Je Ni sawa??

Toboamambo

Member
Sep 16, 2007
26
5
Kuwaruhusu wanafunzi waliokwisha jifungua(wamekuwa akina mama kufikia hapo)kujumuika na wanafunzi ambao bado hawajafikia kuwa wazazi kujichanganya na kusoma kwa pamoja inakuwa sawa???????????

MAONI:
Kwa mimi naona wanatuaribia wanetu kwani sio kama walivyokuwa mwanzo.Sasa ni wazazi na kuchanganywa na wanafunzi inakuwa sio sawa kabisa.

PENDEKEZO:
Nafikiri wafunguliwe shule ambazo wanasoma wazazi kivyao kwani kama ni ELIMU wataipata tuu,kwani hawakujua raha na kharaha zake wakiwa kwenye mambo hayo???
 
duh naona hujafanya hisabu vyema.

hii imetokana na kuwa wanafunzi wengi wanapoteleza na kupata ujazito wakiwa wanafunzi hufukuzwa shule. na kukosa haki yao ya msingi ya kielimu wakiwa na uwezo wa kusoma.


jengine kuwaacha mitaani ni hatari zaidi maana huenda si muda mrefu akaingia kwenye biashara ya ukahaba au kuwa anawagaia akina wale kwa kutafuta chochote.

na kusema tuwaanzishie skuli yao hilo ndio kosa zaidi moja tutawafanya wanafunzi wengi wapotee kwa kuamini kuwa kuna skuli yao, wakati wakirudi skuli wanazosoma hurudi na majuto na kujiona wamekosea na kujirekebisha.

jengine namba yao no ndogo kiasi haiwezeshi kujenga skuli zao peke yao.

kubwa ni kuwaelimisha kabla ya kuingia kwenye mtihani huo na kuendelea kuwaelimisha wanapoteleza.

ndio wajibu wetu wazazi kwa watoto wetu.


nnapendekeza mada hii ipelekwe kwenye mambo ya jamiii au elimu
 
Hujasema ni shule gani?za msingi,sekondari au vyuo vikuu?Sioni tatizo gani akina mama hao kusoma humo mchanganyikoni?Ni sawa kabisa wachanganywe tu ili hao wasiofungua tumbo wajue pia kuwa kumbe kufungua tumbo kupo ili wachague kusuka au kunyoa
 
MAONI:
Kwa mimi naona wanatuaribia wanetu kwani sio kama walivyokuwa mwanzo.Sasa ni wazazi na kuchanganywa na wanafunzi inakuwa sio sawa kabisa.

Lakini hawa wanafunzi unaokataa wasichanganyike na wazazi...si wanaishi na wazazi majumbani mwao? Kuna wazazi kilamahali...tuache wapate elimu,ila tujiulize tunawafanya nini wanaowapa mimba hawa watu,maana ni kuharibiana mifumo ya maisha.
 
Nafikiri katika zoezi hili wafuatilie na wanaowapa ujauzito ni kina nani kama ni wanafunzi wenzao nao pia si wazazi? basi wasichanganywe pia?, tusiangalie one side of the Coin
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom