Je, niachane na mapenzi kwa sasa?

dracular

JF-Expert Member
Dec 24, 2013
769
1,061
Habari ndugu wana JF,

Naamini ni wazima wa afya njema huku mkiendelea na majukumu yenu ya kila siku ya kutafuta mkate wa kila siku, bila kupoteza muda hebu twendeni kwenye maada kuu.

Mimi ni kijana wa kiume niliyehitimu chuo mwaka huu, wakati nimemaliza form six nilirudi mtaani na kuendelea na shughuli zangu ndogo ndogo huku nikisubiri matokeo yatoke niendelee na chuo.

Sasa pale mtaani kwetu kuna familia ilikuwa imehamia baada ya baba wa familia hiyo kuhamishiwa kikazi katika mkoa wetu, katika familia hiyo alikuwepo binti mmoja mzuri mweupe na mwenye umbo la kuvutia sana daaah! Alikuwa ni mzuri jamani.

Bahati nzuri yule baba mwenye familia aliulizia ni wapi atapata mwalimu wa kuwafundisha watoto wake akiwepo yule mkubwa ambae ndo yule binti mzuri kwani alikuwa kafeli mtihani wa mwaka uliopita na aliitaji kurudia ili asafishe chet. Watu walimuelekeza kwangu yule mzee na nikaanza kufanya majukumu yangu ya kiualimu kwa kuwafundisha watoto wake.

Sasa yule mkubwa kiukweli nilimpenda kimapenzi ila niliogopa kumtongoza maana kama angenikataa basi ingekuwa aibu kwangu mimi kama mwalimu then ningehatarisha kibarua changu hivo ikabidi niwe mpole tu lakini baadae nikasema siwezi kufa kwa kiu baharini nikajitosa kumtongoza chaajabu akasema ticha hata mimi nilikuwa nakupenda ila niliogopa kukwambia.

Daaah! Aisee yule binti alinipenda sana na alinipa kila kitu nilichotaka, nilifanyanae mapenzi mpaka nikamkinai na uzuri sikuuona tena maana nikitaka kula tunda nilikuwa napewa mpaka nashiba.

Kosa nililofanya kubwa baada ya kumtumia sana mtoto wa watu nilivyofika chuo nikapata msichana mwingine na yeye nikampotezea. Matokeo yamekuja kutoka binti kafeli tena na mimi sikushangaa maana muda mwingi wa kusoma tuliutumia kufanya ngono.

Na wala sikuumia sana kwani nilihisi ni ujinga wake binafsi. Shida ikawa kwa huyu mpenzi mpya ambae mwanzo nilimuona anafaa sana alikuja badilika akaanza kunifanyia visa kila siku, ikawa vurugu kila siku lakini hatimae huyu mpenzi mpya tukaachana japo alinikondesha mpaka mwili, maana alikuwa na tabia chafu sana na mimi nilimpenda kuliko maelezo lakini jitihada zangu za kumrudisha kwenye mstari sahihi zilishindikana,
Daaah alinifanya niisome namba kwa kiarabu.Huyu binti alienisumbua moyo nimedumu nae kwa miaka mitatu.

Sasa basi baada ya kuwa nimetendwa na nliempenda nikaamua kuwa tafuta wapenzi wangu wa zamani ili nisikose penzi, nilifanikiwa tena kumnasa yule mwanafunzi nilie mfelisha ila cha ajabu nilimkuta tayari amezaa mtoto ila wametengana na alie mpa hiyo mimba na bado kaonesha ananipenda sana na akanilaumu kuwa baada ya mimi kumuacha alijikuta anatafuta faraja ili kuondoa stress ndo kupata hiyo mimba na anadai hakuna mwanaume kama mimi hapa duniani.

Nacho hisi ni kwamba ile law of karma ilinitafuna baada ya mimi kumuumiza na kupata msichana mwingine kama uzi wa PATO3221 ulivoeleza. Sasa roho inaniuma sana na nikikumbuka alivonipendaga na mimi nikamfanyia maovu.

