Je, ni sawa Rais Magufuli aongezewe muda madarakani?

Je, ni sawa Rais Magufuli aongezewe muda madarakani?

Magufuli anafanya kazi kubwa sana ya kulinyoosha hili taifa toka kwenye utawala dhalimu wa ccm.

Tumpe muda zaidi wa kuweka mambo sawa.
Miaka mingine 5 inatosha sana, zaidi ya hapo hapana uongozi wakupokezana ni mzuri, hakuna mtu alitegemea kama MAGU angekuwa rais vivyo hivyo wapo na wengine wazuri atakapo achia yeye mwingine ataanzia hapo, naye ni binadamu
 
Wananchi wanataka Kikwete arudie tena urais ,ningewaona wa maana wabadilishe katiba si kumuongezea rais aliyepo bali hata wale waliopita waombe tena warudie,CCM watoe form za urais na kina kikwete nao waombe!!

hata kama ni hivi as long imetoka kwa wananchi na kura zao ndo zimetoa mwafaka, why not! na kwa hili la magufuli wacha wamamchi waseme wenyewe, kura ndo ztaongea
 
Ndugu yote uliyoandika ni sahihi sana. Ndugai hakustahili kuwa spika kabisa, ni mvunjifu wa katiba, amekuwa dhaifu sana kiasi kwamba badala ya bunge kuisimamia serikali, serikali ndiyo inalisimamia bunge kwa mkono wa chuma. Yaani Nyerere angefufuka akaona mambo ya hovyo anayofanya spika huyu na wabunge wake wa ccm angeomba arudi alikotoka.
 
HIVI WEWE UNAJUA KWANINI UZI WAKO HAUJAPATA MCHANGIAJI HATA MMOJA TANGU UTUMWE SAA 7 MCHANA NA SASA NI SAA 12 JIONI?
Wewe hujitambui, huyo bwana kaandika uchambuzi wa kiwango cha juu na ni ukweli mtupu, nakushangaa ww umepost 0 hapa.
 
Wadau wameappreciate utendaji mzuri wa Rais Ila ni Imani yangu kwamba Rais ataendelea kushikilia msimamo wake wa kuzingatia takwa la muda lililowekwa kikatiba bila kuyumbishwa.
 
kumpta Rais mwengine mfano wa Dr.Magufuli itatuchukua miongo kadhaa.....ni afadhali atusogeze miaka mingi zaidi...maana nchi yetu ilitafunwa sana! na watafunaji wapo pembeni wana njaa ya kufa mtu wanatamani aondoke hata leo waendelee kuitafuna nchi hii, kamwe hatuwezi kukabidhi nchi yetu kwa waroho na walafi.
chini ya Magufuli nchi yetu iko salama sana, kamwe sinto poteza kura yangu mwezi october zaidi ya kumpa mtu mwaminifu Magufuli
Sababu wwe ni mnufaika, umeshawahi sikia Kange akisifu tena zile Tambo sababu anufaiki nazo
 
Hatutaki mambo ya kijingajinga, katiba iko wazi. Unawezaje kusema mtu aongezwe muda ktk nchi inayofanya uchaguzi kila baada ya miaka mitano.

Labda kama uchaguzi ni kiini macho tu na uhuni wa kutafutia pesa kwa wazungu. Mnakuwa na uhakika gani kuwa atashinda.
 
Faida za Mkulu kuendelea na madaraka ni ndogo kulinganisha na hasara! inafaa mjadala huu ufungwe haraka sababu ukiendelea utaamsha waliolala na utaleta mpasuko wa kidini ambao haujawahi kuonekana kwenye nchi hii tangu tupate uhuru!

wabongo ni watu walafi na wanafki mno Karl Marx anasema kila kauli na kitendo cha mwanadamu ndani yake kuna maslahi! wabunge wa kijani wameamua kazi yao sasa ni kulinda maslahi yao tu kwa kumsifia Mkulu kwenye majukwaa na kumpinga na kumdharau wakimwita mshamba wanapoongea kwenye cm, ( refer Kinane na Napi) wabunge sasa kazi yao ni kumpaka Mkulu mafuta kwa mgongo wa chupa kumbe wanatetea tu matumbo yao! wabunge wamejisahau na kuwasahau wapiga kura wao na kudhani nchi ni mali yao shame on them! wabunge wanadhani wanaweza kuwaamulia wananchi lolote, kwa vile wananchi wako kimya . mimi ni kijani ila siungi mkono daima Mkulu kuvunja katiba na kusalia madarakani baada ya miaka kumi hata atujengee magorofa hewani! nchi inahitaji mtu mpya mwenye mawazo mapya kila siku!!

