Je nifanye nini ili mpenzi wangu asiwe na wapenzi wengine? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je nifanye nini ili mpenzi wangu asiwe na wapenzi wengine?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Jpinduzi, Nov 5, 2011.

 1. Jpinduzi

  Jpinduzi Senior Member

  #1
  Nov 5, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mawasiliano ya karibu hufanya uelewe mawazo na matatizo ya mpenzi wako. Mwonyeshe na mthibitishie kwamba unampenda na huna mwingine zaidi yake. Hakikisha unakuwa muwazi na mkweli. Mkielewana vizuri mnaweza kusaidiana katika kutatua matatizo iwapo mmoja wenu atakuwa nayo. Kwa kufanya hivyo mtajenga moyo wa kuaminiana.

  Jitahidi usiwe na marafiki wengine. Utamfahamu vizuri rafiki yako iwapo mtazungumza kila mara kuhusu mipango ya uhusiano wenu, vitu anavyopendelea kufanya baada ya saa za kazi au masomo,watu anaowasiliana nao n.k
  .

  IWAPO HAMTAAMINIANA JIULIZE
  Kwa nini iwe hivyo. Je, inawezekana huyu mtu hanifai au mapenzi yangu ni kidogo kiasi ambacho siwezi kuzuia vishawishi vingine?
   
 2. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #2
  Nov 5, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Hayo yote uliyoyaeleza yanaweza yakawa yako hivyo.
  Tatizo likaja kwenye sita kwa sita Mkuu, mmoja anaridhika na mwingine anaachwa hewani. Hapo lazima kutakuwa na utata.

  Unamkuta mpenzi wako ni kama gari haina betri, kuwaka kwake mpaka kwenye mteremko mkali. Hii haijalishi ni mwanaume au mwanamke.
   
Loading...