Je, ni sheria ipi mamlaka ya maji kuja kukukatia maji nyumbani na kuchukua meter bila mtu yeyote kuwepo?

Musoma Yetu

JF-Expert Member
Mar 11, 2016
2,625
2,000
Mada inajieleza.

Hivi kama unadaiwa bill, na bahati mbaya uko kwenye mchakato wa kulipa, ni sheria IPI inayowapa mamlaka ya maji kuja kukata maji na kuchukua mita bila mtu yeyote kuwepo na mita ipo ndani ya geti na mlango umefungwa!!!!

Hivi nikiwafungilia kosa la wizi au uvamizi ni kosa?
 
Semistocles

JF-Expert Member
Jul 2, 2016
1,940
2,000
Wakati unaunganishiwa maji ulipewa fomu yenye mkataba! Ndani ya mkataba kuna kipengele cha kukatiwa maji! Hebu Angalia vizuri hiyo fomu yako!
 
Musoma Yetu

JF-Expert Member
Mar 11, 2016
2,625
2,000
unaunganishiwa maji ulipewa fomu yenye mkataba! Ndani ya mkataba kuna kipengele cha kukatiwa maji! Hebu Angalia vizuri hiyo fomu yako
Sikupewa mkuu....!

Je , ni sawa kukata bila taarifa yeyote na mtu haupo? Yani unakuja nyumbani mita unakuta haipo, na uliacha umefunga geti la mlango, na kuna ukuta wa tofali kwenye fence
 
Semistocles

JF-Expert Member
Jul 2, 2016
1,940
2,000
Sikupewa mkuu....!

Je , ni sawa kukata bila taarifa yeyote na mtu haupo? Yani unakuja nyumbani mita unakuta haipo, na uliacha umefunga geti la mlango, na kuna ukuta wa tofali kwenye fence
Wana utaratibu wa kutoa notisi ya onyo ya mwezi mmoja kabla ya kukata maji kuhusu madeni yako! Ulipewa notisi? (kupitia simu au njia yoyote??)
 
Semistocles

JF-Expert Member
Jul 2, 2016
1,940
2,000
Sikupewa mkuu....!

Je , ni sawa kukata bila taarifa yeyote na mtu haupo? Yani unakuja nyumbani mita unakuta haipo, na uliacha umefunga geti la mlango, na kuna ukuta wa tofali kwenye fence
Sidhani kama ni sahihi kuvamia nyumba ya mtu kwa kuruka ukuta ili kung'oa mita ya maji! Vinginevyo, hii ni UVAMIZI (trespass)
 
Semistocles

JF-Expert Member
Jul 2, 2016
1,940
2,000
Sikupewa mkuu....!

Je , ni sawa kukata bila taarifa yeyote na mtu haupo? Yani unakuja nyumbani mita unakuta haipo, na uliacha umefunga geti la mlango, na kuna ukuta wa tofali kwenye fence
Haukupewa fomu ya kuunganishiwa maji? Kwanini? Hayo maji ni ya taasisi gani na kutoka mkoa gani?
 
balibabambonahi

JF-Expert Member
Apr 5, 2015
9,483
2,000
Sheria ya mikataba sura ya 345,2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho. Kama hujatimiza promise yako kuna remedies za upande mwingine.
 
jashmoe32

JF-Expert Member
Dec 4, 2012
1,077
1,500
Pole kwa yaliokukuta ila nna maswali mawili matatu ya kukuuliza, Je hapo kwako unaishi mwenyewe au na watu?Una uhakika kua hawakufunguliwa geti?(mind you may be unaeishi nae aliwafungulia geti ndio wakachukua kwa nguvu na kwa sababu unaeishi nae anajua kua wewe ni mkali au mkorofi ndio akaona better akudanganye kua hakuapo.

Mimi sio mwanasheria ila kama unaishi mweyewe then kwa jambo kama hili ningeenda Polisi kuripoti kuhusu hilo tukio na kuelezea kua nimeibiwa na vitu vingine kama mashine ya kukata majani na kusema hata kitasa cha mlango kimevunjwa (chochote) na nia ni kuwapa discipline kua nyumba ya mtu huwezi kuingia bila mhusika
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom