Je, ni vikwazo gani vinasababisha viwanda vya toothpicks kutokuendelea/kufanikiwa nchini Tanzania au Afrika Mashariki?

Masasati

New Member
Jul 16, 2013
3
3
Habari, wanajukwaa!

Ni muda mrefu nimekua nikifuatilia viwanda vidogo vya kutengeneza toothpicks Tanzania na hata Africa Mashariki ili kuona hatua na mafanikio katika kuanzishwa kwake na muendelezo wake. Naona vingi haviendelei kama ilivyo ilivyotarajiwa. Kuna kiwanda bora kabisa kilikuwepo Bagamoyo, leo hii hakizalishi tena, na vingine vingi tu.

Toothpicks zinatengenezwa kwa mianzi na wakati mwingine mbao/miti. Naomba tufahamishane kwa wenye uelewa juu ya jambo hili. Je, ni nini hasa changamoto katika uanzishwaji na uendelezaji wa viwanda hivi vya toothpicks? Wakati viwanda vya viberiti vinafanya vizuri tu sokoni japo kuna ushindani pia toka nchi jirani.

Tatizo ni nini?
Je, hatuna malighafi?
Je, ni sera za nchi?
Je, ni gharama kubwa za uzalishaji/uendeshaji?
Je, hakuna soko la uhakika?
Je, ni ubora hafifu wa bidhaa za ndani?
Je, tumezoea bidhaa za nje ya nchi zaidi kuliko ndani
N.k.

Ni nini kifanyike ili walio na mawazo ya kuanzisha viwanda vya toothpicks waweze kuzalisha kwa ufanisi na kudumu na kuendeleza viwanda hivi nchini?
Nawasilisha!
 
Sijajua ila wabanda vya chips siku hizi sioni toothpicks watu wananawa tu na kula kwa mikono,
Chakula kikiganda kwenye mianya ya meno wanatumia nini kutoa?Maana kazi kuu ya toothpick ni kutoa migando ya kilichokwama kwenye meno zaidi ya kutumika kama uma.
 
Back
Top Bottom