Je, nimuache huyu msichana?

Dec 13, 2015
21
2
Habari ndugu zangu,

Ninakuja kwenu nikiwa na tatizo. Naomba mwenye ushauri wa kujenga anisaidie. Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 27. Nina msichana ambaye ninampenda sana naye sina shaka kuwa ananipenda sana. Toka nikiwa sina kazi, huyu msichana alikuwa bega kwa bega na mimi. Alijitoa sana kwangu. Na mpaka sasa nikiwa na shida, anakuwa mstari wa mbele kunisaidia.

Tatizo lililonifanya nije kwenu kuomba ushauri, ni juu ya ndugu zake. Huyu msichana ni mkubwa na ana ndugu zake watatu, wawili ni vijana mapacha ambao kwa sasa wana umri wa miaka 24.

Kuna kipindi huyu msichana aliwahi kupata matatizo ya mguu. Ni kipindi ambacho kiukweli aliumwa na bado ni kipindi ambacho nilikuwa nimepata kazi na bado nikamuacha. Hakuwa amenikosea bali niliwmona kama nuksi hivi, kwani nilifukuzwa kazi bila sababu za msingi nikiwa bado na huyu binti.

Bado alikuwa mstari wa mbele kunipa ushauri na kunisaidia hata kipesa. Nilipopata kazi nikaona ni kheri kumuacha. Huyu msichana alikuwa akilia kila siku. Aliugulia ugonjwa na bado akaugulia kuachwa nami.

Baada ya binti kuniomba msamaha sana hata kwa kutokuwa na kosa, nikamrudia kwani hata mimi bado nilimpenda.

Baada ya kumrudia binti, tukawa nae karibu. Hakuwa anaweza kutembea kipindi hicho lakini nilipoenda kumsalimia, alijiburuta chini ili kunipokea. Muda mwingine alijiburuta kunitengea chakula au hata kupika huku akitambaa.

Haya yote aliyafanya hata mbele za ndugu zake. Waliona upendo wa binti huyu kwangu. Ikafika kipindi anajilazimisha kunyanyuka kwa ajili yangu. Kumbe akifanya hivyo, anakuwa akijiumiza.

Baada ya kuona hayo, kaka zake wakaanza kunichukia. Mmoja aliniita na kunishutumu kwa maneno makali sana. Kusema ukweli sikupendezwa na kauli zake kwasababu ilikuwa ni kama amenidharau. alinitamkia kuwa situmii akili kabisa.

Ndugu wana jamii, kauli hiyo imeniudhi na hata msichana mwenyewe akinipigia simu nakasirika sana. Natamani kumuacha sababu naogopa kama hivi tu tumeanza kugombana hapo baadaye je, itakuwaje? Sina amani ninapokuwa na msichana huyu. Amenililia sana, ameniomba msamaha sana ila mim moyoni mwangu nina kinyongo kutokana na hizo shutuma.

Ndugu wana jamii, nitakuwa nimekosea kumuacha huyu msichana kweli? Kama ungekuwa wewe ungefanya nini?

Naombeni ushauri wenu.
 
Ulirudiana na nuksi?

Acheni kuwabebesha mizigo yenu wanawake

Hakuna mtu ana nuksi.

Kwani kuna sheria inakulazimu uwe naye?

TAFUTA ASIYE NA NUKSI!

ila NUKSI sio tabia ya mtu

Nuksi ni kama hukutimiza wajibu wako na unatafuta wa kumlaumu.

MKIPATA KAZI MNAWAITA DADA ZETU NUKSI.

MKIFUKUZWA KAZI MTAWAITAJE?
 
sasa wewe unashauri au unafoka!
 
Hujafa hujaumbika ndugu yangu!kama unapendwa pendeka,wewe unakiri unapendwa sasa ndugu zake wametoka wapi?umefanyiwa mangapi mazuri na huyo binti umlipe malipo hayo?Usiwe naye kwa kumuhurumia hata siku moja,kama unampenda go for her no matter what,na usimuache kwa kisingizio cha ugonjwa hujui sekunde ijayo itakuwaje upande wako!
 
Hauna mapenzi ya dhati kwa huyo dada kijana.
Mtu anaumwa na kujiburuza chini kuja kukupokea na kukupikia wewe unaona ni sifa na upendo kweli???
Tena unasema kwa kujiamini kabisaa, ni mwanaume lakini sio mwanaume bora au kwa kidhungu wewe sio gentlemen.
Ushauri wangu usimpotezee ni vyema kumuacha sasa kuliko kuendelea kuwa nae kama huna furaha naye tena.
Anaweza kukulaumu kwa sasa ila mbeleni huko atakuja Ikuelewa na kushukuru pia, unavyoendelea nae unazidi kumpotezea muda wake na wako pia.

