ndugu nimesoma hilo andiko lote hapo juu na kugundua yafuatayo.....
HUFAHAMU VYEMA TAMADUNI NA MILA ZA KIYAHUDI KWA WAKATI WA YESU, PIA MAISHA NA WAJIBU WA MARABI ENZI ZA YESU NA HUMFAHAMU VYEMA PETRO MTUME NA KHALIFA WA KRISTO MWENYEWE....
bahati mbaya nasikitika kukwambia kuwa KUNA VITU NA MAMBO YA MSINGI KATIKA MAISHA YA YESU NA UTAMADUNI WA KIYAHUDI (KWA MWALIMU/RABI KUWA NA WANAFUNZI NA MKUBWA WAO) LAZIMA UTAKUWA HUVIFAHAMU.......
na nadhani ndio chanzo hasa cha madai yako kuhusu PETRO NA KANISA KATOLIKI AMBAYO KWA KIASI KIKUBWA UMEDANGANYA NA NI UZUSHI AMBAO UNATAKIWA USAHIHISHWE....
SO, ninapenda kujibu maswali yako na kutolea ufafanuzi uliosahihi wa madai yako kwa kuanza kwanza na MITUME WA YESU JINSI NA KWANINI ALIWACHAGUA NA LENGO LA YEYE KUA NA HAO WANAFUNZI 12 NA MWISHO TUMUONE PETRO MWENYEWE JAPO KIUFUPI (hivyo vitu mkuu hujavizingatia kabisa kabla ya kuleta hiyo thread yako)...........
Basi, ili kupata majibu ya kuridhisha na sahihi kwa maswali yako yote, nimeona ni vyema nitoe kwanza maelezo mafupi juu ya utamaduni wa wayahudi na jambo la uanafunzi au ufuasi na kwa upande wa Yesu tunasikia neno Mitume.......
MITUME WA YESU, KWANINI MITUME 12, NA MALENGO YA YESU JUU YA HAO MITUME 12 NINI HASA
Hivi ndivyo ilivyokuwa kwa Yesu kuchagua idadi ya mitume 12. Yesu ni Mungu na alichokifanya alifanya kwa mapenzi yake
Ndugu tunaposikia wazo wanafunzi, wafuasi au mitume inafaa kwanza tulitangulize wazo la rabi.
Kama ilivyo sisi siku hizi kwamba kama kuna wanafunzi lazima kuwepo pia na mwalimu anayewafundisha hao wanafunzi, au kama kuna wafuasi basi lazima pawepo na mtu wanayemfuata. Hali kadharika, kama kuna mitume lazima pawepo na mtu anayewatuma
Kwa upande wa Wayahudi, rabi ndiye aliyekuwa mwalimu wa wanafunzi na hivyo hao aliowafundisha waliitwa wafuasi; waliitwa wanafunzi
Wakati ule kulikuwa na marabi wengi tu na kila rabi alikuwa na wanafunzi wake, kumbe kila rabi alikuwa na wale waliomfuata na mara nyingi huyo mwalimu yaani rabi alitangulia mbele na hao wanafunzi walimfuata kwa nyuma
Hii ndiyo sababu unaposoma Mk. 8:32 – 34 Yesu anapomwambia Petro kuwa arudi nyuma shetani, maana yake Petro alitangulia mbele.
Kumbe Petro kama mwanafunzi alipaswa kuwa nyuma aone yale ambayo mwalimu wake alikuwa akiyafanya. Alipaswa kufahamu kuwa wakati ule mwalimu alikuwa mmoja tu yaani Yesu.......
Historia ya urabi na uanafunzi kwa wayahudi ilianza rasmi kipindi ambacho wayahudi waliongozwa na Ezra baada ya kutoka utumwani Babiloni.
Kipindi hicho, watu walijitoa rasmi maisha yao yote kujifunza Maandiko Matakatifu, kuyafafanua na kuyazingirisha katika maisha yao ya kila siku.
