Je, nimuache huyu msichana?

Je, nimuache huyu msichana?

Ulichokifanya ni kitendo cha kinyama sana. Muda wote huo yeye anakuonyesha upendo wa dhati. Hujali. Leo unaweza kusimama kwa miguu yako, badala ya kurudisha fadhila, unakuwa mtu wa kwanza kumjeruhi moyo wake. Tuseme ulimtamani au ulimfata ili umtese? Subiri nuksi lako litakalokupata. Litakua kubwa kuliko kufukuzwa kazi.
 
Habari ndugu zangu,

Ninakuja kwenu nikiwa na tatizo. Naomba mwenye ushauri wa kujenga anisaidie. Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 27. Nina msichana ambaye ninampenda sana naye sina shaka kuwa ananipenda sana. Toka nikiwa sina kazi, huyu msichana alikuwa bega kwa bega na mimi. Alijitoa sana kwangu. Na mpaka sasa nikiwa na shida, anakuwa mstari wa mbele kunisaidia.

Tatizo lililonifanya nije kwenu kuomba ushauri, ni juu ya ndugu zake. Huyu msichana ni mkubwa na ana ndugu zake watatu, wawili ni vijana mapacha ambao kwa sasa wana umri wa miaka 24.

Kuna kipindi huyu msichana aliwahi kupata matatizo ya mguu. Ni kipindi ambacho kiukweli aliumwa na bado ni kipindi ambacho nilikuwa nimepata kazi na bado nikamuacha. Hakuwa amenikosea bali niliwmona kama nuksi hivi, kwani nilifukuzwa kazi bila sababu za msingi nikiwa bado na huyu binti.

Bado alikuwa mstari wa mbele kunipa ushauri na kunisaidia hata kipesa. Nilipopata kazi nikaona ni kheri kumuacha. Huyu msichana alikuwa akilia kila siku. Aliugulia ugonjwa na bado akaugulia kuachwa nami.

Baada ya binti kuniomba msamaha sana hata kwa kutokuwa na kosa, nikamrudia kwani hata mimi bado nilimpenda.

Baada ya kumrudia binti, tukawa nae karibu. Hakuwa anaweza kutembea kipindi hicho lakini nilipoenda kumsalimia, alijiburuta chini ili kunipokea. Muda mwingine alijiburuta kunitengea chakula au hata kupika huku akitambaa.

Haya yote aliyafanya hata mbele za ndugu zake. Waliona upendo wa binti huyu kwangu. Ikafika kipindi anajilazimisha kunyanyuka kwa ajili yangu. Kumbe akifanya hivyo, anakuwa akijiumiza.

Baada ya kuona hayo, kaka zake wakaanza kunichukia. Mmoja aliniita na kunishutumu kwa maneno makali sana. Kusema ukweli sikupendezwa na kauli zake kwasababu ilikuwa ni kama amenidharau. alinitamkia kuwa situmii akili kabisa.

Ndugu wana jamii, kauli hiyo imeniudhi na hata msichana mwenyewe akinipigia simu nakasirika sana. Natamani kumuacha sababu naogopa kama hivi tu tumeanza kugombana hapo baadaye je, itakuwaje? Sina amani ninapokuwa na msichana huyu. Amenililia sana, ameniomba msamaha sana ila mim moyoni mwangu nina kinyongo kutokana na hizo shutuma.

Ndugu wana jamii, nitakuwa nimekosea kumuacha huyu msichana kweli? Kama ungekuwa wewe ungefanya nini?

Naombeni ushauri wenu.

Matatizo kipimo... umejaribu kusaidia hata wa kibinadamu kutafuta msaada wa tiba? au mzee ndo usha kuwa Marioo kwa binti wa watu..
 
Usitafute sababu ya kumuacha kisa umeambiwa na shemeji huna akili angalia mapenzi yake kwako acha kumuumiza mwenzio kuhusu nuksi je kama ww ndio mwenye nuksi kwa sababu alipo anza mahusiano na ww anaumwa miguu
 
Kweli binadamu tumeumbiwa kusahau tulikotoka,roho imeniuma km Huyo Dada ndo Mimi.kweli mpenz wako anaumwa miguu anajiburuta kukupikia ,kukupokea upo tuu unamwangalia na bado unataka kumwacha, ni wazi kabisa humpendi kabisa huyo Dada bora umwache tuu kwa hiari tuu,Mungu atamsaidia atampata anayempenda kweli maana naona ww ulimtaman kwa sabbu alikuwa anajitoa kwako ulivokuwa huna kitu ,kwanza mpk umekuja kuomba ushaur hapa ushaamua kumwacha huna mapenzi nae....
 
Daaaah mtoa post wew s binadamu hufai kuwa na mpenz na hustahili
 
Back
Top Bottom