Je Obama anataarifa la jina Lake kutumika Kuwa-hadaa watanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je Obama anataarifa la jina Lake kutumika Kuwa-hadaa watanzania?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by August, Oct 3, 2010.

 1. A

  August JF-Expert Member

  #1
  Oct 3, 2010
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,509
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  kwa mara ya pili katika muda wa wiki moja mgombea moja wa Uraisi ametumia jina la Raisi wa merekani ili kuvutia wapiga kura, mwanzo ni pale alitumia hotuba ya obam kwenye millinium goal challenge meeting, na sasa hivi ni hili la misaada bila kuzingatia zaidi ya hapo kwamba hiyo misaada sio ya kwake binafsi bali ni kupitia mikataba iwe ya nchi moja moja bilatteral au ya nchi nyingi multi-latteral na zaidi ya hapo hata akija lipumba/slaa misaada hiyo itatoka tu.
   
 2. W

  We know next JF-Expert Member

  #2
  Oct 3, 2010
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Lazima Kijana yupo update, network yake si mchezo, na kwa jinsi alivyo, anaweza kuwaamuru wasaidizi wake, wamtwangie simu huyu anayetumia jina lake vibaya muwa aache mara moja. BO si mchezo, unakumbuka Uganda ktk kikao cha nchi za Africa mwezi wa nane? mwakilishi wake alisoma hotuba kwa niaba yake na akaweka wazi kuwa, atafanya ushawishi kwa mataifa mengine makubwa duniani ili kwamba viongozi wote wa Africa walioweka fedha zao ktk mabenki ya nje, atazitaifisha. That guy is No nonsense......Republican wenyewe pale wamenyosha mikono juu.
   
 3. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #3
  Oct 3, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Niliongelea ulimbukeni wa kumhusisha sana Obama katika uchaguzi wa Tanzania. Watanzania makini wakikusikia unaongelea sana habari za Obama watakuona utakuwa kiongozi kibaraka wa Wamarekani tu, watajiuliza unataka kuendeleza maslahi ya Watanzania au Wamarekani? Una fikira za kujitegemea au za uomba omba ? Unaweza kujiamini na kumpinga Obama kama maslahi ya Watanzania yatakutaka kufanya hivyo?

  Nimeongelea zaidi upuuzi wa kuabudu viongozi wa nje katika chaguzi zetu paragraph ya kumi hapa
   
 4. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #4
  Oct 3, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jk ni kama vitoto vya chekechea...ukikiahidi pipi lazima shule nzima ijue
   
Loading...