Msherwa
JF-Expert Member
- Aug 4, 2012
- 1,323
- 1,230
Yani nmemshangaa kweli huyu mtu Mkuu, anajifnya kachukia, kilichimchukiza hpo ni kipi au kuambiwa ukweli.. ye angekuwa hyo ni mdogo wake anatendewa hyo anayomtendea mtoto wa watu angejisikiaje.. kweli kuna viumbe wazito duniani, mimi pia kaniharibia siku..!Mkuu umenisikitisha sana, hata mimi nakwambia hutumii akili, yani unakubali mpenzi wako mwenye matatizo ya miguu akuhudumie pasipo na msaada wako kweli inaingia akilini!!!? wewe ulipaswa kuwa mfariji kwake na mtu wa kwanza kumsaidia kutokana na hali yake, na ukimuacha nakuhakikishia utapata laana na NUKSI kubwa kuliko hiyo unayofikiri ni laana, Mungu sio wa mchezo mchezo.
Jaribu kufikiri ingekuwa wewe ndio umepata huo ulemavu halafu mkeo anasubiri umuandalie chakula na ulemavu wako bila kumsaidia, ungeendelea kumpenda?? lakini huyo binti pamoja na hali yake, tabia yako mbaya bado anakupenda. Mkuu narudia tena tumia akili kuamua na kufikiri. Kiukweli umeniharibia siku yangu kwa huo ukatili unaomfanyia huyo binti mlemavu.
Kwa namna anavyojieleza unywanywa wake atakuwa anacheka mpaka machozi hyu...Mkuu!Naomba nikuulize swali moja tu na unijibu ukweli. Ni hivi Katika kujiburuza buruza kwake wakati anapokuona kwa maana ya kukupokea au kukuandalia chakura wewe reaction yako ilikuwa inakuwaje na hasa mbele za nduguze.
Huenda ndivyo anavyodhani....Unadhani kuna mahusiano mepesi??
They say u never know what u have until u loose it...mkuu inaonekana huyo mwanamke kakupenda na wewe umelijua hilo, ndio maana unamsumbua,
mara kumuacha bila sababuu,mara kumrudia kwa kua amekubembeleza sana na kukulilia na kukuomba msamaha bila kosa lolote. anakusaidia,anakushauri anakuwezesha ukihitaji msaada.
wewe,uliyonayo kichwani ni nuksi pindi upatapo matatizo,kwani matatizo ya miguu yake nuksi ni wewe?!! mbona hajakuacha?!! Mara ndugu zake,kwani unahakika gani kua ndg zako wote wanampenda?!!
kiuhalisia hakuna balanced love,na nakuambia ukiendelea na hio tabia ya kumkasirikia pindi yanapotokea matatizo,ipo siku atachoka ataenda zake,hapo ndio utaelewa maana ya mema anayoyafanya juu yako. watu km huyo mwanamke hawpo duniani pengine amebaki huyo tu. ukitoka hapo utawakuta vyura wa mjini utatamani uzirudishe siku nyuma.
Habari ndugu zangu,
Ninakuja kwenu nikiwa na tatizo. Naomba mwenye ushauri wa kujenga anisaidie. Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 27. Nina msichana ambaye ninampenda sana naye sina shaka kuwa ananipenda sana. Toka nikiwa sina kazi, huyu msichana alikuwa bega kwa bega na mimi. Alijitoa sana kwangu. Na mpaka sasa nikiwa na shida, anakuwa mstari wa mbele kunisaidia.
Tatizo lililonifanya nije kwenu kuomba ushauri, ni juu ya ndugu zake. Huyu msichana ni mkubwa na ana ndugu zake watatu, wawili ni vijana mapacha ambao kwa sasa wana umri wa miaka 24.
Kuna kipindi huyu msichana aliwahi kupata matatizo ya mguu. Ni kipindi ambacho kiukweli aliumwa na bado ni kipindi ambacho nilikuwa nimepata kazi na bado nikamuacha. Hakuwa amenikosea bali niliwmona kama nuksi hivi, kwani nilifukuzwa kazi bila sababu za msingi nikiwa bado na huyu binti.
Bado alikuwa mstari wa mbele kunipa ushauri na kunisaidia hata kipesa. Nilipopata kazi nikaona ni kheri kumuacha. Huyu msichana alikuwa akilia kila siku. Aliugulia ugonjwa na bado akaugulia kuachwa nami.
Baada ya binti kuniomba msamaha sana hata kwa kutokuwa na kosa, nikamrudia kwani hata mimi bado nilimpenda.
Baada ya kumrudia binti, tukawa nae karibu. Hakuwa anaweza kutembea kipindi hicho lakini nilipoenda kumsalimia, alijiburuta chini ili kunipokea. Muda mwingine alijiburuta kunitengea chakula au hata kupika huku akitambaa.
Haya yote aliyafanya hata mbele za ndugu zake. Waliona upendo wa binti huyu kwangu. Ikafika kipindi anajilazimisha kunyanyuka kwa ajili yangu. Kumbe akifanya hivyo, anakuwa akijiumiza.
Baada ya kuona hayo, kaka zake wakaanza kunichukia. Mmoja aliniita na kunishutumu kwa maneno makali sana. Kusema ukweli sikupendezwa na kauli zake kwasababu ilikuwa ni kama amenidharau. alinitamkia kuwa situmii akili kabisa.
Ndugu wana jamii, kauli hiyo imeniudhi na hata msichana mwenyewe akinipigia simu nakasirika sana. Natamani kumuacha sababu naogopa kama hivi tu tumeanza kugombana hapo baadaye je, itakuwaje? Sina amani ninapokuwa na msichana huyu. Amenililia sana, ameniomba msamaha sana ila mim moyoni mwangu nina kinyongo kutokana na hizo shutuma.
Ndugu wana jamii, nitakuwa nimekosea kumuacha huyu msichana kweli? Kama ungekuwa wewe ungefanya nini?
Naombeni ushauri wenu.
Hii uzi naona watu wamekomentiHabari ndugu zangu,