1. kukaa madarakani zaidi ni kupingana na mwasisi wetu Nyerere na utaratibu wa nchi miaka kumi ikiisha hatukuhitaji kukuabudu tena kafie mbele tuachie nchi yetu si urithi wa baba yako na kukaa zaidi kama Rais ni kuvunja katiba na kuzaa utamaduni mpya wa kidikteta hapa ataanza kukaa Magu ambae sote tunamkubali toka moyoni na kumsifu kwa nyimbo na mapambio , Magu atakaa miaka kumi tu ya kukurunzinza na atakaefuata atakaa hamsini hamtaweza kumtoa mwishowe atakuja atakaejiita Rais wa Maisha hamtakuwa na ubavu wa kumzuia atasema si mimi mlaumuni Magu , usidhani hawa wote kuanzia Magu watakaa madarakani zaidi kinyume na katiba kwa usalama bali vurugu inaweza kuibuka hata usiamini kama uko bongo hilo lilitokea Burundi mwaka 2015, vita yao haijaisha milele na milele Burundi ni kuviziana na kulipiziana kisasi tu kwanza ukiinyonga katiba na kujiongezea muda wa kusalia madarakani mwishoni unakufa ghafla reference ni Nkurunzinza!

2.Hapa ni hesabu tu yaani wabongo wengi akili haijai kijiko! kama Rais Mwinyi ambae pia tulimpenda angekaa miaka kumi zaidi na Mkapa ambae nae tulimpenda kumi zaidi na Mkwere alietufanya leo tuko nyumba zetu si za kupanga pesa kama yote tajiri wa roho yule nae kumi zaidi ina maana tungenunua Bombadia mwaka gani? na SGR ingekuja mwaka gani? yaani hesabu ndogo tu wabongo tunashindwa? ongeza miaka 30 mbele utapata Magu angeingia madarakani mwaka gani? na angekuwa na umri gani?na ungepata Stieglers in 2045! na Magu angeingia madarakani in 2045 akiwa Mzee!!!

3. hapa yaonekana watu wamechoka amani ya nchi hii sababu kuna sera isiyo wazi ya kupishana urais kati ya waislamu na wakristo na sasa baada ya Mkulu ni zamu ya waislam, vita ya waislam huwa si kuletea masihara sababu wao ni wengi zaidi nchini na wako tayari kufia dini yao wanapochokozwa si wa kuwapuuza kumuongezea muda Mkulu hapo mpaka utakuwa umevukwa na akianzisha sekeseke mmoja wao tu kuwa wameporwa nafasi yao ya urais balaa yake hakuna wa kuizuia, manake waislamu wa bara na wa visiwani wataungana nchi haitakalika na nchi inapaswa kulinda amani yake kwa kuwakemea wote wanaoleta mada ya kuongeza muda wa Mkulu ambae hakuna shaka ni Rais bora kuliko hata baba yetu kwa mawazo yangu!

4. Sote tunajua tabia ya wabongo ya kususa ukiwaibia haki yao na wakajua ! huku mtaani kwetu Songea m/kiti wa serikali za mitaa kang’ang’ania madaraka karudisha jina tena kwenye uchaguzi watu wamemchoka kaongoza muda mrefu watu hawakwenda kupiga kura na wanamkwepa mitaani! yawezekana mpango huo wa kumuongezea madaraka Mkulu ukawini na kusitokee vurugu yoyote kwa kuwa wabongo ni kunguru ni waoga wa virungu na mabomu ila hawatapiga kura kwa Mkulu kwa kipindi cha tatu na hawatampa ushirikiano, watu hawataenda kwenye mikutano yake ya hadhara na hawatacheka kwenye hotuba zake na watamwita Nkurunzinza na watamzomea kila atakapopita na umaarufu na thamani yake itashuka na nchi itapata shida sana kwa vikwazo itakavyowekewa na mashirika na nchi zinazoamini demokrasia, ikumbukwe mpango huu ni wa wabunge na matumbo yao si wa wananchi! atakuwa Nkurunzinza the second!!

5.Kimantiki anaweza kuwapo mzalendo mwingine kama Magu au kumzidi japo hajashika kijiti au hajazaliwa! nani alijua kama Magu ni kiboko cha wapinzani na wanaompinga na wavivu na wala rushwa na wanaokwamisha juhudi zake namna hii wakati akiwa nyapara wa barabara hatukudhani atosha urais kumbe ni kiboko sote tunalima kwa meno basi unaambiwa yupo ambae tutaamkia hata watoto wetu kama alivyofanya Makongoro wakati akigombea ubunge wa Africa mashariki! hiki ni chuma kweli ila vyuma vipo na vingine havijashika cheo huwezi kuvijua! nchi always ni kubwa kuliko mtu hata uvume vipi lazima upasuke nchi isonge!