Jamani nifanyeje niachane na huyu binti kwa amani maana nahisi anataka kunipenda tena na mimi kwake nilifata msambwanda tu baada ya kuzinguana na yule kicheche wa kule chuo? Sitaki kumuumiza tena maana nimeshajua malipo ni hapahapa duniani.

Naombeni ushauri jamani sitaki matusi, nahitaji msaada wenu wa kimawazo ili nimuache kwa amani na tusiwe maadui ili na mimi niendelee kubarikiwa.
 
mkuu ushamfunua funua binti wa watu unamjua kuliko anavyojijua yeye then una break up

√√ukimuacha tena hata akikufanya msukule GOD will understand kabisa
 
Haya maneno dhahiri hii Hoja sio ya kuokota...

Mshika Mawili siku zote moja humponyoka...

Hata ukifanya kosa...

Ukaamua kuongopa...

Chagua moja...

Sio unajistukia unagota...

Kugangamala na kusota, ili kutoka...

Au kulala na kuota, kuwa unafoka...

Chagua moja...

Kuamua kungoja...

Au kutumia Kinga kwa kila Tendo moja...
 
Yaani mtu umemaliza chuo hujui kuandika HITIMU unaandika ITIMU
NIKAKIMAWAZO NILIVOFIKA???
UPUZI PELEKA FACEBOOK INAONEKANA HATA FORM 2 ULIFELI HALAFU UNATULETEA PROPAGANDA HAPA!.
Huwa kuna mistakes na errors ambazo hutokea mara kwa mara katika uandishi wowote ndo maana kuna segment ya kudelete.. Cha pili mimi sio mpuuzi ila wewe ndo mpuuzi unaedharau shida za watu wanapo omba ushauri.. Sometimes kukaa kimya ni bora kuliko kujifanya mjuaji wa kila kitu..
 
mkuu ushamfunua funua binti wa watu unamjua kuliko anavyojijua yeye then una break up

√√ukimuacha tena hata akikufanya msukule GOD will understand kabisa
Sio hivo mkuu mi nataka niachane nae kwa sababu tayari kaishazalishwa na mtu mwingine na mimi najiona sipo tayari kuishi na mtu aliezaaa tayari
 
tafuta hela dogo walembo hujileta wenyewe kama ndege anavonasa kwenye ulimbo.....................................mi kupiga mademu waliozaa naonaga shida....watoto wabichi kitaa wapo shazi unahangaika na wazee....inaonyesha ni jinsi gani ulivokosa SOUND
 
tafuta hela dogo walembo hujileta wenyewe kama ndege anavonasa kwenye ulimbo.....................................mi kupiga mademu waliozaa naonaga shida....watoto wabichi kitaa wapo shazi unahangaika na wazee....inaonyesha ni jinsi gani ulivokosa SOUND
Hapana mkuu sijakosa sound ila huyu binti aliwahi kuwa mpenzi wangu sa baada ya kuwa tumezingua na demu wangu nikaamua kurudiana nae but nimegundua amezaa tayari then naona kama anataka Ku fall in love kwa speed sana na mimi sina malengo nae sasa nahofia he nikiachana nae sitapata laana huko mbele ya safari??
 
Hapana mkuu sijakosa sound ila huyu binti aliwahi kuwa mpenzi wangu sa baada ya kuwa tumezingua na demu wangu nikaamua kurudiana nae but nimegundua amezaa tayari then naona kama anataka Ku fall in love kwa speed sana na mimi sina malengo nae sasa nahofia he nikiachana nae sitapata laana huko mbele ya safari??
laana kwani mzazi wako huyo...piga chini chukua watoto wazuri........ashazalishwa wa nini huyo.....
 
Mweleze dhamira yako, kuwa upo tu kupunguza uzito. Ataamua mwenyewe kama aendelee, au ajikatae.
Ahsante kwa ushauri ila nahisi roho yangu inauma sana na jinsi anavo nambia kwamba hata hiyo mimba aliipata kwa stress tu ila ananipenda sana na mungu kanirudisha tena kwake.. Hapo ndo nachanganyikiwa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom