Je, ni nini hasa faida ya kuoa?

Je, ni nini hasa faida ya kuoa?

Joined
Jun 11, 2020
Posts
44
Reaction score
61
Habari wakuu,

Mimi ni kijana niliyefikisha umri wa kuoa nina 27 kwa sasa, ni kwamba familia na jamii inayonizunguka naona wananisisitiza sana nioe eti kwakuwa nina kazi nzuri na ninajimudu kimaisha. Lakini kwa mtazamo wangu sioni ka kuna ulazima katika hili ukizingatia chochote ninachokitaka naweza kukipata kwa wakati kwa sasa, asa kwanini nijibebeshe mzigo?

Naombeni ushauri zaidi wadau katika hili huenda naweza shawishika nikabadili mtizamo wangu
 
Kuoa ni mpango wa Mungu. Mwanamume anashauriwa kuoa na kujenga familia.
Mpango huu unacover mambo mengi sana katika maisha ikiwa ni pamoja na mafanikio na kuishi katika mpango wa Mungu.
Ndani ya ndoa kuna mambo mengi ambayo yatafanikiwa endapo utadumu ndani ya ndoa. Familia ndani ya ndoa zitaishi kwa furaha zaidi wa wale wa nje ya ndoa......
 
Habari wakuu
Mimi ni kijana niliyefikisha umri wa kuoa Nina 27 kwa sasa, ni kwamba familia na jamii inayonizunguka naona wananisisitiza sana nioe eti kwakuwa Nina kazi nzuri na ninajimudu kimaisha. Lakini kwa mtazamo wangu sioni ka kuna ulazima katika hili ukizingatia chochote ninachokitaka naweza kukipata kwa wakati kwa sasa, asa kwanini nijibebeshe mzigo

Naombeni ushauri zaidi wadau katika hili huenda naweza shawishika nikabadili mtizamo wangu
Kiroho ina thamani kubwa sana,ni moja ya sakramenti/nguzo ambazo binadamu lazima uzipitie na ina Baraka zake duniani na mbinguni pia...
 
Una baba na una mama

Kama ulilelewa na single mother rudi tena kwa mama yako muulize "Ipi hasara ya kulea mtoto ukiwa single mother?"

Kama baba na mama yako waliishi katika ndoa mfuate baba yako, nenda umdhihaki kuwa kwa nini baba ulikuwa mjinga? Kwamba ulifuata nini kumuoa mama wakati ulikuwa na uwezo wa kupata chchote kipatikanacho katika ndoa.

Andika majibu watakayokupa tuchangie. Hongera kwa ukamilifu wa kuweza kupata chochote.
 
Back
Top Bottom