beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,881
- 6,377
Angalizo muhimu: Sina panya nyumbani kwangu!
Wakuu,
Naamini wengi tunazifahamu harakati za Panya majumbani mwetu so naomba leo tuliangalie suala hili kwa pamoja..
Ni hivi.. Katika story mbili tatu za kuchangamsha genge na watu wangu hapa, tukapata swali la ghafla; Kwanini Panya wanajificha sana hasa wawapo kwenye makazi ya binadamu!?
Yapo maoni mengi lakini mojawapo linashawishi zaidi ambalo linasema hivi;
Kwa mfano, wewe ungekuwa kiumbe ambaye unakutana na kiumbe kingine ambacho wewe ni kama asilimia 3 tu ya ukubwa wake, ungefanyaje?! Jibu la wazi ni kwamba ungefanya kila unachoweza kujiweka nacho mbali. Hiki ndicho anachokifanya bwana Panya.
Panya anaelewa kwamba wewe ni mkubwa sana kwa umbile kuliko yeye, hivyo ili kujilinda hana budi kukuepuka kama ukoma.. Japo hana uhakika kama utamdhuru au la, anashuku tu kwamba usalama wake mbele yako ni mdogo sana hivyo ili kuepusha shari anaamua tu kujiweka mbali..
Bwana Panya akikuona tu unasogea, basi atajikimbiza hata uvunguni mwa kitanda, nyuma ya ukuta au sehemu yoyote ambayo atahakikisha humuoni..
Kwa mtazamo huo huo ndugu yetu Panya anamuepuka Paka, Mbwa na kiumbe mwingine yeyote ambaye ataonekana mkubwa kwake.
Mtazamo huo unauonaje?!
Kama kuna majibu ya kitaalamu au mtazamo mbadala karibuni sana wadau..