WilsonKaisary
JF-Expert Member
- Apr 4, 2017
- 392
- 954
Kwa mujibu wa katiba yetu ya jamhuri wa muungano ya mwaka 1977, theluthi ya wabunge wakisema ndio basi muswada umepita. Na Kama tunavyojua wabunge wa CCM ni wengi bungeni, kwa namna nyingine huu muswada au hii hoja ikienda bungeni maanake imepita.
Swala si JPM aongezewe muda, swala Ni Tanzania inahitaji kiongozi Bora au taasisi Bora? Tanzania inahitaji taasisi imara au kiongozi imara? Tanzania inahitaji mifumo Bora ya Serikali endelevu au tunahitaji kiongozi Bora endelevu?
Kwanza tujue nchi yetu inahitaji Nini. Tukishajua inahitaji Nini itakuwa rahisi kufanya maamuzi yenye maslahi kitaifa. Tunahitaji maamuzi yenye maslahi kitaifa au maslahi ya chama?
Maslahi yenye tija na Bora kitaifa, Ni kubadili kikatiba Uhuru na utendaji Kazi wa mihimiri mikuu mitatu ya serikali Yani bunge, mahakama na serikali Yani Executive.
Wazo la bunge kutaka JPM aongezewe muda halina maslahi kitaifa Bali Lina maslahi ndani ya chama.
Ipate kufahimika wazi JPM ni binadamu nae atakufa, na akifa maanake uongozi wake thabiti umepotea. Ila tukiweka mifumo ya serikali thabiti na taasisi thabiti chini ya sheria thabiti, mifumo hi ya serikali itabaki miaka na miaka. Kuliko kumpachika mtu aendelee kuongoza eti tu kwa sababu Ni kiongozi mzuri na imara, hayo Ni mawazo ya makalioni.
Ashakumu si matusi.
Hitaji la Tanzania si kiongozi imara au benovelant dictator, hitaji la Tanzania Ni mifumo, taasisi na sheria imara na thabiti.
JPM kwa uimara wake inatupasa tumtumie ili kusimika taasisi hizi na mifumo hii. Na si kumuona Kama ndie kiongozi mteule miaka kumi au ishirini mbele au thelathini mbele.
Bunge linapaswa kwanza lipiganie Uhuru wake na sauti yake juu ya mhimili serikali (Executive) na si kupitisha wazo au muswada wa kumtaka JPM azidi kubaki madarakani.
Kisiasa naweza sema anapekeleshwa na mhimili serikali (executive), wakati Ndugai mhimili wake unapaswa kuwa mhimili mama na mlezi wa taasisi zote za serikali Sasa kwake imekuwa vice versa. Tumhenzi Sana marehemu Samwel Sitta.
Bunge pia lingepaswa kuandaa mifumo Bora ya kiutawala na mifumo ya kupata na kuandaa viongozi imara na thabiti Kama JPM, na si kusimamia mtazamo wa kwamba JPM aongezewe muda.
Je, JPM siku akifa maanake ndio hatupata raisi imara Kama yeye? Mazuri yote aliyofanya JPM ndio yatashindwa kuendelezwa? Alipo ishia JPM hapato endelezwa Tena?