Sasa, ili mmoja aonekane kuwa mtaalamu, mafunzo hao yalianza utotoni ambapo kijana wa kiume alimtafuta mwalimu wa sheria anayemtaka, na kumwomba ampokee kama mwanafunzi wake
Mwalimu alichunguza uwezo wa mwanafunzi kama anafaa kisha alimchukua. Mwanafunzi huyo alijiaminisha kwa mwalimu huyo kwa miaka kama ishirini hadi thelathini na ili kuonekana kuwa tayari mwanafunzi huyo ameiva kwa ujuzi na hekima, alitakiwa atimize miaka walau 40 na hapo ndipo mwalimu wake alimwekea mikono na jamii ikamtambua kama ni mwalimu wa Maandiko Matakatifu
Ishara ya nje urabi au ualimu ilikuwa ni kuvaa kanzu ndefu (Mk. 12:38 – 40) na hivyo watu walikuwa wanamsalimu kila alipokuwa wanapita. Hao marabi waliheshimiwa sana na watu.
Baada ya kuwa rabi (yaani mtalaamu wa Maandiko Matakatifu) mmoja alitakiwa kushika miiko kama hii;
kutoongea na mwanamke yeyote hadharani,
kutoshindwa swali lolote ambalo angeulizwa na watu, kutogusana na watu walionekana kuwa najisi au wenye dhambi kama vile wakoma, wanawake walio hedhini. n.k.
Kwa upande wa Yesu, Biblia inamtaja kuwa alikuwa rabi (Yoh. 1:38). Pia tunasikia mafarisayo wanamwita Yesu mwalimu pale walipomletea mwanamke aliyefumaniwa kwa uzinzi (Yoh. 8:4).
Hata hivyo, Biblia haituambii kuwa Yesu alipataje kuwa rabi/mwalimu. Na tunaona watu wanashangaa kuwa aliwezaje kupata hekima ile - yaani kuweza kufundisha kama rabi wakati hakupata kuwa mwanafunzi wa rabi yeyote katika Uyahudi. Ukisoma enjili ya Marko 6:2-3 inaonekana watu wa nyumbani kwake wanamshangaa. Cha ajabu zaidi, tunasikia kwamba alipokuwa na miaka 12 tu alishaanza kuuliza na kujibu maswali ya wazee. (Lk, 2:46 – 47).
Ndiyo kusema, alipata urabi wa kuzaliwa nao. Hukuupata urabi kwa kusotea kama walivyofanya marabi wengine.
Kwa hiyo, Yesu alishaonekana kuwa rabi na hivyo alikuwa na wafuasi wake au wanafunzi wake kama ambavyo marabi wengine walikuwa na wanafunzi.
Tofauti ya wanafunzi wa Yesu na wale wa marabi wengine ni kwamba, wale wa marabi wengine kwanza walikuwa wanaume tu na pili wao wenyewe wanafunzi ndiyo waliowachagua marabi;
kumbe kwa upande wa Yesu, Yesu mwenyewe ndiye aliyewachagua na hao wanafunzi walikuwa wa kike na wakiume.
Hata hivyo, tofauti nyingine ya wanafunzi wa marabi wengine na wa Yesu ni kwamba, wanafunzi wa Yesu walikuwa wa makundi mawili:
kulikuwa na wafuasi au wanafunzi wa kawaida (yaani wale ambao walimfuata ili kusikiliza mafundisho yake, kwa vile walivutiwa nayo na walivutiwa pia na alivyokuwa anaishi).
Hawa walikuwa wengi na ni wanaume na wanawake (Lk. 8:2). Mfano wa wanawake wanaotajwa ni Maria Magdarena, Yoana mke wa Kuza, Mfanyakazi Mkuu wa Herode na Susana.
Baada ya kundi hili la wafuasi lilikuwa kundi lingine la pili nalo liliundwa na wanaume 12 waliochaguliwa na Yesu mwenyewe kutoka miongoni mwa wale wafuasi wengi, kama tusomavyo hapa,
“Siku moja Yesu alikwenda mlimani kusali, akakesha huko usiku kucha akisali. Kesho yake aliwaita wanafunzi wake, na miongoni mwao akawachagua watu kumi na wawili ambao aliwaita mitume: Simoni (ambaye alimpa jina Petro), na Andrea ndugu yake Yakobo, na Yohane, Filipo na Barthromayo, Mathayo na Thoma, Yakobo wa Alfayo, na Simoni (aliyeitwa Zelote), Yuda wa Yakobo na Yuda Iskarioti ambaye baadaye alikuwa msaliti.” Mwisho wa kunukuu (Lk. 6:12 – 15)
Aliwaita mitume kwa sababu aliwataka si tu wasikilize yale aliyowafundisha na kubaki nayo, bali pia wao aliwataka wakawafundishe na watu wengine. Kwa maneno mengine, aliwataka wajue kusudi awatume wayatangaza yale aliyowaambia; yale waliyoyaona kwake. Anapowaita anasema,
“Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani, Nendeni basi, mkawafanye watu wote kuwa wanafunzi wangu mkiwabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Wafundisheni kuyashika maagizo yote niliyowapeni.” (Mt. 28:19 – 20).
