Je, ni utamaduni wetu kuongelea siasa kuliko Maendeleo binafsi?

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,609
8,749
Najiuliza tu na hii ni sehemu nyingi sana Duniani. Watanzania tukikutana sehemu yeyote tunaongelea siasa sana lakini cha ajabu ni vitu viwili muhimu kwenye maongezi mengi
1. Hatuongelea maendeleo binafsi ya kujiendeleza na cha ajabu maendeleo sisi tunaona kama ni mambo ya kibinafsi isipokuwa harusi na misiba

2. Pamoja na kuongea mambo mengi hatuchukui hatua hata kama za kisiasa. Ni vigumu kumuona Mtanzania analalamika waziwazi au ana simama kwa mambo ambayo anaamini kisiasa

Sasa nchi yetu ya vijana wengi sijui kama kuna mabadiliko siku hizi. Wahindi mfano wana matatizo mengi sana kama jamii lakini wanachanga hasa nje huku na wananunua hoteli au duka. Sisi hata ndugu wa damu hawataki hata kuongelea mambo kama ya kuchanga kibiashara! Najiuliza utamaduni nao unaturudisha nyuma?
 
Back
Top Bottom