Je, oil ya petrol italinda kenchi zangu?

Alejandroz

JF-Expert Member
Feb 14, 2017
327
376
Habari wana JF

Nimepaka oil ya petrol ambayo sio nyeusi sana kwenye kenchi zangu, ila nimekuwa na wasiwasi kama zitazilinda kenchi dhidi ya mchwa au inatakiwa oil yenye weusi mwingi kama ya diesel?

Naomba ushauri wako tafadhari.
 
Bora ungekuja kuomba ushauri kabla hata hujapaka hiyo petrol kwenye kenchi, ungepewa ushauri Murua.
Unakuja kuomba ushauri umeshapaka, je tukikuambia haifai utakwenda kubadilisha kenchi?
 
Duh petrol ni hatari sana. Siku ukiwasha mshumaa au jiko la gesi ikakamata kwenye kenchi huna nyumba. Nani alikushauri kufanya hicho kitu? Risk sana aisee usilale kwenye hiyo nyumba kabla huja-neutralize hiyo kemikali hatari kuliko zote duniani
 
Labda wasiwasi wangu upo katika kudumu kwa 'petrol' katka mbao zako. Petrol inatabia ya 'kuvepa' haraka tofauti mafuta mengine kama oil chafu.
Kuzuia wadudu inaweza Ila haiwezi dumu, itaondoka mapema kwa njia ya gesi.
Oil chafu ni nzuri kwa sababu hudumu, hukaa muda mrefu. Petrol pengine ingefaa katika kulainishia oil chafu (Kama nzito Sana) na si kutumika peke ake
 
Wadudu ni tatizo nimeshtuka,hivi naweza kupaka oil chafu kwenye kenchi hata baada ya kuezeka na kupiga blandering?
 
Duh petrol ni hatari sana. Siku ukiwasha mshumaa au jiko la gesi ikakamata kwenye kenchi huna nyumba. Nani alikushauri kufanya hicho kitu? Risk sana aisee usilale kwenye hiyo nyumba kabla huja-neutralize hiyo kemikali hatari kuliko zote duniani
Umenifurahisha sana, petrol ni compound ambayo ni volatile sana, ukiimwaga mahari ni dk chache inakuwa ime evaporate
 
Jamani mnazidi kumchanganya muuliza swali, ni kwamba kuna oil kwa ajili ya engine za petrol na oil kwa ajili ya engine za dizeli. Sasa yeye katumia oil safi ambayo haijatumika ya petrol engine. Ndio inakuwa nyeupe haijachafuka ikitumika inakuwa nyeusi.
 
kiwatilifu chenye kemikali ya imidacloprid kama Twiga Prid, Mida 200SL, Hotspot ( sina hakika na spelling), nk

Nimetumia Mida 200SL na nimeona matokeo, na nilipanda juu mimi mwenyewe sikuweka mtu
Hiko kiwatilifu unapaka kwenye mbao au unapulizia?
 
Back
Top Bottom