Je nitumie programu gani


Yona F. Maro

Yona F. Maro

R I P
Joined
Nov 2, 2006
Messages
4,235
Likes
52
Points
0
Yona F. Maro

Yona F. Maro

R I P
Joined Nov 2, 2006
4,235 52 0
Sahau kuhusu Bei ya programu hiyo mara nyingi bei inaweza kuonyesha kitu Fulani kuhusu programu husika haswa uwezo wake wa kufanya kazi husika kwa ufanisi zaidi nikimaanisha programu hiyo inaweza kushirikiana na programu zingine katika kufanya shuguli Fulani hili liko zaidi kwenye programu za kuchorea ambapo unaweza kulazimika kuongezea programu zingine ili uweze kufanya kitu Fulani kwenye mchoro au picha .

Lakini najiuliza nikitaka kununua programu yangu ya kompyuta niangalie vitu gani vya muhimu kabisa kabla ya kuamua kufanya uamuzi wa kununua na kwenda kutumia programu husika ?Kuna mambo kama 6 hivi ya kuangalia ingawa mengine yanaweza kuongezeka huko mbeleni .

Kama uko ofisi yenye kompyuta kwa mfano 20 na zaidi hakuna sababu ya wewe kununua kama ni CD kila kompyuta iwe na yake unaweza kuangalia programu zenye leseni nyingi kwa wakati mmoja hii itapunguza sana ufisadi na utendaji wa kazi , kuna programu inaitwa Landesk

Kama umeshafanya utafiti kwa njia ya mtandao mara nyingi unaweza kutumia mitandao mbalimbali kuangalia jinsi watu wanavyoongelea programu husika ni vizuri ukatembelea mitandao zaidi ya 5 hivi kwa sababu kuna mitandao ambayo iko kibiashara hii inahakikisha biashara zao zinaendelea kwahiyo huwezi kuona upande wa pili ukielezewa kuhusu programu unayotaka wewe .

Kabla ya kwenda mbele kumbuka kupata programu halali ambayo ina leseni yake ambayo imepatikana kwa mauziano halali , kama umenunua kwa njia ya mtandao kumbuka kuhifadhi kumbumbu hiyo kwa njia ya mbalimbali unaweza kuprinti ukahifadhi karatasi na njia nyingine mbalimbali .

Pia uwe makini sana sikuhizi kuna programu zinazoweza kutafuta leseni pamoja na namba za programu kwenye kompyuta angalia watu unaofanya nao kazi au wanaokupa msaada wanaweza kutumia programu kama hizi kuweza kuiba leseni yako lakini njia rahisi zaidi ni kusajili programu hiyo kwa njia ya mtandao haraka zaidi ili hali hii inapotokea unaweza kuwa na uwezo wa kudai haki yako .

Je komputa yako huko unapotaka kwenda kutumia programu husika zina uwezo wa kuingiza programu hiyo na kufanya kazi bila tatizo labda matatizo ya kawaida tu hapa namaanisha komputa hiyo ina memory ya kutosha , Vipi kuhusu nafasi kwenye Hardisk Drive yako ?, Kama ni programu ya kuchorea kuna suala la Rangi linalohusiana na VGA card kwenye kompyuta husika .

Programu nyingi zinazotoka sasa hivi zinazingatia sana uwezo wa VGA Card kwenye kompyuta yako mfano mzuri ni Autocad2010 ambapo ukiwekwa itafanya updates kwenye Driver za VGA sasa kama kuna shida au haina uwezo ina maana autocad2010 inaweza isifanye kazi kama inavyotakiwa au kutokufanya kazi kabisa .

Suala lingine ni Operating system unayotumia kama program tarajiwa inaweza kuingia kwenye operating system hiyo bila shida na hakutohitajika programu nyingine ya ziada zaidi ya updates ambazo zinatakiwa kuingia zenyewe unapounganisha kwenye komputa hiyo kwenye mtandao .


Tunaponunua programu za kompyuta hatutegemei kutokea matatizo lakini kama tatizo likitokea kwenye programu hiyo ufanye nini ? ndipo linapokuja suala la kupata huduma kwa wateja kwa haraka wepesi na bure , Unaponunua programu angalia sana kama Kuna kampuni zinazoweza kutoa msaada endapo italeta shida kampuni zilizo karibu na wewe au kama sio hivyo inabidi uweze kupata uwezo wa kupata msaada huo kupitia tovuti husika za kampuni zilizotengeneza programu hiyo .

Hilo la kupata updates kwenye programu yako ni la muhimu sana , sasa tabia za programu ambazo sio halali ni kwamba unakosa nafasi ya kufanya updates muhimu kwa njia ya mtandao pindi unapojaribu kufanya hivyo programu hiyo inaweza kuzuwa kufanya kazi au kukosa baadhi ya vitu muhimu mpaka utakaponunua leseni halali ya programu husika .

