Je, ni sahihi ndugu Zitto Zuberi Kabwe kuwaita uhamiaji wapuuzi?

Mzalendo-Tz

Member
Apr 19, 2017
81
33
Ndugu wanajamvi wenzangu na wazalendo wenzangu hivi siasa ya nchi hii inawapeleka wapi wanasiasa mpaka kufikia hatua ya kujikuta wao ndio wababe na kujikuta na viburi vya madaraka kwa kutumia umaarufu wao wa kisiasa na kuanza kuzalilisha mamlaka zilizohalali kisheria katika nchi huru na yenye kufuata utawala wa sheria chini ya uongozi shupavu wa Dkt John Joseph Pombe Magufuli…

Ninachokiona hapa kauli ya ndugu mbunge Zitto ya kuwaita UHAMIAJI "wapuuzi" ni ya kuilaani na kuchukuliwa hatua kali za kisheria ili siku nyingine asitokee mwanasiasa mwingine either kutoka chama tawala au upinzani kuidharau mamlaka yoyote iliyopo kwa ajili ya kutumikia wananchi wanyonge na kulinda amani ya nchi yetu iliyotukuka...

Ndugu Zitto anapaswa kujilekebisha na ningependa kuona Jeshi la Polisi linamchukulia hatua kali za kinidhamu....
zitto amejisahau anahisi umaarufu wake ndio chanzo cha kuleta dharau za waziwazi
 
Kama wametekeleza majukumu ya bila weredi wanastahili kuitwa wapuuzi vinginevyo aliyewaita hivyo atakuwa na mapungufu kichwani lazima ubainishe kiini cha kuitwa hivyo Ni nine?
 
Kuna maneno huwa yananipa shida nikiyaona.... 'utawala shupavu' na 'wananchi wanyonge" ni kama ya kutafuta huruma hivi kwa watu wanyonge na sio wengine... kwani wababe sio wananchi wa Tanzania na hawana haki ya kibabe????
 
Mngeanza kusafisha ofisi ya Lumumba kwanza mkianza na kichuguu mngeonekana wa maana.
 
Back
Top Bottom