Je, ni wangapi wasiotamani kupata watoto?

Si kila mzungu ni mzima,,wengine ni wehu..sasa unapunguza uchafuzi wa mazingira kwa kutozaa watoto?,,lakini unagegeda kama kawaida.. Kama sio uchizi ni nn? Hivi watoto ni uchafu?huyo hana tofauti na yule jamaa aliyemshitaki MUNGU...
 
Aisee
 
Hivyo mkuu,,heshima ya mwanamke ndoa,,,hayo ya mtoto majaaliwa
Huo ni mtazamo wa jamii, anapewa heshima mwanamke aliyeolewa...hapa tunazungumzia kupenda. Kumbuka kuna mwanamke anaweza kuwa hapendi kuolewa ila akajikuta analazimika kuolewa kuepuka tu masimango. Nikupe mfano, dada yetu mkubwa hajawahi kuolewa na ni mtu anajiheshimu kabisa....huwa ananiambia mdogo wangu we olewa tu, hata kama unahisi ndoa si kitu muhimu kwako ukipata mtu olewa. Ni vizuri kuishi maisha unayopenda lakini jamii inayotuzunguka haimuelewi kabisa na haimuamini mwanamke asiye na mume.
Hapa sio kwamba ametambua kuwa anahitaji ndoa yeye binafsi, bali ameona jinsi jamii inavyomtazama.
Mama yangu pia aliyenisimamia ubatizo pia hajawahi kuolewa sasa hivi ana mvi na watu waliomuona tangu akiwa msichana wanadai kuna uwezekano mkubwa akawa ni bikra[emoji1787][emoji1787][emoji1787] mimi, anadai alipata pressure kutoka kwa watu akiwa binti ila baadae walimkubali na anapewa heshima yake kama binadamu yeyote.
Mimi nadhani kuna idadi kubwa ya watu wanaoshindwa kuishi maisha yao kwa sababu ya kushindwa kuhimili pressure kutoka kwa jamii zinazowazunguka lakini pia wapo manunda wanaoweza kutoboa katikati ya jamii hiyohiyo.
 

Ukimkuta mtu anajadili mtoto ni mzigo, sijuwi mimi nataka mmoja tu sijuwi kwanza bado kuzaa n.k kwa kupuuza jua huyo amekosa mfumo wa dini sahihi kumuongoza katika maisha yake.

Dini yetu ya kiislamu tukirejea kwa kiongozi wetu wa umma huu Mtume wetu, kipenzi chetu Nabii Muhammad S.A.W ametuhimiza kupata watoto ili siku ya malipo (kiama) apate kujifakharisha kwa umma wake kuwa na watu wengi.

Lakini hii kupata mtoto haimaniishi watoto wa nje ya ndoa kama wafanyavyo baadhi ya watu ama wakiristo kwa kuzaa bila ya ndoa hii haikubaliki, tunazungumzia watoto waliozaliwa ndani ya ndoa tena ya kiislamu.

Kuhusu kutokuzaa kwa sababu ya maisha hii si sahihi, mwanadamu yeyote anayezaliwa hapa ulimwenguni yupo kwenye dhamana ya Mungu (Allah) hakuna mtu wala kitu chochote kinachoweza kumpangia rizki huyu au yule hii kazi ni yake mwenyewe Muumba mbingu na Ardhi na vilivyomo.

Lakini hili la kwamba mtoto hatokufaa ukubwani pia si sahihi uislamu umefundisha malezi bora juu ya mtoto tokea anazaliwa anaacha kunyonya, mpaka anafika miaka saba nini afanye na hata baada ya hapo lengo ni kumjenga mtoto aje awe mtu mzuri katika maisha yake lakini pia kwa wazazi wake.

Lakini bahati mbaya mtoto anazaliwa mama ama baba anadumu kunywa ulevi ama club na mfano wa majanga kama haya usitegemee sana kupata mtoto ambaye unadhani atajakuwa yule ambaye leo unasema atakuja kukufaa lazima yule mtoto atainukia kwenye khulka ya malezi ya wazazi wake. Dini yetu ya kiislamu inazo darsa ndefu juu ya malezi bora ya watoto kwa kuja kuwafaa wazazi wao na jamii kwa ujumla.

Ndio mana nimesema ukimuona mtu anajadili vitu kama hivi huyo lazima atakuwa amekosa mfumo wa dini uliosahihi. Huyu dada wa 32years hajui ata alipo na hata anapokwenda

Salam Alykum.,
 
Si kila mzungu ni mzima,,wengine ni wehu..sasa unapunguza uchafuzi wa mazingira kwa kutozaa watoto?,,lakini unagegeda kama kawaida.. Kama sio uchizi ni nn? Hivi watoto ni uchafu?huyo hana tofauti na yule jamaa aliyemshitaki MUNGU...
Wapi nimetaja mzungu?

Mzungu ni nani?

Kipi kinamthibitisha huyu mzungu na huyu si mzungu?
 