(MKUU UPO MPAKA HAPO....)
Kumbe hawa wanafunzi 12 ambao ndiyo tunawaita mitume, hakukuwa na mwanamke hata mmoja. Wote walikuwa wanaume watupu.
TUZIDI KUSONGA MBELE ILI KUUTAFUTA UKWELI ULIO HALISI.....
Kwa nini idadi ya mitume 12 na si vinginevyo na inawakilisha nini ????
idadi 12 ya wale mitume inawakilisha nini au kwa nini wawe 12 na si 24, 40, 50, n.k.......
ndugu yangu idadi hiyo ya kumi na mbili kwa kweli jibu la msingi kabisa ni kwamba Yeye anajua ni kwa nini aliwachagua kwa idadi hiyo kumi na mbili haikuwa kwa ajali tu,
ndiyo maana baada ya kupaa mbinguni mitume walimchagua Mathias achukuea nafasi ya Yuda Iskarioti ili kutimiza idadi hiyo ya kumi na mbili. (Mdo. 1:20 – 26). Huyu Yuda alijinyonga baada ya kumsaliti Yesu. (Mdo. 1:18 – 19).
Namba hiyo 12 ni idadi sawa ya makabila 12 ya wana wa Israeli; wana wa Yakobo ambao toka kwao ndiyo taifa la Israeli lilizaliwa pale mlimani Sinai kwa kupewa zile amri kumi kama katiba.
Wale watoto kumi na mbili wa Yakobo ambao majini yao si mbaya kama nikiyataja hapa: Reubeni, Simeoni, Yuda, Zabuloni, Isakari, Dani, Gadi, Asheri, Naftari, Yosefu, Lawi, na Yosefu. Haya ndiyo makabila kumi na mawili ya watoto wa Yakobo walioingia katika nchi ya Kanaani na kuirithi ila nchi ambayo baba yao Ibrahimu aliahidiwa na Mungu. (Mwa. 13:1 – 18).
Kumbe sasa, anapofika Yesu, anaanzisha taifa jipya la wakristo ambao wanatokana na hao mitume kumi na mbili kama vile taifa la Israeli lilivyoanza na watu 12. Sikia hapa mtume Petro anavyosema.
nanukuu:
“Lakini ninyi ni ukoo mteule, makuhani wa mfalme, taifa takatifu; watu wake Mungu mwenyewe, mlioteuliwa kutangaza matendo makuu ya Mungu aliyewaiteni kutoka gizani.” (1Pet. 2:9).
Kwa hiyo taifa jipya la wakristo, ambalo urithi wao si tena wa Yerusalemu la Kanaani, bali Yerusalemu ya Mbinguni. (Ufun. 21:9 – 14).
Hivyo idadi yao si 24 au 40 au 50 kwa sababu wanaoashiriwa ni watu 12 wa Agano la Kale na hawa wanaanza Agano Jipya. Watu wa taifa jipya ambalo hatima yake si kama ile ya zamani, bali mpya – mbinguni.
(HICHO KIPANDE HAPO JUUKINAWEZA KUWA NI MOJA JIBU NA UFAFANUZI KATIKA MADAI YAKO)
Mwisho wa hiki kipande cha mitume napenda kufafanua kifupi juu ya uhusiano wa mitume 12 na Kanisa la sasa.(KATOLIKI)
Yesu aliteua mitume wale kumi na mbili ili washiriki ukuhani wake kama viongozi wa Kanisa. Wao walipewa mamlaka hayo chini ya kiongozi wao Simoni Petro (Mt. 16:13 – 19).
Kumbe hao mitume ndiyo maaskofu wakisaidiwa na mapadre wa leo hii chini ya kiongozi wao Baba Mtakatifu kama ndiye halifa wa Petro.
Kwa upande mwingine, wale wote waliompokea Yesu, huitwa wafuasi wake. Hawa ni sawa na wale wafuasi wengine wa Yesu ambao hawakuwa mitume.
Hawa nao wanashiriki ukuhani wa Kristo lakini si kama Kristo mwenyewe katika maaskofu na mapadre.
