Je, nimuache huyu msichana?

Je, nimuache huyu msichana?

Hujafa hujaumbika ndugu yangu!kama unapendwa pendeka,wewe unakiri unapendwa sasa ndugu zake wametoka wapi?umefanyiwa mangapi mazuri na huyo binti umlipe malipo hayo?Usiwe naye kwa kumuhurumia hata siku moja,kama unampenda go for her no matter what,na usimuache kwa kisingizio cha ugonjwa hujui sekunde ijayo itakuwaje upande wako!
Kweli mkuu huyu hana kabisa sababu ya msingi ya kumuacha huyu binti kwani amekiri mwenyewe huyu binti anampenda anamsaidia kwa hali na Mali sasa sijui anataka nini tena
 
Hapo ndipo ninapoona tofauti ya mapenzi ya wazungu na waafrika, ingetokea uzunguni hiyo huyo mzungu angemuoa huyo binti wakati huo kwa kuonesha upendo wake kwake na ndio maana wengi wanafunga ndoa na wapenzi wao waliopo kitandani ambao mara nyingine unakuta mwanamke ana stage 4 cancer, lakini kibongo bongo kuugua ndio kwanza inakuaga sababu ya kuachana, Tujifunze kupenda kutoka moyoni bila kuangalia uzima wa mtu, sisi ni wa mwenyezi mungu na kwake tutarejea tusiishi kama tutadumu milele, nakushauri hivi, usiende tu kwa huyo dada hiki ndio kipindi cha kupeleka posa, kwanza uzinzi ni zambi kwa dini zote
 
Hauna mapenzi ya dhati kwa huyo dada kijana.
Mtu anaumwa na kujiburuza chini kuja kukupokea na kukupikia wewe unaona ni sifa na upendo kweli???
Tena unasema kwa kujiamini kabisaa, ni mwanaume lakini sio mwanaume bora au kwa kidhungu wewe sio gentlemen.
Ushauri wangu usimpotezee ni vyema kumuacha sasa kuliko kuendelea kuwa nae kama huna furaha naye tena.
Anaweza kukulaumu kwa sasa ila mbeleni huko atakuja Ikuelewa na kushukuru pia, unavyoendelea nae unazidi kumpotezea muda wake na wako pia.

Kuwa na siku njema,
nikikukwaza niwie radhi saanaaaa.
Well said.huyu jamaa ni shetani kabsa nazani.
 
Mkuu umenisikitisha sana, hata mimi nakwambia hutumii akili, yani unakubali mpenzi wako mwenye matatizo ya miguu akuhudumie pasipo na msaada wako kweli inaingia akilini!!!? wewe ulipaswa kuwa mfariji kwake na mtu wa kwanza kumsaidia kutokana na hali yake, na ukimuacha nakuhakikishia utapata laana na NUKSI kubwa kuliko hiyo unayofikiri ni laana, Mungu sio wa mchezo mchezo.
Jaribu kufikiri ingekuwa wewe ndio umepata huo ulemavu halafu mkeo anasubiri umuandalie chakula na ulemavu wako bila kumsaidia, ungeendelea kumpenda?? lakini huyo binti pamoja na hali yake, tabia yako mbaya bado anakupenda. Mkuu narudia tena tumia akili kuamua na kufikiri. Kiukweli umeniharibia siku yangu kwa huo ukatili unaomfanyia huyo binti mlemavu.
Kwakweli hata mimi kaniudhi sana nabaki najiuliza sijui wanaume wanataka nini kwa wanawake!!?
 
Kwakweli hata mimi kaniudhi sana nabaki najiuliza sijui wanaume wanataka nini kwa wanawake!!?
Huyu anataka laana, furaha kubwa maishani ni kupendana na mpenzi/mke/mume wako katika shida na raha, upendo hufanya mtu hata akiumwa ajione mzima, hata awe katika matatizo makubwa vipi lakini ukipata upendo unaona kama tatizo dogo tu.
 
Huyu binti hana kazi. Kipindi hajaugua alikuwa akifanya kibarua tu. Pesa aliyojitolea kwangu si kubwa ila ukubwa wake ni kule kujinyima yeye na akanipa mimi. Msema ukweli ni mtu wa Mungu.
Sasa nikuulize wewe hasa unachotaka nini au unataka mwanamke gani? Kumbuka " UNACHOKITUPA KWA DHARAU WENZIO WATAKIOKOTA KWA FURAHA" na ukumbuke kuwa " NGUO YA ZAMANI NDIO DEKIO JIPYA" huna akili kabisa laana itakupata kwa hayo machozi ya huyo binti halafu utatafuta wachawi fyuuuuuuu
 
