CCM na Magenge Yenu Msitupotoshe: Uwekezaji Sio Siasa

MGOGOHALISI

JF-Expert Member
Apr 16, 2011
1,985
2,587
Moja kwa moja kwenye mada.

Ulipoanza mjadala kuhusu bandari waliopinga mkataba tuliambiwa wanapotosha. Mjadala haukuishia hapo wapingaji wakazidi kupata nguvu. CCM nao wakaanza ziara nchi nzima kutoa elimu kua mkataba hauna tatizo. Ajabu zaidi wakaanza kitudanganya waziwazi kuwa ule sio mkataba hadi kesi ya juzi mahakamani wote tukaongea lugha moja kuwa ni mkataba.

Baada ya CCM kuzunguka nchi nzima na kushindwa kuzima huu mjadala sasa wamekuja kutuambia tusichanganye dini na siasa. Lengo tu wapingaji waonekane ni wachache na wale wale wa kila siku. Hii haitafanikiwa nawaambia.

Sasa niwaulize CCM, mambo ya uwekezaji ni siasa? Pale bandarini kuna vyama au asasi za kisiasa? Pale bandarini mnaandikisha wanachama wa vyama vya siasa? Pale bandarini kuna msajili wa vyama au tume ya uchaguzi? Mnapotuambia tunaopinga mkataba wa uwekezaji wa DPW tunachanganya dini na siasa mnamaanisha nini?

CCM eleweni pale bandarini hakuna siasa. Ni utaalamu wa biashara ya uwekezaji. Uwekezaji ule hauhusu chama wala uchaguzi bali unahusu urithi wa asili wa watanzania. Watanzania wote wana haki ya kuujadili iwe kuukubali, kuupinga, kuurekebisha au kuukataa moja kwa moja. Bandari ni urithi wetu, bandari sio siasa na haitakuwa siasa.

Watanzania tutaendelea kujadili bandari popote pale. Iwe msikitini, kanisani, kazini, vijiwe vya kahawa, kwenye daladala na chooni tutajadili. Msitufanye sisi malofa bana.

Yaani anasimama mtu na heshima zake eti anataka tuamini bandari ni siasa. La hasha hatutakubali.

Tunachojua siasa inaweza kuingia popote ndio maana JPM kiongozi wa kisiasa alipelekewa hata malalamiko ya wenye ndoa. Lakini haimaanishi kila analofanya kiongozi wa kisiasa ni siasa.

CCM ndio wanufaika wakubwa wa udini. Hata sasa hivi wanalizungumza kama wanakemea lakini dhamira yao ni kulipotosha suala la bandari lionekane ni la kidini ili wapate nafasi ya kunyamazisha mjadala. Hamtawezaaaa.
 
Back
Top Bottom