Kwani mwanamke akiwa na pesa zake akisema hataki kuolewa wewe unapata shida gani?
 
Kuna link umenitumia ya childless _week pedia...ni research ya akina nani kama sio wazungu?hakuna mtu mweusi mwenye kusuport upuuzi huo
 
Kuna link umenitumia ya childless _week pedia...ni research ya akina nani kama sio wazungu?hakuna mtu mweusi mwenye kusuport upuuzi huo
Nimeuliza mzungu ni nani? Unajuaje huyu mzungu na huyu si mzungu?

Hujanijibu.
 
Mkuu lazima uelewe Kama mwanamke hataki kuolewa,,,hiyo ni hiari yake,, lakini hakuna mwanamke mwenye heshima kama mume wako hajulikani,,,,huwezi kupewa heshima kama kila siku upo na wanaume tofauti...elewa hata kama uta tafuta wanaume kwa kujificha,,,siku ukipata mimba bado inaonekana ulikuwa unafanya uzinzi .....wengine hufikia hata kuhisi ni aibu kubwa mimba isiyo na ndoa...
 
Kwani heshima lazima? Kwani kila mtu anataka heshima?

Wengine washaamua kwamba, kati ya kuishi wanavyotaka na kuheshimiwa na jamii, wao wanaona kitu muhimu ni kuishi wanavyotaka, si kuheshimiwa na jamii.

Sasa hao nao unataka kuwalazimisha waone kuheshimiwa na jamii ni kipaumbele zaidi ya kuishi wanavyotaka?

Vipi kama mtu yupo miaka kadhaa mbele ya jamii na kashaona jamii inekosea katika hili na like na itakuja kuelewa mambo miaka ishirini baadaye.

Akisema anataka kuonesha mfano kwa jamii, hajali kama ataonekana valuvalu.

Utataka naye aendekeze kuheshimiwa na jamii?

Albert Einstein angesema theories zake ni ngeni sana machoni oa dunia, akizitoa zitamvunjia heshima kwa jamii, leo tungeweza kurusha mawasiliano ya satellite na GPS kwa kutumia theories za Relativity za Einstein?

Kuendekeza sana kuangalia jamii inakuheshimu vipi kunadumaza maendeleo.

Kwa sababu, kika unapotaka kufanya kitu cha tofauti cha maendeleo, utaleta kitu kipya ambacho jamii haikielewi.

Sasa kama unaoenda sana heshima katika jamii, utaogopa kuleta kitu kipya, utabaki na mambo yale yale ya zamani tu.

Matokeo yake jamii nzima inadumaa.

Kuendekeza kuangalia jamii inakuheshimu vipi ni moja ya sababu jamii masikini zinabaki masikini.
 
Hao waliofanya research ni akina nani?
Kwanza jibu mzungu ni nani na unajuaje huyu mzungu na huyu si mzungu, halafu nitakujibu.

Hutakiwi kuwa unaruka maswali yangu halafu unategemea mimi nijibu yako.
 
Kwanza jibu mzungu ni nani na unajuaje huyu mzungu na huyu si mzungu, halafu nitakujibu.

Hutakiwi kuwa unaruka maswali yangu halafu unategemea mimi nijibu yako.
Hakuna mwafrika atakayeleta,,au kuprove research ya upuuzi huo,,,nimesoma hyo link na kwa 100% hao ni wazungu,..
 
Nadhani hata hujasoma nilichoandika
 
Hakuna mwafrika atakayeleta,,au kuprove research ya upuuzi huo,,,nimesoma hyo link na kwa 100% hao ni wazungu,..
Nimekuuliza mzungu ni nani na unajuaje huyu ni mzungu na huyu si mzungu?

Mpaka sasa hujajibu.

Inaonekna hata wewe unatumia tu hilo neno lakini huwezi kulifafanua maana yake.

Maana yake unaandika vitu usivyovijua.
 
Nimekuuliza mzungu ni nani na unajuaje huyu ni mzungu na huyu si mzungu?

Mpaka sasa hujajibu.

Inaonekna hata wewe unatumia tu hilo neno lakini huwezi kulifafanua maana yake.

Maana yake unaandika vitu usivyovijua.
Hivi kuna mtu asiyemjuwa mzungu?mzungu ni mtu MWEUPE..mwenye asili ya ulaya
 
Hivi kuna mtu asiyemjuwa mzungu?mzungu ni mtu MWEUPE..mwenye asili ya ulaya
Unaelewa kwamba watu wote wametokea Afrika na Ulaya walienda kutoka Afrika?

Sasa unaposema wenye asili ya Ulaya kutoka lini?

Na kwa nini uchukulie kutoka hapo na si kabla?
 
Ndiyo maisha aliyoyachagua, ukweli ni kwamba kuna baadhi ya Watoto wakishakuwa watu wazima wanasahau kuwasaidia Wazazi wao.
 
Mkuu mzungu ni mweupe mwenye asili ya ulaya. Hakuna aliyetoka Africa kwenda huko..ni hadithi za kusadukika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…