Wachangiaji kama wewe wangekuwa 10 tuu JF naamini platform hii ingekuwa inapata sifa za kishindo. Asante sana

Umeweza kuanika ubora wake Mkulu, Mapungufu ya Mkulu uwezekano wa nini kinaweza kutokea iwapo Mkulu ataongezewa muda, uchambuzi bora kabisa,. Wengi waandika utumbo utumbo na inakua kama ndio uwezo wetu wa michango.

PENDEKEZO

Kiongozi Mzuri huzalisha taasisi nzuri na hata siku moja kiongozi lelege hawezi kuleta matokeo bora hata akisimamia taasisi bora.
Na mara zote viongozi wa hovyo wanapo simamia taasisi bora huwa wanapunguza ubora wa taasisi hizo wanazo zisimamia. MFANO NI TRUMP WA USA. Kama mimi kwa mapenzi yangu kwa nchi yangu na ufahamu nilio nao wa uboreshaji wa taaasisi ningependa Mkulu atawale miaka 15, kwa miaka hiyo mazuri mengi yataota mizizi. NI MCHANGO TUU.
 
hata kama ni hivi as long imetoka kwa wananchi na kura zao ndo zimetoa mwafaka, why not! na kwa hili la magufuli wacha wamamchi waseme wenyewe, kura ndo ztaongea
Hakuna mwananchi hata mmoja anayetaka rais aongezewe muda either wabunge washasoma mchezo kwamba aliyeko madarakani anataka kusifiwa(ili waendelee kuteuliwa kwenye kinyang'anyiro cha kugombea ubunge oct 2020) au "Mtu furani" mwenye ndio anayechagua wimbo wabunge wauuimbe huku yeye akiwa nyuma yao!
 
Hivi karibuni mbunge Kessy ametoa wazo juu ya Mhe.Raisi apate kuongezewa muda wa kukaa madarakani. Na Mhe.Spika ameridhia na kusema JPM atake asitake ataongezewa muda.

Kwa mujibu wa katiba yetu ya jamhuri wa muungano ya mwaka 1977, theluthi ya wabunge wakisema ndio basi muswada umepita. Na Kama tunavyojua wabunge wa CCM ni wengi bungeni, kwa namna nyingine huu muswada au hii hoja ikienda bungeni maanake imepita.

Swala si JPM aongezewe muda, swala Ni Tanzania inahitaji kiongozi Bora au taasisi Bora? Tanzania inahitaji taasisi imara au kiongozi imara? Tanzania inahitaji mifumo Bora ya Serikali endelevu au tunahitaji kiongozi Bora endelevu?

Kwanza tujue nchi yetu inahitaji Nini. Tukishajua inahitaji Nini itakuwa rahisi kufanya maamuzi yenye maslahi kitaifa. Tunahitaji maamuzi yenye maslahi kitaifa au maslahi ya chama?

Maslahi yenye tija na Bora kitaifa, Ni kubadili kikatiba Uhuru na utendaji Kazi wa mihimiri mikuu mitatu ya serikali Yani bunge, mahakama na serikali Yani Executive.

Wazo la bunge kutaka JPM aongezewe muda halina maslahi kitaifa Bali Lina maslahi ndani ya chama.

Ipate kufahimika wazi JPM ni binadamu nae atakufa, na akifa maanake uongozi wake thabiti umepotea. Ila tukiweka mifumo ya serikali thabiti na taasisi thabiti chini ya sheria thabiti, mifumo hi ya serikali itabaki miaka na miaka. Kuliko kumpachika mtu aendelee kuongoza eti tu kwa sababu Ni kiongozi mzuri na imara, hayo Ni mawazo ya makalioni.
Ashakumu si matusi.

Hitaji la Tanzania si kiongozi imara au benovelant dictator, hitaji la Tanzania Ni mifumo, taasisi na sheria imara na thabiti.

JPM kwa uimara wake inatupasa tumtumie ili kusimika taasisi hizi na mifumo hii. Na si kumuona Kama ndie kiongozi mteule miaka kumi au ishirini mbele au thelathini mbele.

Bunge linapaswa kwanza lipiganie Uhuru wake na sauti yake juu ya mhimili serikali (Executive) na si kupitisha wazo au muswada wa kumtaka JPM azidi kubaki madarakani.