Wao wanashiriki kwa ushuhuda wa maisha yao na kutangaza neno la Mungu. Kundi hili ni la wabatizwa wote. Wao wana upadre/ukuhani wa wate. Wenzetu waingereza wanauita Common Priesthood. (1Pet. 2:9; Rev. 1:6).
tusonge mbele katika kuutafuta ukweli na uhalisia wa PETRO na kanisa KATOLIKI....
sasa naomba tumtazame MTUME PETRO (KHALIFA WA KWANZA WA KRISTO) JAPO KIUFUPI MAISHA YAKE MPAKA KIFO CHAKE.....
Petro alifia wapi na kwa sababu gani na nini kiliendelea baada ya hapo
Ni kweli kabisa kwamba kama walivyo binadamu wengine, Petro alizaliwa na kuishi, kipindi na muda wake wa kuishi ulipomalizika alikufa.
Petro mtume ndiye alikabidhiwa kanisa na Bwana wetu Yesu Kristo kabla ya kifo na ufufuko wake rej.Mt 16:18.
Jina lake halisi lilikuwa Simon Bar-Yona mwenyeji wa Galilaya.Kazi yake ilikuwa ni uvuvi kabla hajaitwa kuvua watu kama tunavyosoma Mt 4:18-20.
Pamoja na kwamba Petro anatufundisha mambo mengi,Biblia haituelezi mwisho wa maisha yake.Tunachoambiwa ni kwamba,baada ya mitume kumpokea Roho Mtakatifu,siku ile ya pentekoste walianza kazi ya Kutangaza habari za ufufuko wa Yesu.
Kazi ya kutangaza habari za ufufuko wa Yesu ilikuwa ngumu na iliwabidi mitume wasambae huko na huko ili kueneza habari hiyo kwa watu.Habari za mitume na kazi zao baada ya kumpokea Roho Mtakatifu tunazipata kutoka katika kitabu cha Matendo ya mitume.
Sasa,kuhusiana na Petro,maelezo ya wazi kutoka katika Biblia Takatifu yanaanza pale tunapoelezwa juu ya Philip ambaye baada ya kumpokea Roho Mtakatifu alienda hadi Samaria na huko akafanikiwa kupata wafuasi wengi.
Aliporudi kanisa la Yerusalemu likamtuma Petro ili akatoe msaada zaidi huko rej.Mdo 8:14-16,baada ya hapo tunaambiwa kwamba Petro alikwenda hadi Kaisaria akambatiza Kornelio rej.Mdo 9:32,
halafu alipotoka huko Petro alirudi Yerusalemu akakamatwa na Herode Agrippa akafungwa rej Mdo 12:1-3,na baada ya kuokolewa kwa muujiza na malaika toka gerezani,Biblia inatuambia kwamba aliamua kuwa mhubiri wa mataifa rej.Mdo12:17-19.
Maelezo hayo ndiyo yaliyo wazi kabisa kutoka katika Biblia yetu.Hapa ndipo sasa utajiri wa kanisa katoliki unapodhihirishwa wazi linapotumia vyanzo vikuu viwili vya mafundisho ya imani yaani Biblia Takatifu na Mapokeo.Utajiri tulionao kutoka katika mapokeo ndio unaoweza kutufanya kupata na kujua mambo na habari muhimu kuhusu petro.
Watu wa madhehebu mengine yasiyo ya kikatoliki hawana na hawapendi kutumia chanzo hiki cha mafundisho ya imani yaani mapokeo ndiyo maana kwao inaweza kuwa vigumu kujua kama alikufa na kuzikwa mahali fulani ingawa wanaamini kwamba aliishi kwani hilo halimo katika Biblia Takatifu.
Kutokana na mapokeo Petro baada ya kutoka Yerusalemu inasadikika kwamba alikwenda kati ya Antiokia au Alexandria.Ndiyo maana ukisoma Mdo 15:7-11 pale katika mkutano wa Yerusalemu Petro anaongea kama mmisionari na ukisoma pia Gal 2:7-8 Petro anatajwa kama mtu aliyewahubiria wayahudi.
Sasa,alipotoka huko yaani Antiokia au Alexandria ndipo alikwenda Roma na huko akachaguliwa kuwa kiongozi mkuu wa mitume na Askofu wa kwanza wa Roma.Kama kiongozi wa Roma Petro alifanya kazi katika mazingira magumu maana ilimbidi apingane na utawala wa kirumi uliokuwa chini ya Nero aliyekuwa adui wa wakristo.
