Je ni sahihi katiba ya muungano kuundwa kabla ya ile ya tanganyika?

scramble

JF-Expert Member
Nov 29, 2012
1,593
256
kwanza nianze kwa kusema kuwa mimi siyo mwanasheria. haya ni mawazo yangu ya kawaida. nitashukuru wanaoifahamu sheria wakiniweka wazi kwa faida ya watanzania wenzangu. kwanza nampongeza jaji warioba na timu yake kwa kazi nzuri waliyofanya! rasimu ipo mbele yetu. tuisome watanzania ili tupendekeze marekebisho katika maeneo ambayo tunaona hayajakaa sawa. kuna maswali najiuliza. 1. JE NI SAHIHI KATIBA YA MUUNGANO KUITANGULIA KATIBA YA TANGANYIKA? mmmmhhh! mimi bado nashangaa rasimu ya katiba ya muungano kutangulia kabla ya ile ya Tanganyika au Tanzania bara kupatikana. Zanzibar wana katiba yao. Tanganyika haina katiba yake. hamuoni kuwa kutanguliza ya muungano ni kumfanya MTOTO AZALIWE KABLA YA WAZAZI WAKE? NAULIZA SWALI: Ina maana ikitungwa ya bara baadaye na baadhi ya maoni yakakinzana na hii ya muungano, ya muungano itaguswa tena! hamdhani kuwa ya muungano lazima itaiburuza ya bara iandikwe kwa kufuata vipengele vya hii ya muungano. hamdhani kuwa ikitungwa ya Tanganyika kutakua na tafrani kubwa. hivi kazi yetu kwa miaka miwili au mitatu ijayo itakua malumbano ya katiba? mmmmmhhhh! ka nchi haka kana mambo. 2. JE SIYO KWAMBA HALI ITAKUA ILEILE YA SERIKALI MBILI KUTOKANA NA KATIBA YA BARA KUBURUZWA NA ILE YA MUUNGANO? KAMA NI HIVYO TUNAHARIBU PESA ZA NINI? sikatai katiba mpya lkn ilikua ipatikane katiba ya bara kwanza kisha tuandike katiba ndogo isiyozidi kurasa 15 inayozungumzia mambo ya muungano ambayo kwa maoni ya sasa hayazidi 7. hii rasimu, nionavyo ni katiba ya bara iliyochanganywa na mambo ya muungano! ka nchi haka kana mambo!!!!!!! naomba kusaidiwa kuhusu maswali yangu wadau!
 
Serikali ya 'TANZANIA BARA' imepindekezwa kwenye ile Draft, kama itapitishwa, ina maanisha kwamba itabidi Katiba ya Muungano isubiri wananchi wa upande wa serikali isiyokuwepo waunde serikali yao na waanishe mambo yao, mipaka yao, na miiko yao.
Ndipo ya muungano ifuate, haiwezekekani ya 'Tanzania Bara' itengenezwe kwa kufuata ya muunhgano, kufanya hivyo itakuwa ni Uboya.
 
ndugu yangu unayo akili sana.
_-_-_-_-_-
MAWAZO YANGU
_-_----_--_-_-_
vyema sana Kutunga ya kila Nchi , baadaye ya muungano. Ndio italeta maana ya katiba ya muungano.
 
Wewe mwanasheria bhana. yani post yako ina maana sana, inabidi tume ya warioba ikae pembeni tuunde katiba ya Tanganyika kwanza ndio turud kwenye hiyo ya Muungano.
 
Wewe mwanasheria bhana. yani post yako ina maana sana, inabidi tume ya warioba ikae pembeni tuunde katiba ya Tanganyika kwanza ndio turud kwenye hiyo ya Muungano.

Tume ya warioba ni kwa ajili ya katiba ya muungano,lazima iyundwe tume nyengine kushughulikia katiba ya tanganyika bara.
 
kamanda umeona eeh hatua moja mbele kumi nyuma na kujidnganya tunasonga, haijawahi tokea mtto kuja mwanzo kuliko wazee, haya ni maajabu ya dunia Tz tunahitaji kuingizwa the Giness hahaaaaaa!aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa?:heh:
 
Mie siyo Mwanasheria pia. Kwa hali iliyopo ni SAHIHI katiba ya Muungano ipite ndipo ya kipenzi Tanganyika ifuate kwa sababu:
Katiba iliyopo inatambua serikali mbili, hakuna njia ya kuanzisha katiba ya Tanganyika hadi katiba hii ifutwe na katiba mpya. Katiba mpya inatambua kuanzishwa kwa serikali ya Tanganyika hivyo hakuna tatizo. Cha msingi kN 'Tanzania Bara' kiondoshwe na nomino 'Tanganyika'.
 