Unaponunua antivirus kwa mfano suala la kupata msaada ni muhimu inahusiana na ulinzi wa mali na masuala yako mengine nyeti kwahiyo kwenye tovuti za watengenezaji wa programu hizi kuna kuwa na forums unazoweza kuuliza maswali na hata kampuni nyingi zinakuwa na ushirikiano na kampuni mbalimbali duniani zinazoweza kukusaidia .

Kumekuwa na tatizo pia la watu kuelewa vitu Fulani kuhusu programu hizi kuna wengine wanaposikia programu Fulani imeshushwa kwa njia ya mtandao anaanza kuhisi inawezekana ameuziwa famba , inawezekana kununua programu kwa njia ya mtandao ukaweza kushusha programu hiyo na kupewa leseni yake pamoja na ushahidi mwingine kuonyesha uhalali wake ingawa kuna ambao wanalaghai watu haswa wale wasiojua au wanaotaka vitu kwa bei ambayo sio halali zaidi bei rahisi .

Je programu ninayotaka kutumia inaweza kuleta shida ninapotaka kufanya jambo Fulani kama kuscan hivi , hili lipo zaidi kwenye programu za ulinzi Mara nyingi unapotaka kuondoa Spyware kwa mfano kwenye komputa yako kutumia Programu ya kampuni tofauti na antivirus yako unaweza kupata ujumbe kwamba kuna programu inataka kubadilisha vitu kwenye System yako au Antivirus hiyo inaweza kudetect programu hiyo kama virus kwa mtu asiyejua atapata tabu sana kwahiyo utalazimika kutumia Antivirus yenye vitu vyote hivyo , Lakini ni vizuri upate kama ni Antispyware ambayo inaweza kufanya kazi bila programu zingine kudetect kama inataka kuleta madhara kwenye kompyuta .

Na kwa sasa lugha yetu ya Kiswahili inakuwa sana watu wengi sana wanatumia lugha hii je programu husika ina lugha ya Kiswahili au lugha ambayo wewe unaielewa kiurahisi kwa ajili ya utendaji ? Kuna kampuni kadhaa sasa zinatumia lugha ya Kiswahili katika programu zao kama Microsoft na zingine zinazotengeneza kamusi za kutumika kwenye kompyuta Kwahiyo hili ni suala muhimu sana .

Maelezo kama haya hawawezi kukamilika bila kupata maelezo ya ziada toka kwa wachangiaji wengine , karibu sana katika mjadala huu tuendelee kuelimisha wenzetu

www.wanabidii.net www.naombakazi.com
 
Baba_Enock

Baba_Enock

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Messages
6,900
Likes
338
Points
180
Baba_Enock

Baba_Enock

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2008
6,900 338 180
..najiuliza nikitaka kununua programu yangu ya kompyuta niangalie vitu gani vya muhimu kabisa kabla ya kuamua kufanya uamuzi wa kununua na kwenda kutumia programu husika ?
Hilo ndilo swali hapo juu la kuchangia? Maana naona umenza na ngonjera!
 
Yona F. Maro

Yona F. Maro

R I P
Joined
Nov 2, 2006
Messages
4,235
Likes
52
Points
0
Yona F. Maro

Yona F. Maro

R I P
Joined Nov 2, 2006
4,235 52 0
Hata kusoma ni kuchangia hata hicho ulichoandika wewe ni mchango ila unapotoa mchango angalia unachangia kwa faida ya nani yako mwenyewe ( ubinafsi ) au jukwaa zima ili hata mwandikaji nae aweze kujifunza pamoja na waangaliaje wengine hilo ni jambo muhimu sana la kuangalia - jioni njema
 
Prisoner

Prisoner

Senior Member
Joined
Jan 26, 2010
Messages
120
Likes
0
Points
0
Prisoner

Prisoner

Senior Member
Joined Jan 26, 2010
120 0 0
haya bishaneni mkimaliza semeni na sisi tuchangie
 
Yona F. Maro

Yona F. Maro

R I P
Joined
Nov 2, 2006
Messages
4,235
Likes
52
Points
0
Yona F. Maro

Yona F. Maro

R I P
Joined Nov 2, 2006
4,235 52 0
Kuna vitu vya kusoma tu sio lazima kila kitu uchangie au utoe maoni yako labda pale inapohitajika sana kurekebisha baadhi ya lugha ndani ya bandiko hilo lakini nazidi kusisitiza tunapotoa maoni yetu na marekebisho mengine tuangalie kama ni kwa faida ya wote au wachache na kama yanajenga au la tusishangae sasa watu waanze kutoka ndani ya jukwaa kuamua kwenda kwenye majukwaa mengine ambayo wanafikiri hawawezi kupata usumbufu wowote ule
 

Forum statistics

Threads 1,250,033
Members 481,189
Posts 29,718,777