Mababa wa kanisa yaani wale ambao walikuwa wanafunzi wa mitume au wafuasi wa wanafunzi wa mitume, wanatupatia habari nyingi zaidi kuhusu Petro.Wa kwanza anayetupatia habari hizo ni Clement wa Roma.Huyu ndiye aliyekuwa askofu wa tatu wa Roma baada ya Petro na Linus.
Katika barua yake kwa wakorintho aliyoiandika mwaka 96 BK aliwataarifu wakorintho kwamba Petro na Paulo waliuawa huko Roma na aliyewaua ni Nero kutokana na wivu na chuki kwa kanisa.Ukitaka kuelewa juu ya mateso waliyoyapata hawa wawili naomba usome 2kor 11:23-27.
Baada ya mateso kutoka kwa Nero kuzidi, Petro aliamua kutoroka kutoka Roma.Mapokeo yanatudhihirishia kwamba alipokuwa akiondoka kutoka mjini Roma, alikutana na Yesu ndipo Petro akamuuliza Yesu akisema, “ QUO VADIS”,tafsiri yake “unakwenda wapi”?.Yesu akamjibu, “nakwenda huko Roma unakotoka nikasulibiwe tena”.
Hapo Petro alijisikia vibaya kuona kwamba anayakimbia mateso aliyokubali kuyapokea siku alipokubali kwa dhati kuwa mfuasi wa Yesu.Akaamua kurudi tena Roma.
Baba wa kanisa Tacitus katika maandishi yake anasema kwamba aliporudi Roma alikamatwa na kusulibiwa akachagua kuteswa msalabani kichwa chini miguu juu maana Petro mwenyewe alisema kwamba hakustahili kusulibiwa kama Bwana wake Yesu Kristo.
Baada ya kifo chake, Petro alizikwa mahali ambapo leo hii kanisa linalojulikana kama kanisa la Mt Petro limejengwa yaani huko Vatican Roma. Kinachotuthibitishia hilo ni kile kilichotokea mwaka 1939 hadi 1949 wakati kanisa hilo la Mt.Petro lilipokuwa likifanyiwa ukarabati.
Wajenzi waliligundua kaburi lake na kwa uhakika wote walielewa kwamba ndilo hasa lenyewe walipokuta ukuta mwekundu wenye maandishi ya kigiriki yaliyosomeka, “PETROS ENI ” tafsiri yake kwa kiingereza ni“PETER IS INSIDE”,na kwa kiswahili,“PETRO YUMO NDANI”.
Mwaka 1950 siku ya Krismasi Baba mtakatifu Papa Pius XII alithibitisha hilo.Mambo haya ya kale sisi tunashindwa kuyaelewa kwa urahisi kwa sababu hatujihusishi sana nayo kama ndugu zetu wa nchi zilizoendelea wale wanaoitwa archeologists.
MWISHO NAOMBA UELEWE KUWA BABA MTAKATIFU AU PAPA NI NANI HASA
naomba nieleze kinagaubaga kuhusu Baba Mtakatifu au Papa ni nani, sawia na mamlaka yake katika Kanisa Katoliki.
Papa au Baba Mtakatifu ni wakili wa Yesu Kristo, Halifa wa Mtume Petro, Mkuu wa Kanisa Katoliki, Askofu wa jimbo la Roma, na Baba wa Kanisa la Magharibi ambalo kabla ya Mtaguso wa Mkuu wa pili wa Vaticano, lilitumia lugha ya Kilatini katika Ibada zake. Zaidi ya hapo Baba Mtakatifu ni Mkuu wa Jimbo la Kanisa la Italia na ni Rais wa Nchi ndogo ya Vaticani.
Kadiri ya Imani Katoliki, cheo cha Baba Mtakatifu kinatokana na ujumbe aliopewa Mtume Petro na Bwana wetu Yesu Kristo mwenyewe. Mtume Petro, kufuatana na ushahidi dhahiri alikufa Roma, na kaburi lake liligunduliwa chini ya Altare kuu ya Kanisa la Mtakatifu Petro huko Roma.
