaa matunda mazuri.” Ukitegemea uthibitisho ambao umetolewa, je, unafikiri kwamba Petro au Kristo wangependa kuhusianishwa na matunda ambayo mapapa wametokeza?— *Mathayo 7:17, 18, 21-23*.

Mazungumzo ya Yesu na Petro yalihusu kumtambua Kristo na jukumu lake, na si kuhusu jukumu ambalo Petro angetimiza. *(Mathayo 16:13-17)* Baadaye, Petro mwenyewe alisema kwamba Yesu ndiye mwamba ambao juu yake kutaniko lingejengwa. (1 Petro 2:4-8) Mtume Paulo alithibitisha kuwa Yesu, wala si Petro, ndiye “jiwe la msingi la pembeni” la kutaniko la Kikristo.—Waefeso 2:20.

Yesu na mitume walionya kwamba kutaniko la Kikristo lingevamiwa na watu ambao wangefundisha mafundisho ya uasi. (Mathayo 13:24-30, 36-43; 2 Timotheo 4:3; 2 Petro 2:1; 1 Yohana 2:18) Maneno hayo yalitimia wakati kanisa, au kutaniko, la karne ya pili lilipoanza kukubali mapokeo ya kipagani na kuchanganya mafundisho ya Biblia na falsafa za Wagiriki.

Sent using Jamii Forums mobile app

Usiulize babu pigia mstari
 
Back
Top Bottom