Je, ni nini kinacholitesa a taifa hili kwa sasa?

Hata hao unaowasema walishajichokea,
1.SSIT ni taaluma yenye heshima.
Unamwingiza kada afanye kazi zisizo zake na huku alishafiji kitambulisho cha fani hiyohiyo.
2.Makada wawe wanawanunua upinzani kwa bei na kwa amri toka juu.

KATIBA KATIBA KATIBA
Mi nawaomba watusaidie jamani najua tunawalipa kwa kodi zetu
Hebu watekeleze majukumu yao kwa weledi wailinde nchi.
Mbona haya waliyaweza wakati ule? Umaarufu wote wa Baba ilikuwa ni wao nyuma yake
Wanakwama wapi wakati huu tunapowahitaji?
 
Karibuni tuyabainishe sote labda viongozi watafunguka akili karibuni.
Watanzania tulio wengi ni "Mazuzu" kwa tafsiri ya Professor aliyesema Muhimili mmoja wa Nchi umejaa Mazuzu (Kwa maana nyingine hatujitambui).

Pili, asilimia kubwa ya walio ktk nafasi za maamuzi ya maendeleo ya Nchi na Watu, hawawajibiki itakiwavyo sababu ya kukosa weledi wa kazi na wengine kukosa sifa za kuwa kiongozi, badala yake wanatanguliza maslahi binafsi na familia zao.

Tatu, Chombo kimoja kati ya Mihimili hii mitatu Tanzania, kinatia aibu kwa kukanyaga waziwazi sheria na kukandamiza watu ili tu kimfurahishe Kiongozi mmoja wa muhimili mmojawapo.

Hembu tuyadadavue haya.
 
Ukiona ktk TAIFA lolote watu wake wanaexperience ugumu wa maisha kwa wakati wote basi ni wazi kwamba kuna ombwe kubwa sana la uongozi lisiloelezeka.kuna mambo wanaaminishwa watanzania ni vichekesho vitupu,Yaani watu wanakaa mezani wanapanga mgao wa umeme,kuna wakati huwezi kuelewa ni maslahi ya aina gani ambayo viongozi wetu wanayatafuta,SWALI KUBWA NA LA MSINGI NI HILI:JE NI NANI MTETEZI WA WATANZANIA KTK OMBWE HILI.Yawezekana uongozi unajisifu sana ili kublind watu hali wanajua kuwa hali ni mbaya sana Kule mitaani.NI BAHATI MBAYA SANA KWAMBA VIONGOZI WETU HAWAJUI HATA KIDOGO TU MAMBO MSINGI YANAYOWAKERA WATANZANIA.WAO BADALA YA KUJIBIDISHA KURAHISISHA MAISHA YA WATANZANIA WAMEVUMBUA MBINU YA KUFANYA MAISHA YA WATANZANIA KUWA MAGUMU ZAIDI.SABABU KUBWA NI WATU WENYE AKILI NDOGO KUPEWA UONGOZI WA NCHI NA HIVYO INAKUWA SI RAHISI SANA WAO KUTAMBUA UGUMU WA MAISHA YA WATANZANIA.UKICHEZEA MAISHA YA WATU KWA MANUFAA YA KUNDI DOGO LA VIONGOZI WAFANYABIASHARA NI SAWA NA KUFANYA SARAKASI KTK TRANSFOMER YENYE UMEME MKALI ITAKAPO LIPUKA SIJUI KAMA USALAMA UTAKUWEPO.VIONGOZI WA SERIKALI YA CCM NI VIZURI KUJITATHIMINI YAWEZEKANA TUNACHOKIAMINI KUHUSU WATANZANIA SIO CHA KWELI.YAWEZEKANA SIKU MOJA KTK MAISHA YETU TUKAISHI UHAMISHONI.TUJITAFAKARI.
 
Hebu na mie niandike walau kidogo tena kwa uchungu wa kulia kabisa
Kuna watu pahala wanazembea(sina neno mbadala) kumsaidia mama na lawama hii naielekeza kwanza ni TISS
TISS mna mikono hodari macho yenye lenzi kali lakini mmeshindwa kumsaidia mama
Watu wanatuchezea Watanzania kabisa nawambia. Sina ushahidi wowote lakini kabisa nawaeleza roho wa Mungu kuna kitu ananiambia kwamba haya yanayoendelea ni hujuma.
Haiwezekani leo tu eti mabwawa hayana maji kwahiyo umeme wa mgao
Leo tu mala eti hakuna maji dar na dodoma
Leo tu gafla sijui hiki sijui kile ....
Hizi makitu mbona hazikuwepo wakati wa Baba?
Nawaomba sana nyie watu saidieni nchi isonge mbele waonaotuhujumu mnawajua mwogopeni Mungu jamani tusaidieni Watanzania
Mkiamua mnaweza basi roho wa Mungu awape kutenda kwa hekima mkitanguliza maslahi ya wanyonge.
Tatizo la maji ni nchi nzima.

Karibia mikoa yote idara za maji zimetoa notification kwa wateja wake kwamba kutakuwa na ukatikaji wa maji usiojulikana mwisho wake kutokana na mgao wa umeme.

Huduma zitarejea pindipo umeme utakapotengemaa, kwani mitambo yao inategenea umeme wa grid.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SiAsa Chafu alizopandikiza mwendakuzimu.

siasa chafu ndio zinafanya mpaka sasa hujaoga siku ya tatu.

nyinyi mnaoshindwa kukubali mchango wake ndio mnafanya nchi inaandamwa na mikosi kila kukicha,amefariki badala maisha yenu yabadilike bado mnanuka njaa na ufukara usiomithirika.
 
Karibuni tuyabainishe sote labda viongozi watafunguka akili karibuni.
Kiburi
Screenshot_20211119-123449.jpg
 
siasa chafu ndio zinafanya mpaka sasa hujaoga siku ya tatu.

nyinyi mnaoshindwa kukubali mchango wake ndio mnafanya nchi inaandamwa na mikosi kila kukicha,amefariki badala maisha yenu yabadilike bado mnanuka njaa na ufukara usiomithirika.

Yeye ndio alitutia ufukara, ni bora hayupo.
 
Mi nawaomba watusaidie jamani najua tunawalipa kwa kodi zetu
Hebu watekeleze majukumu yao kwa weledi wailinde nchi.
Mbona haya waliyaweza wakati ule? Umaarufu wote wa Baba ilikuwa ni wao nyuma yake
Wanakwama wapi wakati huu tunapowahitaji?
Mtoto asipolia hatanyonyeshwa. watume nao wataitikia ukikaa kimya kwa ajili ya kulinda maslahi yako nao watakuacha.
 
Back
Top Bottom