Tukirejea kwenye sheria za Kanisa Katoliki ambazo ni ufafanuzi wa zile amri Kumi za Mungu, sheria namba 331, inasema hivi nanukuu; “Askofu wa Kanisa la Roma ambaye katika yeye inadumu ofisi iliyokabidhiwa na Bwana kwa Petro mwenyewe, wa kwanza katika Mitume na inayopaswa kupitishwa kwa Mahalifa wake ni Mkuu wa jopo la Maaskofu, wakili wa Kristo na mchungaji wa Kanisa zima hapa duniani; hivyo kwa dhati ya ofisi yake anayo madaraka ya kawaida, ya juu, kamili, yanayojitegemea, naya jumla katika Kanisa, ambayo anaweza daima kuyatumia kwa uhuru”. Mwisho wa nukuu.
Pia sheria ya Kanisa Katoliki namba 333, inasema, nanukuu; “Baba Mtakatifu hupata madaraka kamili na ya juu katika Kanisa kwa njia ya uchaguzi halali alioukubali mwenyewe pamoja na kupewa uaskofu. Hivyo Yule aliye Askofu tayari hupata madaraka hayo tangu wakati anapokubali uchaguzi wake kuwa Baba Mtakatifu. Lakini kama Yule aliyechaguliwa hana uaskofu, anabidika kupewa uaskofu mara moja”. Mwisho wa nukuu, hata hivyo kifungu cha pili cha sheria hiyo namba 333, kinasema hivi, nanukuu, “Ikitokea kuwa Baba Mtakatifu anajiuzulu ofisi yake, ili iwe halali inatakiwa ajiuzulu kwa hiari na tendo hilo lidhihirishwe ipaswavyo, lakini si kwamba likubaliwe na yeyote”. Mwisho wa nukuu.
baada ya maelezo hayo mafupi kuhusu Baba Mtakatifu kama ni nani na wadhifa wake katika Kanisa Katoliki, naomba sasa twnde kwenye chimbuko la jina papa
chimbuko la jina hili Papa, hadi wakawa wanapewa viongozi hawa wa dunia wa Kanisa Katoliki, ni kwamba jina hili Papa ni neno la Kiitaliano ambalo limetokana na neno la Kigiriki Pappas, ambalo kwa kiingereza ni Fadher na Baba kwa lugha yetu ya Kiswahili.
Neno hili Papa lilitumiwa na Mapadre wa Makanisa ya Kigiriki. Na hapo ndipo sasa Mababa wa Kanisa Katoliki wakaona ni jina linalofaa apewe kiongozi wa dunia wa Kanisa Katoliki, yaani Baba Mtakatifu, kulingana na hadhi yake kama Baba wa Wakatoliki wote duniani.
Baba Mtakatifu ni kilele cha muundo wote wa daraja za Kanisa, na uwezo wote wa kimuundo katika Kanisa unatoka kwake, na hivyo tunaweza kusema ni sawa na Baba wa familia katika hali ya kawaida, kuwa yeye ni kichwa cha familia na anayo madaraka yote ya ndani ya familia ile. Ndivyo ilivyo kwa
Baba Mtakatifu kama halifa wa Mtume Petro, Askofu wa Roma, wakili wa Yesu Kristo hapa duniani na mkubwa wa Kanisa Katoliki (rej. Mt 16:18-19; Yn 10:16). Nanukuu, “Nami nakuambia: Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga Kanisa langu, wala milango ya kuzimu haitalishinda.
Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lolote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni, na lolote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni”. Mwisho wa nukuu (rej. Mt 16:18-19).
Zaidi ya hapo, zamani hizo, jina hili Papa (yaani Baba), lilitolewa kwa Maaskofu, na lilitumiwa sana katika mzingo wa Kimonaki na likawa jina la kawaida kwa Mapadre wa Kanisa la Orthodoksi na pia Mapadre wa sehemu fulani za Kanisa Katoliki la Roma.
Na huko Misri jina hilo Papa lilikuwa ni haki ya Askofu wa Alexandria tu. Lakini kuanzia katikati ya karne ya sita (6th c), na kuendelea hadi hivi leo, jina hilo Papa limewekwa maalumu kwa ajili ya Askofu wa Roma tu, yaani kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani. Na utume huo uliwekwa kisheria na Baba Mtakatifu Gregori wa VII.
Sanjali na hilo kuna sababu za kimazingira kuwa Waitaliano ndiyo waliopokea mafundisho ya Mitume wenye sifa bora, nao ni Mtume Paulo na Mtume Petro ambaye alikuwa kiongozi wa Mitume na halifa wa Yesu Kristo.