Sijaona sababu ya kumuacha,na kuhusu hao ndugu wameona dada yao anaumwa na anakuhudumia ww wanaona huruma kuwa anajiumiza kwa ajili yako na ww humkatazi
NB😀amu ni nzito kuliko maji
 
Hapo ndipo ninapoona tofauti ya mapenzi ya wazungu na waafrika, ingetokea uzunguni hiyo huyo mzungu angemuoa huyo binti wakati huo kwa kuonesha upendo wake kwake na ndio maana wengi wanafunga ndoa na wapenzi wao waliopo kitandani ambao mara nyingine unakuta mwanamke ana stage 4 cancer, lakini kibongo bongo kuugua ndio kwanza inakuaga sababu ya kuachana, Tujifunze kupenda kutoka moyoni bila kuangalia uzima wa mtu, sisi ni wa mwenyezi mungu na kwake tutarejea tusiishi kama tutadumu milele, nakushauri hivi, usiende tu kwa huyo dada hiki ndio kipindi cha kupeleka posa, kwanza uzinzi ni zambi kwa dini zote
Punguza kuangalia tamthilia dada
 
Kwanza ungekua muungwana wala usingethubutu hata kuuliza ungeona aibu et "JE NIMUACHE HUYU MSICHANA? Huna haya wala huruma katili mkubwa wewe subiri laana zako.
 
Ndugu usifanye kosa kama hilo, unakili amekusaidia kwenye shida na raha hadi umepata kazi.
Mbona sasa wewe unashindwa kuwa imara kwenye shida inayomuhusu.
Usimuumize kwa sababu ya ndugu zake.
Tafadhali rudi kwake haraka ndugu huo ni ukatili kama ukatili mwingine.
 
Habari ndugu zangu,

Ninakuja kwenu nikiwa na tatizo. Naomba mwenye ushauri wa kujenga anisaidie. Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 27. Nina msichana ambaye ninampenda sana naye sina shaka kuwa ananipenda sana. Toka nikiwa sina kazi, huyu msichana alikuwa bega kwa bega na mimi. Alijitoa sana kwangu. Na mpaka sasa nikiwa na shida, anakuwa mstari wa mbele kunisaidia.

Tatizo lililonifanya nije kwenu kuomba ushauri, ni juu ya ndugu zake. Huyu msichana ni mkubwa na ana ndugu zake watatu, wawili ni vijana mapacha ambao kwa sasa wana umri wa miaka 24.

Kuna kipindi huyu msichana aliwahi kupata matatizo ya mguu. Ni kipindi ambacho kiukweli aliumwa na bado ni kipindi ambacho nilikuwa nimepata kazi na bado nikamuacha. Hakuwa amenikosea bali niliwmona kama nuksi hivi, kwani nilifukuzwa kazi bila sababu za msingi nikiwa bado na huyu binti.

Bado alikuwa mstari wa mbele kunipa ushauri na kunisaidia hata kipesa. Nilipopata kazi nikaona ni kheri kumuacha. Huyu msichana alikuwa akilia kila siku. Aliugulia ugonjwa na bado akaugulia kuachwa nami.

Baada ya binti kuniomba msamaha sana hata kwa kutokuwa na kosa, nikamrudia kwani hata mimi bado nilimpenda.

Baada ya kumrudia binti, tukawa nae karibu. Hakuwa anaweza kutembea kipindi hicho lakini nilipoenda kumsalimia, alijiburuta chini ili kunipokea. Muda mwingine alijiburuta kunitengea chakula au hata kupika huku akitambaa.

Haya yote aliyafanya hata mbele za ndugu zake. Waliona upendo wa binti huyu kwangu. Ikafika kipindi anajilazimisha kunyanyuka kwa ajili yangu. Kumbe akifanya hivyo, anakuwa akijiumiza.

Baada ya kuona hayo, kaka zake wakaanza kunichukia. Mmoja aliniita na kunishutumu kwa maneno makali sana. Kusema ukweli sikupendezwa na kauli zake kwasababu ilikuwa ni kama amenidharau. alinitamkia kuwa situmii akili kabisa.

Ndugu wana jamii, kauli hiyo imeniudhi na hata msichana mwenyewe akinipigia simu nakasirika sana. Natamani kumuacha sababu naogopa kama hivi tu tumeanza kugombana hapo baadaye je, itakuwaje? Sina amani ninapokuwa na msichana huyu. Amenililia sana, ameniomba msamaha sana ila mim moyoni mwangu nina kinyongo kutokana na hizo shutuma.

Ndugu wana jamii, nitakuwa nimekosea kumuacha huyu msichana kweli? Kama ungekuwa wewe ungefanya nini?

Naombeni ushauri wenu.
Mbona yy alikusaport why u. hata utakayeoa hutapata aman inaonesha unapenda ukiwa na shida.
 
Back
Top Bottom