Bunge la awamu ya tano Ni dhaifu Sana, Tena chini ya spika mdhaifu. Ndugai Has hajui ukubwa na uthamani wa chombo anachokiongoza.

Kisiasa naweza sema anapekeleshwa na mhimili serikali (executive), wakati Ndugai mhimili wake unapaswa kuwa mhimili mama na mlezi wa taasisi zote za serikali Sasa kwake imekuwa vice versa. Tumhenzi Sana marehemu Samwel Sitta.

Bunge pia lingepaswa kuandaa mifumo Bora ya kiutawala na mifumo ya kupata na kuandaa viongozi imara na thabiti Kama JPM, na si kusimamia mtazamo wa kwamba JPM aongezewe muda.

Je, JPM siku akifa maanake ndio hatupata raisi imara Kama yeye? Mazuri yote aliyofanya JPM ndio yatashindwa kuendelezwa? Alipo ishia JPM hapato endelezwa Tena?
Haya yote uliyosema hapa wanajua sana tu. Sema ndio hivyo wanalinda maslahi yao .
 
Hakuna mwananchi hata mmoja anayetaka rais aongezewe muda either wabunge washasoma mchezo kwamba aliyeko madarakani anataka kusifiwa(ili waendelee kuteuliwa kwenye kinyang'anyiro cha kugombea ubunge oct 2020) au "Mtu furani" mwenye ndio anayechagua wimbo wabunge wauuimbe huku yeye akiwa nyuma yao!

uko cdm nn? yaaani nmetoka kusema apo sasa hv kwamba na mm nasupport aongezewe mda alafu unasema hakuna mwananchi hata mmoja? kwan mmepeleka wap akili zenu, mwaka huu mgumu sana kwenu aisee
 
Achana na kushabikia ccm kabisa. Hiki chama kipo madarakani miaka 60 sasa. Huko tunapokwenda kuomba misaada hawaachii chama kutawala zaidi ya miaka 8 lazima wabadilishe. Sisi tunashabikia chama kimoja miaka 60 halafu tunakwenda kuomba omba, wanatucheka na kutushangaa sana.

Ushabiki wa ccm hapa Tz upo zaidi mikoa iliyo nyuma zaidi kimaendeleo. Ukiendea mikoa ambayo watu wake wana uelewa wa mambo na wapo vizuri zaidi kiuchumi kama vile Dar es Salaam na Kilimanjaro utaona watu walishaachana na ccm kwa kiasi kikubwa. Inashangaza nyie vijana mliozaliwa mkaikuta ccm bado mnashabikia chama hiki ndio maana hatuendelei.

hatuendelei ama wewe ndo hauendelei
 
Hakuna mwananchi hata mmoja anayetaka rais aongezewe muda either wabunge washasoma mchezo kwamba aliyeko madarakani anataka kusifiwa(ili waendelee kuteuliwa kwenye kinyang'anyiro cha kugombea ubunge oct 2020) au "Mtu furani" mwenye ndio anayechagua wimbo wabunge wauuimbe huku yeye akiwa nyuma yao!
Wanataka matumbo yao yaendelee kutuna kama mafurukobe tu hakuna jingine
 
Hakuna mwananchi hata mmoja anayetaka rais aongezewe muda either wabunge washasoma mchezo kwamba aliyeko madarakani anataka kusifiwa(ili waendelee kuteuliwa kwenye kinyang'anyiro cha kugombea ubunge oct 2020) au "Mtu furani" mwenye ndio anayechagua wimbo wabunge wauuimbe huku yeye akiwa nyuma yao!
Hizo takwimu umezichukua lini? sema hataki, ikipigwa referendum hapa the majority wanaichange hiyo katiba asubuhi tu in favor of Magufuli.
 
...ni afadhali atusogeze miaka mingi zaidi...maana nchi yetu ilitafunwa sana! na watafunaji wapo pembeni wana njaa ya kufa mtu wanatamani aondoke hata leo waendelee kuitafuna nchi hii
Na hii ndio weakness ya Magufuli. Badala ya kuandaa na kuhakikisha kuna institutions and means thabiti za kumbana mtu yeyote na genge lake watakaokuja baada ya muda wake kuisha, yeye yupo busy kujijenga yeye. Hatuhitaji watu thabiti saaana wenye tendencies za udikiteta.

Tunahitaji mifumo thabiti ambayo itahakikisha mambo mazuri yanatendeka hata kama Rais ni kilaza. Sasa hivi Magufuli anasamehe wezi majukwaani na sisi (including polisi na mahakama) tunashangilia 😉
 
Back
Top Bottom