Je, ni wangapi wasiotamani kupata watoto?

Je, ni wangapi wasiotamani kupata watoto?

Hujajibu swali.
Hakuna aliekukataza kuzaa.
Dunia imeshajaa.


Dunia ipi hiyo?

unajua dunia zaidi ya robo tabu bado haijakaliwa na watu?

Kama umewahi kuzunguka duniani, walau kwenda Ulaya huwezi ongea upuuzi kama huo. Dunia bado sana.
 
Hata mti usiozaa unaleta kivuli acha kuishi kiformula formula worry about your own seed si kulazimisha wengine kuleta watoto duniani wasiowataka. Mnaongea weeee lakini malezi hamsaidii , hela za matunzo hamtoi so why does your opinion matter??


Kuzaa ni jambo jingine na kulea ni jingine.
Unazungumza mambo mawili kama jambo moja. Wakati sio sahihi.

Asiyezaa anamakosa makubwa ikiwa anambegu na anauwezo wa kuzaa na alikuwa na muda wa kuishi.

Aliyezaa akashindwa kulea pia anamakosa lakini sio Makubwa kwani Mungu ndiye Mlezi.

Huitwa Mola Mlezi. Hata usipolelewa na wazazi wako utakua tuu. Lakini kama hukuzaliwa basi huwezi kuzaliwa.

kuzaliwa ni zaidi ya kulelewa.

Kuzaa ni kushiriki katika uumbaji, ni uungu.
 
Pamoja na gazeti lako reeefu ambalo sijalisoma, bado mtazamo wangu ni uleule...mimi napenda watoto lakini siwezi kuwa msemaji wa kila mwanamke aliyepo chini ya jua kwamba anapenda. Kila mtu ameumbwa na hisia zake, matamanio na akili zake. Hatuwezi kufanana hata siku moja
100% correct
 
Najua ndio, hakuna mtu amemkataza mtu kuzaa
Najua ndio, hakuna mtu amemkataza mtu kuzaa

Sasa mbona ukaniuliza kuwa nani kanikataza Kuzaa.

Hapa tunazungumzia watu wasiotamani Kuzaa wapo?

Jibu ni hapana.
Ikiwa MTU anaakili timamu.
ikiwa mtu anaafya timilifu.
Ikiwa mtu anambegu na uwezo wa Kuzaa.

Jibu ni ndio.
Ikiwa mtu hana akili timamu, Aidha anawendawazimu, au anaongozwa na viumbe wa roho chafu.
Ikiwa mimba zinatoka, hashiki mimba na matatizo ya uzazi kama hayo.
 
Dunia ipi hiyo?

unajua dunia zaidi ya robo tabu bado haijakaliwa na watu?

Kama umewahi kuzunguka duniani, walau kwenda Ulaya huwezi ongea upuuzi kama huo. Dunia bado sana.

Ungekuwa unanifahamu usingethubutu kuandika ulichoandika.
Dunia ina watu wengi kushinda idadi inayoweza kuhimili. Tukiendekeza kuzaliana hovyo tutapata majanga makubwa mno.
Jaribu kusoma nyaraka zilizochapishwa karne hii.
Biblia unayonukuu si kila mtu anaifuata kati ya binadamu billioni 7 duniani.
Akili za kukariri tu.
 
Hio ni defensive mechanism tu, huenda ana tatizi huyo, tena akina dada ndo wanaongoza kupenda watoto

Huyo anatatizo katika uzazi!!
 
Hio ni defensive mechanism tu, huenda ana tatizi huyo, tena akina dada ndo wanaongoza kupenda watoto

Huyo anatatizo katika uzazi!!

Sio kweli, jamii ina watu tofauti wenye mitazamo tofauti, ngoja nikupe mfano, kipindi covid imechanganyia marekani kuna ukurasa maarufu kwenye mtandao wa instagram unaitwa “The shade room” walipost kuuliza hivi; kama una mtoto mmoja na mume wote wameugua korona na kuna mashine moja ya ventilator utampa nani atumie? Kuna dada mmoja alijibu kuwa mi binafsi nitampa mume wangu atumie, nitajaribu kumuokoa mume na sio mtoto. Kiukweli ile kauli ni kali sana na wengine walimzodoa na wengine walimuunga mkono.

Nilimsoma yule dada nikagundua anampenda mume wake na anaweza kumchagua over mtoto wake, na kwenye account yake alikuwa amepost picha zake, za mumewe na za mtoto wao kusindikiza na caption kedekede, i came to realize that, to others watoto ni matokeo tu sio kitu kinachowapa msisimko wa maisha. Sijasema kuwa alivyoandika ndivyo alivyomaanisha kwa sababu mwisho wa siku hatuwezi kujua moyoni mwake, but again that shows ni namna gani dunia ina watu tofauti tofauti wenye mawazo tofauti na yako au yangu.
 
Na pia kuna watu wana watoto na wanajuta kuwa na hao watoto. Kuna wazazi wanafika mahali wanawakana watoto wao hawataki hata mtu ajue kama huyu ni mtoto wake!

Watu wengi wanazaa ili tu kuondoa ile "nuksi" ya kuonekana kwamba hawana uwezo wa kuzaa, na sio eti kwamba wanapenda watoto. Kuna watu ukiwaangalia unajua tu huyu hakutakiwa kua na mtoto.
[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
 
Una mawazo na misimamo kama yangu. Ningekuwa andaeitini kama wewe nakuhakikishia usingechomoa; na tungeishi maisha ya uhuru, furaha na amani sana - bila mikatale ya jamii na vifungo vya kimila [emoji2099][emoji2099][emoji2099][emoji2099][emoji2099][emoji2099][emoji2099][emoji2099][emoji2099][emoji2099]
Wacha we!
 
Sio kweli, jamii ina watu tofauti wenye mitazamo tofauti, ngoja nikupe mfano, kipindi covid imechanganyia marekani kuna ukurasa maarufu kwenye mtandao wa instagram unaitwa “The shade room” walipost kuuliza hivi; kama una mtoto mmoja na mume wote wameugua korona na kuna mashine moja ya ventilator utampa nani atumie? Kuna dada mmoja alijibu kuwa mi binafsi nitampa mume wangu atumie, nitajaribu kumuokoa mume na sio mtoto. Kiukweli ile kauli ni kali sana na wengine walimzodoa na wengine walimuunga mkono.

Nilimsoma yule dada nikagundua anampenda mume wake na anaweza kumchagua over mtoto wake, na kwenye account yake alikuwa amepost picha zake, za mumewe na za mtoto wao kusindikiza na caption kedekede, i came to realize that, to others watoto ni matokeo tu sio kitu kinachowapa msisimko wa maisha. Sijasema kuwa alivyoandika ndivyo alivyomaanisha kwa sababu mwisho wa siku hatuwezi kujua moyoni mwake, but again that shows ni namna gani dunia ina watu tofauti tofauti wenye mawazo tofauti na yako au yangu.
Yah ni kwel lakini
 
Back
Top Bottom