Inasadikika kwamba Mitume hao wakuu yaani Perto na Paulo waliacha mafundisho ya Yesu mikononi mwa Waroma na ndiyo maana mpaka leo hii makao makuu ya Kanisa Katoliki yapo Roma. Kutokana na mapokeo ya Kanisa sisi tunajua kwamba Mtume Petro kama kiongozi wa Kanisa la Roma alikamatwa na Mfalme Nero pamoja na Paulo Mtume na Wakristo wengine wengi.
Na baada ya kufungwa katika gereza la Mamertino, Petro alisulubiwa katika shamba la kuzikia lililokuwa katika ukingo wa mlima Vatikano mwaka Sitini na Saba (67), na hivyo Wakristo wa zamani walijenga kumbukumbu hapo.
Tena, mara baada ya Mfalme Mkuu Konstantino kutoa uhuru wa dini, Wakristo kwa msaada wa Kaisari huyo walijenga Kanisa la kwanza juu ya kaburi la Mtume Petro, wakiliacha kaburi chini ya Altare. Na kwa udhibitisho walichimba kwa miaka mingi chini ya Altare ya Kanisa la Mtume Petro, na mwisho wakafika kwenye kaburi lenyewe kwa kukuta maneno “Petro iki” yaani Petro yu hapa.
Ndugu ili kudhibitisha ukuu wa Kanisa la Roma mapokeo yanasema ;
Askofu wa Lione (Ufaransa), mwaka 115, Mt. Ireneo aliyekuwa mfuasi wa Mt. Polycarpi ambaye ni mwanafunzi wa Mtume Yohane, aliandika maneno yafuatayo katika kitabu chake kinachoitwa Dhidi ya Waasi sura ya II.
Nanukuu, “Mafundisho ya Mitume duniani kote yaweza kupatikana katika kila Kanisa, na kila mtu anaweza kuyapata, sisi tunaweza kuleta orodha ya Maaskofu waliopata cheo kutoka kwa mitume na mahalifa wao, mfuatano hadi siku hizi zetu. Lakini ingekuwa kazi ya kuchosha mno kuleta katika kitabu hiki mfuatano huo wa Mitume katika Kanisa. Ni bora nilete mapokea ya kitume na mafundisho ya imani ya Kanisa kubwa zaidi, ya zamani zaidi na lililojulikana kwa watu wote, ambalo liliwekwa kwa kimsingi huko Roma na Mitume wenye sifa bora, yaani Petro na Paulo. Kanisa hili limefika kwetu hadi leo kwa njia ya mfuatano wa Maaskofu na Mahalifa wao. Sasa basi kila Kanisa, yaani waamini wa duniani kote lazima wakubaliane na kushirikiana na Kanisa la Roma, kwa sababu ya cheo chake bora sana”. Mwisho wa nukuu.
Na zaidi ya hapo kuna uhakika kuwa mapokeo ya Mitume yanahifadhiwa huko Roma na baada ya Mitume waadhama kuweka misingi ya Kanisa la Roma na kuliongoza, uaskofu walipitisha wao kwa Linus kwa ajili ya uongozi wa Kanisa zima. Linus huyu ni Yule anayekumbukwa na Mtume Paulo katika waraka wake wa pili kwa Timotheo, (rej. 2Tim 4:21).
ndugu kutokana na ukweli huo kuwa misingi ya Kanisa Katoliki iliwekwa Roma na Mitume hao maarufu, yaani Petro na Paulo, bila shaka utakubaliana nami kuwa Waitaliano ni moja ya watu walioachiwa Kanisa na kuchukua jukumu la kuendeleza kazi ya uenezaji wa neno la Mungu duniani kote, kama ilivyokuwa ujumbe wa Kristo mwenyewe kwa Mitume wake.
Nanukuu, “Basi, enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi. Na tazama mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari”. Mwisho wa nukuu (rej. Mt 28:19-20).
Kwa udhibitisho wa hilo na mengi zaidi ya hayo nilio kueleza toka mwanzo unaweza kutafuta na kukisoma kitabu chenye kichwa cha habari PAPA NI NANI, kilichoandikwa na Padre Medri na Padre Magnus Lunyungu ambaye
MKUU NAAMINI KUWA NITAKUWA NIMEKUJIBU VEMA KABISA HAYO MASWALI YAKO NA KUKUPATIA UFAFANUZI WA KWELI NA ILIO HALISI
AHSANTE..............