Wewe mwanasheria bhana. yani post yako ina maana sana, inabidi tume ya warioba ikae pembeni tuunde katiba ya Tanganyika kwanza ndio turud kwenye hiyo ya Muungano.
Haya yote ni Matokeo ya kuizika Tanganyika baada Muungano.
Ila tutaufufua tu.
Hata Kama waliifukia kwenye Kaburi la mita mia moja
kwanza nianze kwa kusema
kuwa mimi siyo mwanasheria. haya ni mawazo yangu ya kawaida. nitashukuru
wanaoifahamu sheria wakiniweka wazi kwa faida ya watanzania wenzangu.
kwanza nampongeza jaji warioba na timu yake kwa kazi nzuri waliyofanya!
rasimu ipo mbele yetu. tuisome watanzania ili tupendekeze marekebisho
katika maeneo ambayo tunaona hayajakaa sawa. kuna maswali najiuliza. 1.
JE NI SAHIHI KATIBA YA MUUNGANO KUITANGULIA KATIBA YA TANGANYIKA?
mmmmhhh! mimi bado nashangaa rasimu ya katiba ya muungano kutangulia
kabla ya ile ya Tanganyika au Tanzania bara kupatikana. Zanzibar wana
katiba yao. Tanganyika haina katiba yake. hamuoni kuwa kutanguliza ya
muungano ni kumfanya MTOTO AZALIWE KABLA YA WAZAZI WAKE? NAULIZA SWALI:
Ina maana ikitungwa ya bara baadaye na baadhi ya maoni yakakinzana na
hii ya muungano, ya muungano itaguswa tena! hamdhani kuwa ya muungano
lazima itaiburuza ya bara iandikwe kwa kufuata vipengele vya hii ya
muungano. hamdhani kuwa ikitungwa ya Tanganyika kutakua na tafrani
kubwa. hivi kazi yetu kwa miaka miwili au mitatu ijayo itakua malumbano
ya katiba? mmmmmhhhh! ka nchi haka kana mambo. 2. JE SIYO KWAMBA HALI
ITAKUA ILEILE YA SERIKALI MBILI KUTOKANA NA KATIBA YA BARA KUBURUZWA NA
ILE YA MUUNGANO? KAMA NI HIVYO TUNAHARIBU PESA ZA NINI? sikatai katiba
mpya lkn ilikua ipatikane katiba ya bara kwanza kisha tuandike katiba
ndogo isiyozidi kurasa 15 inayozungumzia mambo ya muungano ambayo kwa
maoni ya sasa hayazidi 7. hii rasimu, nionavyo ni katiba ya bara
iliyochanganywa na mambo ya muungano! ka nchi haka kana mambo!!!!!!!
naomba kusaidiwa kuhusu maswali yangu wadau!
Serikali ya 'TANZANIA
BARA' imepindekezwa kwenye ile Draft, kama itapitishwa, ina maanisha
kwamba itabidi Katiba ya Muungano isubiri wananchi wa upande wa serikali
isiyokuwepo waunde serikali yao na waanishe mambo yao, mipaka yao, na
miiko yao.
Ndipo ya muungano ifuate, haiwezekekani ya 'Tanzania Bara' itengenezwe
kwa kufuata ya muunhgano, kufanya hivyo itakuwa ni Uboya.