Je, ni sahihi sadaka ikatumwa kwa M-Pesa na Tigo Pesa au ni janja janja ya viongozi wa makanisa ya kiroho?

Mzee wa Twitter

JF-Expert Member
Nov 5, 2023
1,278
2,041
Wadau nawasabahi. Kama mada ilivyo kumekuwa na utaratibu mpya kwa makanisa ya kiroho (haya ya watu binafsi kama Kanisa la Gwajima, Mwingira na mzee wa upako n k) kuwatangazia waumini wao kutuma sadaka zao kwa njia ya mpesa Tigo Pesa nk. Utaratibu huo ni tofauti na makanisa ya Lutheran, Roma, Anglican, Moravian n.k.

Kwa uzoefu wangu toka nimeanza kwenda makanisani utaratibu wa kutoa sadaka ni muumini kwenda kanisa muda wa kutoa sadaka ukiwadia waumini wote huenda madhabauni kutoa sadaka zao.

Kutokana na huo utaratibu wa kutoa sadaka kwa mpesa tigo pesa n.k binafsi siuone kama ni sahihi, je mdau mwenzangu je huo utaratibu ni sahihi au ni wizi wa kidini?

Nakaribisha maoni yenu
 
Mtu anatembea kwa miguu sio anavuja bali anamwaga jasho hana nauli lakini ameacha buku tano kwenye kapu la sadaka.

Akifika nyumbani anaomba chumvi kwa jirani na watoto hawana mafuta ya kupakaa anawaambia wapake mafuta ya kula.

Mnaohamasisha sadaka semeni wenye ziada ndio watoe wengine inabidi sadaka ikitoka wapewe palepale wapate nauli na chumvi.

Ahsante
 
Teknolojia imebadirika bakuri na vikapu vya Sadaka na Zaka vimehamia kwenye Simu, unapigwa tu hata uwe wapi ukituma inaingia hio maana yake SIO LAZIMA UENDE KANISANI KANISA LITAKUKUTA HUKOHUKO ULIPO
 
Tuache upumbavu,makanisa haya yanayojiita ya wokovu ni vichaka vya wezi,ujinga ndio mtaji wao mkuu,viongozi wao ni matapeli,wezi,wabakaji(bushiri aka major 1 amekimbia kesi ya ubakaji na utakasaji wa fedha,halafu kuna wapumbavu hapa nchini wanamwamini)
 
Mtu anatembea kwa miguu sio anavuja bali anamwaga jasho hana nauli lakini ameacha buku tano kwenye kapu la sadaka.

Akifika nyumbani anaomba chumvi kwa jirani na watoto hawana mafuta ya kupakaa anawaambia wapake mafuta ya kula.
Mnaohamasisha sadaka semeni wenye ziada ndio watoe wengine inabidi sadaka ikitoka wapewe palepale wapate nauli na chumvi.

Ahsante
Watu wanakamuliwa hadi damu aisee, wanaambiwa kabisa toa ulichonacho hadi nauli. Nina jirani yangu yeye anapeleka hadi mikungu ya ndizi, wakirudi anaanza kusumbua majirani kuomba nyanya na unga....pambavu.
 
Mtu anatembea kwa miguu sio anavuja bali anamwaga jasho hana nauli lakini ameacha buku tano kwenye kapu la sadaka.

Akifika nyumbani anaomba chumvi kwa jirani na watoto hawana mafuta ya kupakaa anawaambia wapake mafuta ya kula.
Mnaohamasisha sadaka semeni wenye ziada ndio watoe wengine inabidi sadaka ikitoka wapewe palepale wapate nauli na chumvi.

Ahsante
Sadaka ya kujiteketeza
 
Hicho ni kipimo tosha kua wachungaji wengi wanathamini Pesa kuliko kondoo
Uchungaji ni ajira.
Wacha weeeeee, mbona wewe wanakutumia nauli pamoja na ya kutolea kwa Mtandao? Unawaambiaga, tuma huku pamoja na ya kutolea ili nije. 😀😃😄😁😆😅🤣😂
 
BN640311.jpg

Bora m pesa na tigo pesa kapu kama hili linatsha sana
 
Mimi si waamini hao mapastor ila zama zinabadilika. Zamani sadaka zililipwa kwa njia ya wanyama na mavuno, ikaja kwa sarafu, sasa kama ni kwa mobole money fresh ni mabadiliko ya nyakati.

Kuna watu wanasema usisome bible kwenye ipad, wanasahau kuwa hata bible ya kitabu wanachosoma si original format ya bible kitabu ni maendeleo ya tech.
 
Teknolojia imebadirika bakuri na vikapu vya Sadaka na Zaka vimehamia kwenye Simu, unapigwa tu hata uwe wapi ukituma inaingia hio maana yake SIO LAZIMA UENDE KANISANI KANISA LITAKUKUTA HUKOHUKO ULIPO
Kwanini WAKUPIGIE wakati kutoa SADAKA ni Takwa la Moyo wako kwani ni DENI? HUO NI WIZI
 
Back
Top Bottom