Kuwa na siku njema,
nikikukwaza niwie radhi saanaaaa.
 
sasa wewe unashauri au unafoka!

mkuu, kijana unapofika umri wa kuanza kuishi na mtu ndani halafu una fikra kama za huyu, NI WA KUKEMEWA KWA NGUVU ZOTE

Unadhani wanahitaji muujiza hawa kutengeneza yatima?

Au watahitaji msaada wa jf kutengeneza watoto wa mtaani?

Ni kukemea tu tabia ya watu wachache kudhani matatizo waliumbiwa kina fulani tu
 
Mkuu umenisikitisha sana, hata mimi nakwambia hutumii akili, yani unakubali mpenzi wako mwenye matatizo ya miguu akuhudumie pasipo na msaada wako kweli inaingia akilini!!!? wewe ulipaswa kuwa mfariji kwake na mtu wa kwanza kumsaidia kutokana na hali yake, na ukimuacha nakuhakikishia utapata laana na NUKSI kubwa kuliko hiyo unayofikiri ni laana, Mungu sio wa mchezo mchezo.
Jaribu kufikiri ingekuwa wewe ndio umepata huo ulemavu halafu mkeo anasubiri umuandalie chakula na ulemavu wako bila kumsaidia, ungeendelea kumpenda?? lakini huyo binti pamoja na hali yake, tabia yako mbaya bado anakupenda. Mkuu narudia tena tumia akili kuamua na kufikiri. Kiukweli umeniharibia siku yangu kwa huo ukatili unaomfanyia huyo binti mlemavu.
 
Hauna mapenzi ya dhati kwa huyo dada kijana.
Mtu anaumwa na kujiburuza chini kuja kukupokea na kukupikia wewe unaona ni sifa na upendo kweli???
Tena unasema kwa kujiamini kabisaa, ni mwanaume lakini sio mwanaume bora au kwa kidhungu wewe sio gentlemen.
Ushauri wangu usimpotezee ni vyema kumuacha sasa kuliko kuendelea kuwa nae kama huna furaha naye tena.
Anaweza kukulaumu kwa sasa ila mbeleni huko atakuja Ikuelewa na kushukuru pia, unavyoendelea nae unazidi kumpotezea muda wake na wako pia.

Kuwa na siku njema,
nikikukwaza niwie radhi saanaaaa.
Kweli kabisa mkuu, na huyu jamaa ipo siku atakua na ulemavu zaidi ya huyo binti na yatamfika makubwa ambayo hayatasimulika.
 
Mkuu umenisikitisha sana, hata mimi nakwambia hutumii akili, yani unakubali mpenzi wako mwenye matatizo ya miguu akuhudumie pasipo na msaada wako kweli inaingia akilini!!!? wewe ulipaswa kuwa mfariji kwake na mtu wa kwanza kumsaidia kutokana na hali yake, na ukimuacha nakuhakikishia utapata laana na NUKSI kubwa kuliko hiyo unayofikiri ni laana, Mungu sio wa mchezo mchezo.
Jaribu kufikiri ingekuwa wewe ndio umepata huo ulemavu halafu mkeo anasubiri umuandalie chakula na ulemavu wako bila kumsaidia, ungeendelea kumpenda?? lakini huyo binti pamoja na hali yake, tabia yako mbaya bado anakupenda. Mkuu narudia tena tumia akili kuamua na kufikiri. Kiukweli umeniharibia siku yangu kwa huo ukatili unaomfanyia huyo binti mlemavu.
ila mpaka anamtengea chakula unahisi ni upendo gani jamaa anaonyeshwa mkuu... huyu jamaa anahitaji counselling....
 
Itakua huyo dada yuko njema mfukoni ndo mana inakua ngumu kumuacha
Huyu binti hana kazi. Kipindi hajaugua alikuwa akifanya kibarua tu. Pesa aliyojitolea kwangu si kubwa ila ukubwa wake ni kule kujinyima yeye na akanipa mimi. Msema ukweli ni mtu wa Mungu.
 
kaka ake wanakwambia hutumii akaili kwa sababu yule ni mgonjwa kwa nini usinewambia asiandae chakula au umwambie nitakuja tupike wote huku ukichukua part kubwa ya kupika .. mkuu kama huwezi kuja kumuoa ni beter ukajisepea kimya kimya kiana japo maradhi hayana mtu usijisahahu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom