Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,634
- 697,845
Huruma ya jumuiya ndani ya jamii kuna watu automatically inawakataa, ama inawasuta kama si kuwabeza! Mwenyekiti wa chama cha upinzani aliyeondolewa madarakani ni mmojawapo!
Harakati za mageuzi Tanzania, kumbukumbu na historia yake tangu kuasisiwa 1992, vinaweza kumuangalia kwa makengeza, ama kumtazama kwa jicho chongo kama si kumuona kwa upofu kwa yale yote aliyoutendea upinzani Tanzania na harakati zake
Akiwa na sura mbili na ngozi ya kinyonga, uhalisia wake nyuma ya pazia ulianza kujionesha hadharani mara baada ya uchaguzi mkuu wa 1995 kwenye kikao kilichofanyika hotel ya Mkonge Tanga, wakati huo NCCR-Mageuzi chini ya mrema kikiwa ndio chama maarufu kilichoitikisa vilivyo CCM...
Mwamko wa mageuzi kipindi hicho ndio ulikuwa unajengeka na ufunguo wa motokari ya kukubalika wakakabidhiwa NCCR.. Matumaini ya wananchi waliokuwa wamechoshwa na CCM yote yakahamia NCCR! Lakini kilichotokea pale Tanga Mkonge hotel kiliwaumiza wengi na kuacha doa kubwa jeusi kwenye harakati za mageuzi nchini..!
NCCR ilifitinishwa, ikachonganishwa na kugombanishwa! Na viongozi wakiwa wamepenyezewa mamluki wakakubali kugombanishwa na kufarakana vibaya mno! Ilikuwa ni aibu kubwa kwakuwa ngumi na ugomvi wa kurushiana vitu. Meza nk vilitumika! Uharibifu mkubwa na majeruhi vikatokea! NCCR - Mageuzi chama kilichokuwa tumaini la wengi kikameguka mapande mawili makubwa na mengine madogo madogo
NCCR ya James Mbatia ndio hii iliyodumu mpaka leo hii lakini kikiwa kama joka la kibisa ama umbwa kibogoyo! Mambo yake mengi yalikuwa meusi huku kikiwa kimejaa mashaka kutokana na kuwa kigeugeu ama kuwazunguka wenzake kila nyakati za chaguzi zilipokaribia
Mifano ni mingi kwenye hili tena ya wazi kabisa, na kwenye hayo mambo yote meusi ya kuhujumu upinzani yalipokuwa yakitokea JM alikuwa na mkono wake ama alikuwa ndio kinara mkuu wa michezo ovu
Uchaguzi wa 2015 ulidhihirisha rangi zake kamili, chama kikazidi kupoteza mvuto na kuthibitisha mashaka ya wengi kwamba kiko upinzani kwa ajili ya kuua upinzani wenye nguvu
Dhambi ya usaliti huwa haifi mpaka kiama! Bali humea,hukua na kuzaana! Inapotunga mimba na kupata familia ambayo baadae hugeuka ukoo, hicho kizalia ndio kinakuja kuwa adui wako wa kukumaliza.. Daima kikulacho ki nguoni mwako!
Kutumika hakujaanza leo lakini daima hakuwi na mwisho mwema! JM na chama chake wana madoa mabaya kwenye mabango ya harakati za mageuzi ya kisiasa nchini.. Mwisho wa kutumika ni kuachwa kwa aibu kama usipotii wanavyotaka wao! Ama ukitaka zaidi, ama ukienda nao kinyume!
Sioni haja ya kumhurumia labda tu kwa unafiki wa kawaida wa kibinadamu.. Hii ni asili inachukua mkondo wake! ISIZUIWE MAANA HAIZUILIKI!
Wengine wajiandae asili inakaribia kubisha hodi malangoni mwao! Bado kitambo kidogo tuu.. Najua KZ na HL wananisoma na kunielewa vema! Hii ni asili na asili ni KARMA! Pole JM...!