Je, ni Speed gani kubwa zaidi ushawahi kutembea na gari au pikipiki?

BinSalum7

JF-Expert Member
Jan 26, 2019
1,678
3,732
Kwema wakuu, je ni speed gani kubwa zaidi ushawahi kutembea na gari au pikipiki na ilikuwa ni gari gani au pikipiki gani?

Nikianza mie nakumbuka mwaka 2017 nilikuwa na Cresta GX100 yenye engine ya 1jz turbo dashboard iliwahi kusoma 186 Kph (Dashboard ilikuwa ya digital) na ilikuwa ni sehemu inaitwa Samuye kuna down hivi kali kuitafuta Shinyanga. Nilikuwa na ndugu yangu alipiga kelele sana kuwa mwendo ni mkali ila nimuuliza tu "KWANI MIE NIPO NJE YA GARI?"

Pia nakumbuka kuna jamaa yangu alinunua pikipiki Kawasaki Ninja Z2 ina speed 260 nikasema ebu ngoja niitest , bwana wee, nikaingia Kilwa Road kuanzia pale Kurasini Mivinjeni kuelekea uhasibu T.I.A yani ile nimepiga gear ya kwanza hadi ya nne mafuta mengii naona chuma inasoma 190+. Weeee nilipunguza mwenyew bila kuambiwa.


Naombeni experience zenu wakuu kwenye masuala ya Speed.

RRONDO
Extrovert
Bavaria
JITU LA MIRABA MINNE

20210721_133115.jpg
 
Mkuu kipindi flani nilitafutaga Sana gari ya mkononi kwa mtu either cresta/ grande mark 2 yenye 1jz/2jz-gte lkn nilikosaga.

Ni gari Chache Sana zilibahatika kupata hio engine. Niliwahi kuendesha Verossa VR25 yenye 1jz-gte Nilikuwa namwaga Moto tu njia nzima.
 
Mkuu kipindi flani nilitafutaga Sana gari ya mkononi kwa mtu either cresta/ grande mark 2 yenye 1jz/2jz-gte lkn nilikosaga.Ni gari Chache Sana zilibahatika kupata hio engine.Niliwahi kuendesha Verossa VR25 yenye 1jz-gte Nilikua namwaga Moto tu njia nzima.
Acha kabisa mkuu, mie nilikuwa natembea sana na hiyo gari.... yaani ina jeuri haswaa, ila nilikuja kuiuza kwa jamaa fulani hivi traffic police mkoa wa Manyara.
 
Mleta mada mimi naomba niulize kitu..hio GX100 uliifanyia modification na kuweka hio turbo? Maana JZX100 ndo ina 1JZGTE...nirudi kwenye point mimi speed kubwa ni 170KPH Altezza 3SGE sehemu mbili moja ukiwa unaitafuta kitonga baada ya kuimaliza iringa sehemu ya pili ni mikumi mbugani hii siku niliiacha Range Rover..ya 2014..na sehemu ingine ukishamaliza mikumi kutafuta vijiji vya mangae/mangai😀😀😀
 
Mleta mada mimi naomba niulize kitu..hio GX100 uliifanyia modification na kuweka hio turbo? Maana JZX100 ndo ina 1JZGTE...nirudi kwenye point mimi speed kubwa ni 170KPH Altezza 3SGE sehemu mbili moja ukiwa unaitafuta kitonga baada ya kuimaliza iringa sehemu ya pili ni mikumi mbugani hii siku niliiacha Range Rover..ya 2014..na sehemu ingine ukishamaliza mikumi kutafuta vijiji vya mangae/mangai
Hapana mkuu, niliinunua hvo hvo ikiwa na Turbo yake na sio modification, tena nilikuwa na wazo la kununua 2jz-GTE niifunge humo ila tu ndio nikaiuza.
 
Hapana mkuu, niliinunua hvo hvo ikiwa na Turbo yake na sio modification, tena nilikuwa na wazo la kununua 2jz-GTE niifunge humo ila tu ndio nikaiuza.
Fresh mzee...kati ya engine za toyota alizotulia na kuzitengeneza vizuri ni
1. 2JZGTE -320 HP
2. 1JZ GTE-280 HP
3.3S-GTE - 260HP (Hapa itabidi ninunue Caldina yenye 3SGTE..fully body kit na BOV...😂😂😂
 
Back
Top Bottom