Haya yote ni Matokeo ya kuizika Tanganyika baada Muungano.
Ila tutaufufua tu.
Hata Kama waliifukia kwenye Kaburi la mita mia moja
 
Mtoto hawezi kuzaliwa kabla ya wazazi.
Wazazi ni katiba ya Muungano then zinazaliwa Zanzibar na Tanganyika.
Hii ni kwa kuwa huwezi kutunga katiba nje ya Muungano.
Nampongeza sana Jaji Warioba na tume yake !
 
inawezekana Rais alikurupuka na hakujua matokeo yake. na ndio maana watoa maoni karibu wote walitoa maoni ya katiba ya Tanzania. Warioba kaja na rasimu ya Muungano. Tanganyika kwanza.
kwanza nianze kwa kusema
kuwa mimi siyo mwanasheria. haya ni mawazo yangu ya kawaida. nitashukuru
wanaoifahamu sheria wakiniweka wazi kwa faida ya watanzania wenzangu.
kwanza nampongeza jaji warioba na timu yake kwa kazi nzuri waliyofanya!
rasimu ipo mbele yetu. tuisome watanzania ili tupendekeze marekebisho
katika maeneo ambayo tunaona hayajakaa sawa. kuna maswali najiuliza. 1.
JE NI SAHIHI KATIBA YA MUUNGANO KUITANGULIA KATIBA YA TANGANYIKA?
mmmmhhh! mimi bado nashangaa rasimu ya katiba ya muungano kutangulia
kabla ya ile ya Tanganyika au Tanzania bara kupatikana. Zanzibar wana
katiba yao. Tanganyika haina katiba yake. hamuoni kuwa kutanguliza ya
muungano ni kumfanya MTOTO AZALIWE KABLA YA WAZAZI WAKE? NAULIZA SWALI:
Ina maana ikitungwa ya bara baadaye na baadhi ya maoni yakakinzana na
hii ya muungano, ya muungano itaguswa tena! hamdhani kuwa ya muungano
lazima itaiburuza ya bara iandikwe kwa kufuata vipengele vya hii ya
muungano. hamdhani kuwa ikitungwa ya Tanganyika kutakua na tafrani
kubwa. hivi kazi yetu kwa miaka miwili au mitatu ijayo itakua malumbano
ya katiba? mmmmmhhhh! ka nchi haka kana mambo. 2. JE SIYO KWAMBA HALI
ITAKUA ILEILE YA SERIKALI MBILI KUTOKANA NA KATIBA YA BARA KUBURUZWA NA
ILE YA MUUNGANO? KAMA NI HIVYO TUNAHARIBU PESA ZA NINI? sikatai katiba
mpya lkn ilikua ipatikane katiba ya bara kwanza kisha tuandike katiba
ndogo isiyozidi kurasa 15 inayozungumzia mambo ya muungano ambayo kwa
maoni ya sasa hayazidi 7. hii rasimu, nionavyo ni katiba ya bara
iliyochanganywa na mambo ya muungano! ka nchi haka kana mambo!!!!!!!
naomba kusaidiwa kuhusu maswali yangu wadau!
 
nilazima kwanza katiba ya Tanganyika bila hivo ni kumaanisha hakutakuwepo na dola hata ya kusimamia mchakato wa hio katiba ya Tanganyika
Serikali ya 'TANZANIA
BARA' imepindekezwa kwenye ile Draft, kama itapitishwa, ina maanisha
kwamba itabidi Katiba ya Muungano isubiri wananchi wa upande wa serikali
isiyokuwepo waunde serikali yao na waanishe mambo yao, mipaka yao, na
miiko yao.
Ndipo ya muungano ifuate, haiwezekekani ya 'Tanzania Bara' itengenezwe
kwa kufuata ya muunhgano, kufanya hivyo itakuwa ni Uboya.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom